Rasmi: Mbwana Samatta asaini miaka minne na nusu Aston Villa

Rasmi: Mbwana Samatta asaini miaka minne na nusu Aston Villa

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
January 20, 2020
Birmingham England

NEW SIGNING MBWANA SAMATTA
Exclusive haya ni mahojiano ya Mbwana Samatta akiongea na chaneli rasmi ya klabu ya Aston Vill FC baada ya kukamilisha mkataba kuchezea klabu hiyo.



Source: Aston Villa FC

Habari kamili :
Mchezaji wa kimataifa wa Tanzania amesaini rasmi mkataba wa miaka minne na nusu na Timu ya Aston Villa ya mjini Birmingham, England.

Mbwana Samatta na klabu yake mpya wameweza kukubaliana mkataba na sasa klabu inafuatilia kukamilisha kupata kibali cha kazi na international transfer clearance certificate vitavyo mruhusu kuchezea klabu hiyo.

Hii inamaana Aston Villa na Genk KRC wameafikiana masuala yote mchezaji huyo nyota wa Tanzania kuhama kwa kitita cha £ 10,000,000. Klabu ya Aston Villa ipo nafasi ya 18 ktk msimamo wa league ya Premier League ikiwa na pointi 24. Mbwana Samatta pamoja na midfielder Jack Grealish ndiyo karata turufu atakayo itegemea kocha Dean Smith wa Aston Villa ili timu hiyo isiteremke daraja.

Mmojawapo wa Shabiki mkubwa wa Aston Villa ni Prince William ambaye ni mjukuu wa Malkia wa Uingereza Elizabeth II. Hii ina maana kuwa kasri ya Malkia Elizabeth II itakuwa inazizima kwa kelele, furaha, gonga-tano-kiganja za mjukuu na kusikia jina la Mbwana Samatta na Tanzania kila atapofunga goli.

Aston Villa chini ya midfielder kapteni Jack Grealish mwenye miaka 24 aliyefunga mabao 7 na Mbwana Samatta kuchukua nafasi ya namba 9 kuwa tumaini kubwa kuwachachafya walinzi wa timu pinzani na kuleta matokeo makubwa ya pointi kibao kwa Aston Villa isiteremke daraja.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 wa zamani wa Genk KRC ya Ubelgiji alifumania nyavu mara 76 akiwa na timu hiyo ya Ubelgiji katika michuano ya ligi ya Ubelgiji, Europa na mwaka jana ktk Uefa Champion league.

Katika UEFA Champion league Mbwana Samatta aliweza kufunga magoli dhidi ya timu kubwa zenye kuta ngumu za ulinzi za Liverpool na Napoli ya Italy na kuanzia hapo nyota ya Mbwana Samatta ilingara na timu kubwa ulaya kuanza kutafuta saini yake.

Uwanja wa nyumbani wa Villa Park umekuwa wa kihistoria maana toka 1897 timu ya Aston Villa haijawahi kutumia uwanja zaidi ya huo. Timu zingine kama Arsenal, Manchester United n.k ama walihamisha viwanja au kuvifanyia ukarabati mkubwa viwanja vyao.

Historia nyingine ya kutukuka ya Aston Villa ni walicheza miaka 24 mfululizo ktk premier league ya Uingerza kuanzia 1992 hadi 2016 walipoteremka daraja. Lakini hawakukaa ktk daraja la chini muda mrefu na kurejea tena ktk premier league mwaka jana 2019.

Video toka maktaba:
Shabiki mkubwa wa Aston Villa, Prince William alipewa heshima ya kuingia ktk pitch ya uwanja wa Villa Park pamoja na mkewe Kate walipata fursa kuongea na wachezaji pia kuona miradi ya klabu hiyo kurudisha fadhila kwa wapenzi na mashabiki kwa kushirikisha watoto wa mji huo.



Source: The Royal Family Channel
 
Amkeni amkeniiiiSio mambo ya NIDA !sasa ni wakati wa Samatta!

tapatalk_1579554615250.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamaa ndio mpambanaji namba 1 akifuatiwa na Diamond. Tanzania tujivunie kuwa na watu kama hawa..

Ukiisikiliza interview yake kaitaja Tanzania mara nyingi sana. anamzidi hadi Waziri wa mambo ya nje na waziri wa utalii kwa kuotangaza nchi.

Mtanzania pekee ambaye kila mtu anamsupport awe CCM au CHADEMA jamaa anatuunganisha Watanzania🔥

Najiombea mema pia namuombea na yeye atuwakilishe kwa kupiga magoli nyumbu za EPL
 
Klabu ya Aston Villa imemsajili nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta kwa mkataba wa miaka 4 na nusu akitokea klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji.

Official Mbwana Ally Samatta ni mchezaji wa Aston Villa baada ya kukamilisha usajili akitokea KRC Genk ambao ni mabingwa wa Belgium.

Misimu mitatu na nusu ya Samatta ndani ya Genk.

Mechi 191
Magoli 76
Assist 20

IMG_20200121_000157_193.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwana wa Mfalme Prince William na mkewe wakiwasili uwanja wa Villa Park. Prince William ni shabiki mkubwa wa timu ya Aston Villa yenye makazi yake katika uwanja wa Villa Park jijini Birmingham Uingereza.

22 Nov 2017
Birmingham, England

Prince William and Kate have visited Villa Park for a tour of the stadium today as part of a wider visit to the West Midlands. The Prince is a big Villa fan and couldn't resist talking about the team's progress this season.



Source: The Royal Family Channel
 
Back
Top Bottom