Rasmi: Sead Ramovic amrithi Gamondi! Atangazwa kuwa Kocha Mkuu mpya wa Yanga

Rasmi: Sead Ramovic amrithi Gamondi! Atangazwa kuwa Kocha Mkuu mpya wa Yanga

Sead Ramovic ni raia wa Ujerumani aliyezaliwa huko Stuttgart tarehe 14 ya Mwezi Machi mwaka 1979. Hivyo ana umri wa miaka 45. Pia, Kocha huyu ana uraia wa Bosnia.

Kocha huyu ana Leseni ya UEFA Pro na ana wastani wa miaka 3.13 katika kazi ya Ukocha. Pia anapendelea kutumia formation ya 4-2-3-1

Takriban wiki moja iliyopita Kocha huyu alifanya jambo la kushangaza alipotangaza kuachana na TS Galaxy ya Afrika Kusini moja kwa moja kwenye TV baada ya klabu hiyo kutoka sare ya 1-1 na Stellenbosch kwenye Uwanja wa Athlone.

TS Galaxy imeanza vibaya kampeni za 2024/25 - wakiwa wamekusanya alama mbili pekee kutoka kwa mechi sita za ligi. Pia walitupwa nje ya shindano linaloendelea la Carling.

Ramovic anayependa kuzungumza waziwazi alifichua kuwa kupoteza wachezaji kwenye timu nyingine kila dirisha la uhamisho kulisababisha ajiuzulu nafasi yake ya ukocha wa TS Galaxy.

Katika siku za hivi karibuni, wachezaji muhimu wa Galaxy kama Fiacre Ntwari, Pogiso Sanoka, Lehlohonolo Mojela, Given Msimango, Melusi Buthelezi, na Bathusi Aubaas wamechukuliwa na Kaizer Chiefs na Orlando Pirates, miongoni mwa vilabu vingine vya PSL.

View attachment 3153068

HISTORIA YA KOCHA RAMOVIC KATIKA KAZI YAKE

Enzi zake za kusakata kabumbu Ramovic alikuwa akicheza nafasi ya Golikipa na baada ya kustaafu Mei 2014, alianza kujihusisha na Ukocha. Hii ni historia yake ya Ukocha kwa mujibu wa Mtandao wa Trasfermarkt

View attachment 3153093
Ramovic anayependa kuzungumza waziwazi alifichua kuwa kupoteza wachezaji kwenye timu nyingine kila dirisha la uhamisho kulisababisha ajiuzulu nafasi yake ya ukocha wa TS Galaxy.😀
Huku sijui atasingizia majeruhi au hali ya hewa?
 
Sisi ndiyo Simba SC AKA;

1. Makolokolo SC.
2. Mbumbumbu SC.
3. Mipang'ang'a SC.
4. Malalamiko (Lialia) SC.
5. Makelele SC.
6. Madunduka SC.
7. Manyaunyau (mapaka) SC.
8. Mwakarobo SC.
9. Mikia SC.
10. Miso Misonda SC.
11. Manyang'au SC.
12. Mazumbukuku SC.
13. Mazombi SC.
14. Kinyume nyume SC.
15. Ngada SC.
16. Kolowizard SC.
17. Zuwena SC.
18. Bebwabebwa (Mbeleko) SC.
19. Panya roads SC.
20. Kikanuni SC.
21. Kufa Kiume SC.
22. Ubaya ubwege SC.
23. 5imba SC.
24. Visingizio (Visababu) SC.
25. Manguruwe SC.
JamiiForums-2104962820.jpeg
 
Mkuu tusibishane sana acha tutajua nani mkweli

Pep kule City mechi mfululizo 4 kapoteza ila vipi hakubadili mbinu? Uwezo umeshuka? Mbona management haijamfukuza?

Ramovic takwimu zake si afadhali hata Gamondi?

Halafu sajili msimu huu injinia kabugi sana basi tu

Nani alimtaka chama na baleke? At least Dube nitakuelewa

Na baleke mwenyewe kocha alikuwa hamtaki hata kumtumia
Nadhani kilikuwa kipindi cha kuyumba mechi kadhaa then tungerudi kwenye mfumo tena.

Uongozi ujitafakari jezi tu mpya za CAF humo wamevujisha why?
Huwezi kurudi kwenye mfumo na kocha aliyeruhusu wachezaji wale starehe.

Mwenendo wa Gamondi ulikuwa unaenda kuizamisha timu. Angalia sub kwenye mchezo wa Tabora United zilikuwa hazilingani na mahitaji ya siku ile. Kuhusu wachezaji sidhani kama hilo ni tatizo, angalia ball possession ya mechi zote mbili tulizopoteza. Shida ilikuwa kwenye game plan ya mechi ili ushinde basi.

Wacha tuone huyu aliyekuja Kaja na nini.
 
Back
Top Bottom