Mkuu
Tuko hii ni rasimu ambayo itajadiliwa na makundi ambayo yameanishwa kwenye sheria ya mabadiliko ya katiba.
Kumbuka kuna mabadiliko tena yatafanyika kulingana na jinsi vikundi/makundi yatakavyo pendekeza ambapo bunge la katiba ndilo litakalo pitisha hii sheria mama.
Mpaka sasa hatujajua na wajumbe wa tume hawajajua kwa uhakika ni serikali ngapi zitakuwepo, kwa maana hiyo, huwezi kuanza kutafuta katiba kwa serikali ambazo hazipo na hazijulikani kama zitakuwepo. Kufanya hivyo, ni kujichukulia madaraka ya kidikteta na kuonyesha haya siyo mapendekezo bali ndiyo sheria yenyewe.
Kinachojulikana ni kwamba, kutakuwa na serikali ya Muungano na hii ni rasimu ya sheria mama kwa serikali zozote zitakazo kuja.
Kuna watu wanafikiri ngoma ndiyo imeisha wakati ngoma ndiyo inaanza kabisa. Kazi ngumu ndiyo inaanza ambapo kwa sasa makundi katika jamii atleast, yameona mwelekeo wa katiba mama utakuwaje.
Mvulugano na mvutano wa kimaslahi ndiyo unaanza. Tegemea maandamano kwa wingi na kipigo cha polisi!!.