Rasmi: Kibu Dennis ni Mtanzania

Rasmi: Kibu Dennis ni Mtanzania

Cambodian

Member
Joined
Sep 6, 2021
Posts
24
Reaction score
60
Tutegemee kumuona Kibu akivaa tena jezi ya Taifa baada ya sakata lake kuisha.
===

Chibu Denis (kushoto) akiwa katika kikosi cha Taifa Stars. Kulia ni John Bocco
WAZIRI wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, George Simbachawene, amehitimisha sakata la uraia wa Kibu Denis Prosper kwa kutangaza kumpa uraia mchezaji huyo wa Simba. Anaripoti Damas Ndembela, TUDARCo … (endelea).

Simbachawene ametumia mamlaka aliyopewa kwa mujibu wa Sheria ya Uraia, Sura ya 357 (Rejeo la 2002), kumpa uraia Kibu.

Uamuzi huo umetangazwa usiku wa Jumamosi tarehe 2 Oktoba 2021 kupitia ukurasa wa kijamii wa Twitter wa wizara hiyo uliyoweka picha ya Kibu na maneno yaliyosomeka;

“Mamlaka aliyopewa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, kwa mujibu wa Sheria ya Uraia, Sura ya 357 (Rejeo la 2002), baada ya kupokea ombi lililoletwa kwake na TFF, amempa URAIA wa Tanzania Mchezaji wa Mpira wa Miguu, Kibu Denis Prosper, Sept. 30, 2021.”

Waziri Simbachawene ametangaza uamuzi huo ikiwa imepita siku moja tangu, Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe kuibuka na kumtaka, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuingilia kati suala hilo akidai linatia aibu Taifa.

Mbali na Majaliwa, Zitto aliwatupia mzigo Waziri Simbachawene na Innocent Bashungwa, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo akisema, wakiamua wanaweza kuhitimisha suala hilo ndani ya siku moja.

Zitto aliibuka kuzungumzia suala hilo alipofanya mahojiano maalumu na MwanaHALISI TV na MwanaHALISI Online akishangazwa na uamuzi wa Serikali kushikilia hati ya kusafiria ya Kibu ambaye amesajiliwa Simba msimu huu akitokea Mbeya City.

Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT Wazalendo
Mwanasiasa huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) alisema, ilikuwaje Kibu akacheza Mbeya City, timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars “hakuulizwa uraia, ila amesajiliwa tu Simba anaulizwa uraia.”

Kibu anayevalia jezi namba 38 aliyopewa baada ya kusajiliwa Simba, aliicheza Taifa Stars kwa mara ya kwanza kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Malawi, tarehe 13 Julai 2021, uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa na Stars kuibuka na ushindi wa 2-0.

George Simbachawene, Waziri wa Mambo ya Ndani
Kwenye mchezo huo, Kibu anayecheza nafasi ya ushambuliaji, alionesha kiwango kinachoridhisha na kuwezesha ushindi huo na baadaye akizungumza na waandishi wa habari alisema “nashukuru sana kwa mara ya kwanza kuichezea timu yangu ya Stars. Wazidi kunipa moyo kwani safari bado ndefu.”

Baada ya uamuzi huo wa Serikali, Zitto ameandika kwenye Instagram yake akipongeza uamuzi huo akisema “nazishukuru na kuzipongeza mamlaka za uraia.”
 
Kama namuona m2 flan🤓
 

Attachments

  • twitter_20211002_230950.mp4
    37.7 KB
Tunajitia Aibu Sana Hili Taifa. Ni bora wasinge Tangaza Chochote na Wangemuonya Kibu Denis kutokusema Chochote. Wangempa Uraia Kimyakimya Kumpa Uraia kwa Matangazo hivi wanaiabisha sana hii nchi Yetu.

Kuna Maswali Zaidi ya 100 kwenye hili sakata Vs Wahamiaji Haramu wanaokamatwa kila siku Vs sheria za Nchi.

1. Apewa Uraia Wa Tanzania Kutoka Uraia Wa nchi Gani?

2. Nchi Gani Ililalamika Kuwa Kibu Denis Ni Raia Wao?

3. Ameshacheza Mechi Ya Timu Ya Taifa na kufunga Goli, Alicheza Kama Raia wa Wapi? Na CAF na FIFA illimtambua Kama Raia Wa Wapi? Tufutiwe matokeo? Yale aliyocheza Kibu Denis?, kafu Watuchukulie hatua kwasababu tulichezesha Raia sio wa Kitanzania?

4. Kwa miaka Yote Aliyocheza Ligi Kuu Tanzania Bara Alicheza Kama nani? Kama Raia Wa Nchi Gani?

5. Miaka Yote aliyo ishi Tanzania Ameishi kama Raia Wa Nchi Gani? Alipewa PR visa? Working Visa? Sturdy Visa? Au alipewa nini?

6. Katika Haya Yote kwa miaka Yote viongozi walikuwa wapi?

7. Kusajiliwa Simba Ndio Sababu Ya hili sakata?

Yaani mambo ni Mengi kiufupi hii nchi ni ngumu sana.
 
Tunajitia Aibu Sana Hili Taifa. Ni bora wasinge Tangaza Chochote na Wangemuonya Kibu Denis kutokusema Chochote. Wangempa Uraia Kimyakimya Kumpa Uraia kwa Matangazo hivi wanaiabisha sanaaa hii nchi Yetu...
Wewe usiteseke sana. Jua tu Kibu Denis ni Mtanzania na Mchezaji halali wa Simba Sports Club! Basi!!!!
 
wale jamaa wenye usongo na kombe miaka 4 waliweka figisu uhamiaji, kama angebaki mbeya city wala hakuna ambaye angehangaika naye
Unatakuwa basi uwashukuru uhamiaji na hao Yanga kwa kuwaumbua TFF na mamlaka nyingine za nchi kwa kushindwa kumbaini mhamiaji haram kiasi cha kujipenyeza mpaka kuchezea timu ya Taifa.
 
We kweli huna akili kama alivyosema msukule wenu manara ukiachana na mzee kikwete na mzee manara
nyie uto hamkuliona hili kwamba sio raia wa tanzania alipofunga goli na kuasist dhid ya malawi ndio mlione aliposajiliwa na simba?
Unatakuwa basi uwashukuru uhamiaji na hao Yanga kwa kuwaumbua TFF na mamlaka nyingine za nchi kwa kushindwa kumbaini mhamiaji haram kiasi cha kujipenyeza mpaka kuchezea timu ya Taifa.
 
We kweli huna akili kama alivyosema msukule wenu manara ukiachana na mzee kikwete na mzee manara
nyie uto hamkuliona hili kwamba sio raia wa tanzania alipofunga goli na kuasist dhid ya malawi ndio mlione aliposajiliwa na simba?
Unaleta ushabiki maandazi kwenye mambo ya msingi. Pole sana.
 
Nilidhani taarifa ya waziri ingeanza na neno "imethibitishwa" na siyo "amepewa"

Taarifa ya Waziri inatupa uthibitisho kwamba Kibu hakuwa raia wa Tanzania Ila sasa amepewa uraia kutokana na maombi maalumu.

Kama CAF na FIFA wataipata hii taarifa, kuna uwezekano mkubwa tukapoteza point za michezo yetu ya nyuma.
 
Unatakuwa basi uwashukuru uhamiaji na hao Yanga kwa kuwaumbua TFF na mamlaka nyingine za nchi kwa kushindwa kumbaini mhamiaji haram kiasi cha kujipenyeza mpaka kuchezea timu ya Taifa.
Hao yanga walikuwa wapi siku zote
 
Hata sisi ni rahisi tu..nina wasiwasi na uraia wa fei toto anafanana na raia wa visiwa ya comoro.
 
Nilidhani taarifa ya waziri ingeanza na neno "imethibitishwa" na siyo "amepewa"

Taarifa ya Waziri inatupa uthibitisho kwamba Kibu hakuwa raia wa Tanzania Ila sasa amepewa uraia kutokana na maombi maalumu.

Kama CAF na FIFA wataipata hii taarifa, kuna uwezekano mkubwa tukapoteza point za michezo yetu ya nyuma.

Waziri anasena eti Kibu anacho kitambulisho cha Uraia!

Kuna Mtanzania ana kitambulisho cha uraia??

Labda angesema kitambulisho cha Taifa na si cha Uraia kwani yeye mwenyewe Waziri alishasema Kitambulisho cha Taifa anapewa mtu yeyote akiwemo mgeni.
 
Tunajitia Aibu Sana Hili Taifa. Ni bora wasinge Tangaza Chochote na Wangemuonya Kibu Denis kutokusema Chochote. Wangempa Uraia Kimyakimya Kumpa Uraia kwa Matangazo hivi wanaiabisha sanaaa hii nchi Yetu...
Utopolo wana chuki za ajabu sana, tulishawaachia Mapinduzi cup ili wawe wanajifariji kila season lakn hawatosheki.

Sasa vikombe vyote msimu huu wataambulia sifuri
 
Mimi naona ingepigwa propaganda ya kuwa ni mtanzania afu kimya kimya akapewa uraia

Taarifa aliyoitoa Waziri Anazidi Kujichanganya Tuuu.

Anasema Kibu Denisi Wazazi Wake Walikuwa ni Wacongo waliingia nchini kwa kukimbia Mapigano CONGO wakati Kibu Denis Akiwa na Umri Wa Miaka 6.

Baadae Wazazi wake Sijui walifariki lakini anasema Kibu denis alikuwa na nyaraka zote za Kuwa mtanzania na kwa alikulia Tanzania Akajua yeye ni mtanzaniaa kwasababu wazazi wake wakati wanaingia Tanzania Yeye alikuwa hajui chochote!

Najiuliza Ina maana Mtoto wa Miaka 6 hajui chochote hata kujua kuwa tumetoka hapa kwenda hapa kwasababu ya Mapigano? Waziri anasema Kibu Denis yupo Tanzania Toka Mwaka 1998 inamaana alikuwa hajijui? Taifa hili tunachekesha sana.
 
Back
Top Bottom