Rasmi serikali yaruhusu na kuzindua matumizi ya magari ya umeme Tanzania

Kuna sehemu ngapi za kuchajia haya magari?

Maandalizi stahiki yamefanyika kweli?

By the way, hivi kabla ilikuwa marufuku kutumika Tanzania?
Jamani hii Ndiyo fursa changamoto ni sehemu ya mfanyabiashara ama mtumiaji kwani huwezi kununua betri ya ziada ama charger? Mnapendaz sana kulalamika? Wataalamu wa kulalamika kwenye hili siwaungi mkono
 
kazi ipo mpaka vifike choto😁😁.
FB_IMG_17171342994418928.jpg
 
Kwanza waweke vituo vya kuchaji magari na sio siasa
Yapo magari rahisi bei ya kutupa kama Dacia, Citroën, Mazda na hata MG ambapo unaweza pata nje kwa 90m unaongeza na ushuru na usajili

Ila zingine mziki wake ni mnene na brand new Toyota kama Rav4 ila umeme ni 150m ongeza ushuru
Hapo labda chuo kikuu watoto watengeneze za kwetu au injinia Kipanya
 
Attachments

  • Screenshot_20240531_065324_Auto Trader~2.png
    Screenshot_20240531_065324_Auto Trader~2.png
    884.9 KB · Views: 3
Kutoka Dodoma Naibu Waziri Mkuu Dotto Biteko amezindua matumizi rasmi ya magari ya umeme Kwa Wananchi wanapotaka kuyatumia.

View: https://twitter.com/Jambotv_/status/1796238475554877899?t=2YlUT7xwMIB0Q-koiyrmQg&s=19

My Take
Safi sana ,ukilalamika bei ya Juu ya Mafuta geukia magari ya umeme au gesi.

Samia amesema by 2034 anataka 80% ya Watanzania watumie Nishati safi.

Kazi za Samia zinaongea huhutaji propaganda.

Amezindua kiwanda cha utengenezaji wa magari au kutumika kwa hayo magari?
 
Kwanza waweke vituo vya kuchaji magari na sio siasa
Yapo magari rahisi bei ya kutupa kama Dacia, Citroën, Mazda na hata MG ambapo unaweza pata nje kwa 90m unaongeza na ushuru na usajili

Ila zingine mziki wake ni mnene na brand new Toyota kama Rav4 ila umeme ni 150m ongeza ushuru
Hapo labda chuo kikuu watoto watengeneze za kwetu au injinia Kipanya
Level zetu tutumue zile zenye mifumo miwili fuel+electric.
 
Kwani magari ya umeme yalikuwa hayaruhusiwi hapa Tz mpaka yaruhusiwe sasa?

Mbona tangu kitambo sana (japokuwa ni kwa uchache sana) yalikuwepo hapa Tz?

Nini mantiki ya bajeti ya serikali ta mwaka jana kutangaza kupunguza ushuru wa uiagizaji wake ikiwa yalikuwa hayajaruhusiwa kuingizwa nchini?

Nini mantiki kwa serikali kutokuyaruhusu kwa kipindi chote hapo kabla mpaka sasa ndio taruhusiwe?
 
Kutoka Dodoma Naibu Waziri Mkuu Dotto Biteko amezindua matumizi rasmi ya magari ya umeme Kwa Wananchi wanapotaka kuyatumia.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amezindua magari yanayotumia mfumo wa umeme ikiwa ni jitihada za serikali za kuwezesha wananchi kutumia nishati safi nchini. Uzinduzi wa magari hayo umefanyika Alhamisi Mei 30, 2024 jijini Dodoma sanjari na uzinduzi wa Ofisi za Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) pamoja na kituo cha uzalishaji wa umeme wa jua.

"Niwapongeze wadau wetu kutoka Umoja wa Ulaya (EU) na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa hatua hii, mtakumbuka kwamba serikali inaendelea kutafuta mbadala wa kuwawezesha wananchi hasa wale walio na uhitaji zaidi wa nishati safi” Amesema Dkt. Biteko. Amesisitiza kuwa ni muhimu kwa wadau wanaoshirikiana na Serikali kutafuta uwezekano wa kuwa na nishati safi ya uhakika ili kufikia malengo ya asilimia 80 ya Watanzania kutumia nishati safi ifikapo 2034. Kwa upande wake mwakilishi wa UNDP, Weyinmi Omanuli ameipongeza serikali kwa hatua zinazoendelea kuelekea kuwawezesha wananchi wake katika nyanja mbalimbali kijamii na kiuchumi.

Amesema kuwa kampeni ya Nishati Safi ya kupikia imekuwa kielelezo thabiti cha serikali kuwajali wananchi wake hususani wale wa kipato cha chini. Naye mwakilishi wa Umoja wa Ulaya, Cedric Marel amesema umoja huo una imani kubwa na serikali kupitia Wizara ya Nishati kuendeleza jitihada za kuwakomboa wananchi kwa kuandaa mazingira wezeshi yanayolenga kuboresha maisha yao. Akitoa salamu za utangulizi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amesema hatua ya uzinduzi wa magari yanayotumia umeme ni mwendelezo wa mpango wa Taifa wa matumizi ya nishati safi ya kupikia. "Huu ni mwendelezo wa utekelezaji wa kampeni ya kitaifa chini ya Rais wetu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inayolenga kuongeza matumizi ya nishati safi nchini” Amesema Senyamule.​

My Take
Safi sana, ukilalamika bei ya Juu ya Mafuta geukia magari ya umeme au gesi.

Samia amesema by 2034 anataka 80% ya Watanzania watumie Nishati safi.

Kazi za Samia zinaongea huhutaji propaganda.

View: https://twitter.com/EUinTZ/status/1796415222804312126?t=BHF9GAIIOipYbLaHcClY0w&s=19

Kupata vichekesho kama hv huna haja ya kumtafuta mchekeshaji, wasikilize mawaziri na viongozi wengine wa serikali
 
Asante kwa taarifa!
 
Back
Top Bottom