Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Wameandika mwenye mafanikio yake amefika. Ingawa watu wengi wanahisi atatangazwa Manzoki lakini inadaiwa kuwa atatangazwa kocha raia wa Ureno.
Tusubiri hapa mbivu na mbichi
===
Confirmed
Zoran ni 𝗠𝗡𝗬𝗔𝗠𝗔 🦁
Kwa furaha kubwa tunapenda kumtangaza kocha wa makombe, Zoran Manojlovic (@zoran_manojlovic_maki) kuwa Kocha Mkuu wa timu yetu. Kujua zaidi kuhusu mafanikio yake kwenye soka la Afrika.
MFAHAMU KOCHA MPYA SIMBA SC
Kabla ya kutua Simba Zoran Maki (60) alikuwa anaifundisha Al Tai FC ya Saudi Arabia 🇸🇦 ambayo alijiunga nayo aikitokea CR Belouizdad ya Algeria 🇩🇿 na kuiwezesha kufika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Zoran pia amewahi kuinoa Wydad Athletic Club ambayo ni miamba ya soka nchini Morocco 🇲🇦 Mwaka 2018 aliifikisha Primeiro De Agosto ya Angola 🇦🇴 Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo.
Kocha Zoran si mgeni kwa Tanzania 🇹🇿 amewahi kuja na Timu ya Al Hilal ya Sudan 🇸🇩 na kushiriki mashindano ya Super Cup yaliyoandaliwa na Simba mwaka jana.