Rasmi Dar yakumbwa na uhaba wa Maji, RC Makalla athibitisha uwepo wa Mgao

Ndio tatizo la kuwa na viongozi wasanii na sio wana sayansi kama Magufuli.
 
Hapo tumeambiwa tusubiri mvua inyeshe, ndo imeisha hiyo.

Sent from my SM-M115F using JamiiForums mobile app
 
Binafsi naona kama serikali ya ccm wangejenga reservoir kwenye mto wami,wangeweza kufua umeme na kupata maji ya kutumia Dar.
Lile bonde lilipo daraja jipya maeneo hayo yana kina kirefu ambayo yangeweza kuhifadhi maji ya kutosha jiji la Dar es salaam
 
Kukosekana chanzo cha uhakika cha maji dar es salaam ni kujitakia, kilomita 180 kutoka katikati ya jiji mpaka kufika daraja la mto rufiji kuna maji yanatiririka mamilioni ya lita kuingia baharini, hata siku moja sijasikia mpango wa kuhamisha yale maji yaje dar
 
Wizara ya maji lazima sasa ibadilike, isiwe inategemea chanzo kimoja tu cha maji (mto ruvu) ambao chanzo chake ni mvua, mvua zikiwa chache uhaba wa maji unaongezeka.

Wizara Ichimbe visima virefu ili visima hivyo viwe vinaokoa jahazi wakati wa ukame kama huu.

DAWASA inakusanya mapato ya kutosha hivyo wataalamu wake lazima wakune vichwa kuangalia njia mbadala
 
Kwa akili Zangu za kawaida nilizojaaliwa kiwa nazo ninawaza haya yafeatayo;

(1) 99% of tap water in Dubai comes from desalination plants. Kimsingi dubai inapata 99% ya mahitaji yake ya maji, kutoka baharini.

Sisi bahari tunayo lakini tunaiangalia tu. Dar es salaam ni commercial hub ya nchi, ni mkoa muhimu sana, haiwezekani mpaka leo tumekosa wataalamu wakutusaidia kuondokana na adha hii.

(2) sea water, Dar es salaam ina ground water aquifer kubwa kule kimbiji, je hii haiwezi kuwa altenative source ya maji kwa mkoa wa Dar es salaam, kwa kipindi kama hiki chenye uhaba wa maji?

(3) Rain water harvesting: Kuna kipindi nilisikia kulikua na mpango wa serikali kujenga mabwawa makubwa ya kukusanya maji yatakayovunwa wakati wa mvua, ili maji hayo yatunzwe kwaajili ya matumizi ya kawaida nyakati za shida ya maji. Wazo hili ni zuri ila sijui liliishia wapi.

(4) Recycling of sewage water for domestic use. Haya maji ya vyooni yanayojazwa na malori ya maji taka, kwenye oxidation ponds kama zile za mikocheni mabwawani, alafu yanatiririshwa kwenda baharini, badala ya kutiririshwa kwenda baharini yangekuwa ya akuwa recycled, treated, then yanaingizwa kwenye mfumo wa usambazaji maji Dar es salaam ili yaweze kutumika majumbani, yangesaidia sana nyakati kama hizi za ukame. Hili linawezekana kabisa na linafanyika sehemu nyingi tu huko duniani.

Tanzania tuache blah blah, its time tuwe serious na mambo ya msingi katika maisha yetu, sio kuwa bize kubeti na kucheza singeli kwenye mikutano ya siasa.
 
Aweso ataenda tena kutafuta maji na gumboots asivyokuwa na akili. 2035 Dar itakuwa na watu milioni 12 maji si itabidi yauzwe sheli?
 
Hatutaki maji yetu ya mikoani myachukue. Safisheni ya bahari mkishindwa kunyweni kiswahili au maghorofa yenu
 
Hakuna sera zozote za utunzaji wa mazingira huko Morogoro
 
Hivi hamna mechanism yoyote kisayansi kutumia maji ya bahari na kuyageuza kuwa maji salama kwa matumizi ya mwanadamu,?

Miaka nenda rudi wanasayansi wamekwama wapi?
Mkuu waarabu ndo maji wanayitumia hada dubai huwezi sikia kuna mgao wa maji ...njooo mwetu sisi kina mwajuma ndala ndefu mto rufiji tu unamwaga mwaji kibao baharini lakini huku sisi tunalia na mgao wa maji ...hushangai km mwanza wanalia mgao na maji yapo pua na mdomo ....
 
Nchi ya kipumbafu hawataki hii kitu

Seawater Desalination
 
Hapa nilipo hatuna maji kwa week 2 sasa. Imebidi tuagize watu wa tank walete kwa sh 15 elf
 
Nchi ya maziwa matatu inalalamikia ukame dunia ya leo? Hivi kama 'think tank' zimechoka huko kwenye system si mpishe damu changa aisee?
Yani kuna mambo yanakera kupita maelezo.
Maana ya kuwa na ziwa Victoria, Tanganyika na Nyasa ni nini sasa?
 
Kyela na kigoma wanalalamika maji hii nchi ya mazombi..
 
Hivi hamna mechanism yoyote kisayansi kutumia maji ya bahari na kuyageuza kuwa maji salama kwa matumizi ya mwanadamu,?

Miaka nenda rudi wanasayansi wamekwama wapi?

Inawezekana kwa kufanya desalination, ni technology inayotumia nishati kubsa (energy intensive)
Nchi za kiarabu kama Saudi Arabia, UAE, Oman na nyinginezo pia hata Israel wameweza kufanya kwa kutumia gas kuzalisha umeme kufua maji ya chumvi
Hapa gas ya Mtwara ingeweza kusadia
 
Hivi misri wanakuwaga na uhaba wa maji kwao?

Ova
 
Kwa hiyo kaishia hapo.
Hawajali kwa sababu wanajua Rais hawezi kufanya kitu.
Maisha yangu yote sitakuja kumsahau JPM .....kwa hakika Makala angeshatumbuliwa asubuhi tu..hayuko serious...
Hivi kwanini wafuasi wa Jiwe akili zao ni kama zako?
 
Enzi ya JPM kulikuwa hakuna shida ya maji Dar es salaam? Au ngekuwepo yeye angefanya maji yaongezeke mto Ruvu ili uzalishaji upande toka 64% hadi 100%?
Angekuja na propaganda au vyombo vy habari visingeruhusiwa ku report hiyo habari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…