Rasmi: Kibu Dennis ni Mtanzania

Rasmi: Kibu Dennis ni Mtanzania

Rais Samia ampa Uraia Kibu Denis Prosper mchezaji machachari wa Taifa Stars na Simba | Hakika hii ndio Serikali rafiki wa michezo na wanamichezo wote​


View attachment 1962626
Aisee,

Hii kitu iliniuma sana, Yanga wanafitina sana,
Asante Sana Rais mpenda wanamichezo Sisi Simba tumefurahi sana kwa hili,

Mungu akulipe yaliyo mema mama yetu,
Yanga mjiandae
 
.... aliyetoa uraia kwa huyo kijana kwa mujibu wa sheria za nchi ni Rais au Waziri? Hivi mkinyoosha maelezo mnakosa nini?
 
MOD, peleka mawazo haya jukwaa la michezo.
 
Hili nalo ni jambo kubwa kitaifa?? Au una matatizo ya akili?
Mtoa mada hajui hata tatizo kubwa la maisha yake ni nini. Ukimuuliza, leo kalala kwa raha ya mcheza mpira ingawa ameshinda na muhogo mkononi. Viumbe wa aina hii ktk kampeni wanapewa kofia tu!
 
Nifitna tu za Yanga
Sio fitina ni uzembe wa wizara ni kweli uraia wake ulikuwa na walakini wao wizara walishindwaje
kugundua hilo mapema na kulimaliza hadi
amekuwa mchezaji mkubwa , na sasa wanataka tuwaone ni mashujaa kwa kutatua uzembe wao
 
Sio fitina ni uzembe wa wizara ni kweli uraia wake ulikuwa na walakini wao wizara walishindwaje
kugundua hilo mapema na kulimaliza hadi
amekuwa mchezaji mkubwa , na sasa wanataka tuwaone ni mashujaa kwa kutatua uzembe wao
kibu ni Mtanzani kitambo kama ulivyo wewe,

Shida ni Ujadi tu wa Simba na yanga,

Ashukuriwe Rais kwa kumaliza hili,
 
Hii taarifa wala sio ya kimichezo pekee,

Inaswitch kote kote
Hili ndo tatizo lako ktk maisha? Mbona wa-TZ tunakuwa na ufahamu mdogo kiasi hiki? Kwa hiyo Samia kawa rais bora kwa kutoa uraia kwa mcheza mpira? Akili kama hizo, CCM itatawala milele maana siku ya kura utapewa pilau tu!
 
Back
Top Bottom