Lakini mkuu, ukumbuke kwamba Jaji Warioba alisema, namnukuu, "Tume ilifikia uamuzi wa kupendekeza mfumo wa Serikali tatu. Yaani Serikali ya Shirikisho, Serikali ya Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar."
Angalia vizuri ktk rangi nyengundu, tume inapendekeza serikali ya "Tanzania Bara." Imekwepa kusema "Tanganyika." Kwa nini? Labda tushauri kwanza kwamba katika rasimu warekebishe mahali hapo ili pasomeke kwamba "Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar." La sivyo, jina litakalorejeshwa kwa bara litakuwa hilo lililopendekezwa na tume.