Rasmi: Mbwana Samatta asaini miaka minne na nusu Aston Villa

Rasmi: Mbwana Samatta asaini miaka minne na nusu Aston Villa

Gumzo la matumaini ya mashabiki wa Aston Villa ujio wa Mbwana Samatta

Mbwana Samatta kucheza nafasi ya namba 9 kuwa tumaini kubwa kuwachachafya walinzi wa timu pinzani na kuleta matokeo makubwa ya pointi kibao kwa Aston Villa.

Wachambuzi ktk gumzo hili wamekuwa wakimfuatilia Mbwana Samatta akiwa Genk KRC wakati wa mahojiano na kubaini ni mchezaji makini siyo tu uwanjani na hata anavyojibu maswali kuhusu timu yake hiyo ya zamani ya Ubelgiji.

Tayari wachambuzi wanasema Mbwana Samatta akiendeleza maajabu yake tusishangae akitua katika timu kubwa ukubwa wa za Arsenal n.k hivi karibuni maana mikataba huwa haimfugi mchezaji daima lolote linaweza kutokea nyota yake ikizidi kungara Aston Villa, wenye ubavu na bajeti kubwa wanaweza kumchukua.

Ghafla podcast hii ya uchambuzi wa timu ya Aston Villa imeanza kupata wafuatiliaji wengi wa East Africa.

20 Jan 2020

MBWANA ALLY SAMATTA signs for Aston Villa Football Club | Transfer Reaction

Aston Villa have tonight announced the transfer of Mbwana Ally Samatta from Belgian side Genk. The striker who captains his home nation Tanzania has put pen to paper on a four year deal. The Claret & Blue podcast team settle down to take a look at the incoming front man. "Sama Samagoal, Samagoal, Sama Samagoalllllll"



Source: The Claret & Blue - An Aston villa podcast
 
Jamaa ndio mpambanaji namba 1 akifuatiwa na Domo... Tz tujivunie kuwa na watu kama hawa..

Ukiisikiliza interview yake kaitaja TZ mara nyingi sana .... anamzidi hadi waziri wa mambo ya nje na waziri wa utalii kwa kuotangaza nchi..

MTz pekee ambaye kila mtu anamsupport awe ccm au chadema... jamaa anatuunganisha watz🔥

Najiombea mema pia namuombea na yeye atuwakilishe kwa kupiga magoli nyumbu za epl

Huyu Mbwana Samatta ni balozi wetu 'asiye na wizara / ofisi maalum' huko Ulaya ya Kaskazini.

Tumuenzi na kumuomba Mola amzidishie mafanikio katika nchi mpya na ligi ya huko iliyo bora zaidi ya Ubelgiji.
 
Juzi nilikuwa nikiwasiliana na mtu aliye katika viunga vya Jiji la Birmingham lakini pia muandishi wa habari. Alisema uongozi wa juu wa Aston Villa ulishtushwa na hali ya waTanzania wengi kuanza kuiunga mkono timu hiyo kitendo kilichopelekea kuongeza wafuasi takribani Million 9 katika mitandao yao ya Kidigitali na kijamii ndani ya siku 5 tu.

Pia alinambia zipo tetesi kuwa wataanzisha kurasa rasmi za Kiswahili kuweza kuwapa coverage ya kutosha maana inaonekana nguvu yao imefunika nguvu ya Astonians.

Jana alikuwa akisema siku ya kumtambulisha wanaweza kuja kivingine. Kweli naona majibu sasa katika hiyo hashtag #KaribuSamatta
 
isajorsergio,
Habari nzuri hii kwa Tanzania hususan watu duniani Watatamani kuchungulia ligi ya Tanzania VPL . Kubwa kituo cha television cha Azam TV waboreshe uonekanaji wa mechi za ligi kuu zionekane vizuri youtube na wachezaji wengine waonekane dunia labda watasainiwa kupitia mgongo wa nyota ya Mbwana Samatta. Kazi kwao wadau wote kuchangamkia fursa.
 
Habari nzuri hii kwa Tanzania hususan watu duniani Watanabe kuchungulia ligi ya Tanzania VPL . Kubwa kituo cha television cha Azam TV waboreshe uonekanaji wa nchi za ligi kuu zionekane vizuri youtube na wachezaji wengine waonekane dunia labda watasainiwa kupitia mgongo wa nyota ya Mbwana Samatta. Kazi kwao wadau wote kuchangamkia fursa.
Hakika! Kwanza kwa trend ya hashtag hii watu wanafuatilia kujua inahusu nini, ndio hapo wanaona Kiswahili+Tanzania.

Hivi Shabani wa Watford alifikia wapi kumalizana na TFF maana alikuwa anadai wanazingua?!
 
Hongera Zake Samatta. Wakati yeye akisonga mbele na kuingia EPL, bado namuombea Hasheem Thabeet pia arudi kwenye NBA.

Samatta anaweza kuitangaza Tanzania kiutalii zaidi ya mara kumi kuliko msanii yoyote Tanzania; watu wanaofikiwa na ujumbe wake ni watu wa kaliba kubwa na ni wengi sana kuliko watu wanaofikiwa na wasanii wetu wanaoimba mapenzi tu.

Itakuwa ni vizuri kama Wizara ya Mali asili na Utalii ikamwita wakakaa na kuongea, na ikiwezekana Samatta apewe diplomatic passport ya Tanzania badala ya hizi zetu za walalahoi.
 
Mbwana Samatta atakuwa kama Jamie Vardy wa Leicester City wote wameingia England Premier League wakiwa wamechelewa lakini Vardy ni mnyama hatari ktk harakati za kulifumamia goal. Na staili ya uchezaji wa Mbwana Samatta na kasi yake upo kama wa Jamie Vardy hivyo tutegemee mabao mengi sana kila wiki toka kwa Mbwana . Tutasikia wimbo wa Sama Sama Goal ! kila mechi toka kwa wapenzi na mashabiki wa Aston Villa.



Source: LCFC
 
Back
Top Bottom