Rasmi: Kisinda ruksa kuichezea Yanga

Rasmi: Kisinda ruksa kuichezea Yanga

Kambole Alikuwa Hajapata Timu, Kitu kilicho Fanya Yanga Kuendelea Kusomeka Kuwa na Wachezaji 12 wa Kigeni. Na Mwanzo Yanga Hawakuwa katika Mpango wa Kuachana Na Kambole. Mpango wa Kuachana na Kambole Umekuja Baada Ya TFF kuwashauri kuwa Waachane na Mchezaji Mmoja Ndio Yanga Wakaona Wamtoe Kafala Kambole. TFF isingeweza Kubariki Uhamisho wa Kisinda wakati KAMBOLE HAJAPATA timu.
Unakiherehere
 
Unakiherehere

Tatizo Linakuja Pale ambapo Mkipewa Utaratibu mnahisi Kuonewa.

Na Simba na Yanga Ndio Timu zinazotumia Mashabiki Kuipa Pressure TFF, Hili Jambo Lingetokea IHEFU usinge sikia Hizi Kelele.

Tulieni na Fuateni Utaratibu muache kuhisi Kila Kitu mnaonewa
 
Nakumbuka hili swala wakati linaongelewa mwenyekiti wa kamati ya mashindano yanga alisema kila kitu Hadi Itc imefika tayari.

Sasa wewe ni nani kuleta taarifa kuwa Itc haikuwa imefika?
 
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imepitisha usajili wa Twisila Kisinda kuichezea Yanga baada ya klabu hiyo kumuhamisha mchezaji wake wa kigeni Lazarous Kambole.

Awali Kamati hiyo ilizuia usajili wa Kisinda licha ya kuwa ulifanyika ndani ya dirisha la usajili kwa vile tayari Yanga ilikuwa na wachezaji 12 wa kigeni.

Licha ya changamoto hiyo, pia Kisinda aliombewa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ambayo tayari imepatikana.

Hivyo kwa kumuhamisha Kambole imepata nafasi ya kumsajili Kisinda kama ilivyokuwa imeshauriwa huko nyuma. Kwa mujibu wa Kanuni ya 62(1) ya Ligi Kuu Toleo la 2022, klabu inaruhusiwa kusajili wachezaji wa kigeni wasiozidi 12.

Kambole amejiunga na timu ya Wakiso Giants inayocheza Ligi Kuu ya Uganda, na tayari TFF imetoa ITC.
View attachment 2358005
bagamoyo
 
Nakumbuka hili swala wakati linaongelewa mwenyekiti wa kamati ya mashindano yanga alisema kila kitu Hadi Itc imefika tayari.

Sasa wewe ni nani kuleta taarifa kuwa Itc haikuwa imefika?

Bado Unaitaja Yanga? Kama Ilitakawa Kuwafurahisha Mashabiki?

TFF ihurusu Wachezaji wingine Kusajiriwa Imzuie Kisinda Tuuu Kwa Kipi?
 
Wanaua vipaji vya ndani

Hizi team ni bora liende tu hawajali

Kukuza vipaji vya ndani

Ova
Tuwe wakweli jamani Tanzania kwasasa wachezaji wengi wana vipaji vya kawaida.

Kama unataka kuamini hili hebu angalia timu yetu ilokua inatafuta nafasi ya kwenda chan nambie ni namba 9 gani wa maana tunaye?
Ni beki gani namba 4 na 5 wa maana tulonao wanaocheza ligi ya ndani?

Kama inafika hatua timu zenye academy Bora kama mtibwa na azam wanajaza wachezaji wa nje hapo inafikirisha sana
 
Bado Unaitaja Yanga? Kama Ilitakawa Kuwafurahisha Mashabiki?

TFF ihurusu Wachezaji wingine Kusajiriwa Imzuie Kisinda Tuuu Kwa Kipi?
Kwahiyo unachobisha sasa ni kipi?

Tuisila si kasharuhusiwa kucheza
 
Tatizo Linakuja Pale ambapo Mkipewa Utaratibu mnahisi Kuonewa.

Na Simba na Yanga Ndio Timu zinazotumia Mashabiki Kuipa Pressure TFF, Hili Jambo Lingetokea IHEFU usinge sikia Hizi Kelele.

Tulieni na Fuateni Utaratibu muache kuhisi Kila Kitu mnaonewa
Tatizo unaongea uongo inaewekanaje kusajiri dirisha likiwa closed kubali tu kua TFF walivurunda kwenye hili
 
Kumbuka Yanga Walikuwa wana Ipa Pressure TFF ya Kutaka Kumruhusu Kisinda Acheze wakati kambole Tayari alikuwa na ICT ya Kucheza Tanzania na TFF ndio Ilikuwa Msimamizi wake, Kama TFF ingekubali Pressure ya YANGA bila Kumzingatia Kambole, Basi Kambole Angeweza Kushtaki Fifa Kwa Kufanyiwa Hujuma
Na wewe si ujitahidi kuelewa! ICT ndiyo nini? Ni mafunzo ya computer hayo?
 
Kumbuka Yanga Walikuwa wana Ipa Pressure TFF ya Kutaka Kumruhusu Kisinda Acheze wakati kambole Tayari alikuwa na ICT ya Kucheza Tanzania na TFF ndio Ilikuwa Msimamizi wake, Kama TFF ingekubali Pressure ya YANGA bila Kumzingatia Kambole, Basi Kambole Angeweza Kushtaki Fifa Kwa Kufanyiwa Hujuma
Mkuu hujajibu swali, au umelikwepa Kwa maksudi.. Iko hivi, klabu inajukumu la kuhahikisha mchezaji aliyeachwa anapata timu? Maana klabu kama imemua kutoendelea na mkataba na mchezaji vipi walazimishwe?
Au ndo Yale yale ya mpira wetu kivyetuvyetu!!!!
 
Alisajiliwa lini na dirisha lilifungwa lini? Sheria zinasemage au ni hisia zinatumika kufanya maamuzi? Naomba nieleweshwe?
 
Kwenye hili TFF walipuyanga sana..
All in all Kisinda amepata fursa ya kucheza acha akiwashe ili hapo October tuone umri wa Onyango ni miaka 27 kama vyeti vyake vinavosema au ni miaka 45 tunayoijua sisi wakongwe wenzake..
 
Kambole Alikuwa Hajapata Timu, Kitu kilicho Fanya Yanga Kuendelea Kusomeka Kuwa na Wachezaji 12 wa Kigeni. Na Mwanzo Yanga Hawakuwa katika Mpango wa Kuachana Na Kambole. Mpango wa Kuachana na Kambole Umekuja Baada Ya TFF kuwashauri kuwa Waachane na Mchezaji Mmoja Ndio Yanga Wakaona Wamtoe Kafala Kambole. TFF isingeweza Kubariki Uhamisho wa Kisinda wakati KAMBOLE HAJAPATA timu.
Pumbavu!
 
achana nao hao mkuu huwa hawaelewi. tff waliweka very clear ila tatizo la viongozi wa yanga hii ya hersi ni kila jambo hata kama la kikanuni wao wanalichukulia kishabiki. kama tff walikuwa wanataka kuziba wasingeomba ITC ya kisinda wangeuchuna. kama walikubali basi walitaka kufanya kitu sahihi sio kubania mtu. yanga walitaka kukata jina la kambole wakati tayari alishapatiwa leseni. kumtoa kambole ni lazima ahamishwe kwenda timu nyingine either kwa mkopo au mumteme mazima ili atolewe ktk system kwakuwa wana wachezaji 12 tayari.
mbona baada ya kushauriwa hivyo wamemtoa kwa mkopo uganda na kisinda ameingizwa.
 
Kwahiyo utaratibu wakuingiza mchezaji acheze NBC ni muda wowote hata dirisha linapofungwa?. Kama kisinda anaonesha hajasajiliwa ndani ya muda hiyo nguvu yakupokea uhamisho wa kambole na ku-mreplace na kisinda wameitoa wapi?
hivi unajua unachokiongea au kukiandika au [emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom