Mashabiki wengi wa nchi hii akili zao wanazijua wenyewe,ulaya na Africa kuna utofauti mkubwa sana.Makocha wengi kule wanafatilia ligi za huko wanawajua wachezaji wengi,kuna scouting za wachezaji na ni rahisi kulingana na mifumo waliyojiwekea.
Leo hii ni rahisi Mourinho,guadiora au ancelloti wakipewa timu na pesa za usajili ni rahisi kwao.Ila huku Africa makocha wengi ni mawakala wa wachezaji hivyo ukiwapa power kubwa ya kusajili utaingia cha kike bado mpira wa kiafrika hatujafika levo hizo.
Mfano mwinyi zahera aliwahi kuleta wachezaji wake wakina kindoki pale,ni vile kwasababu timu haikua na pesa na mwinyi zahera alisaidia hata pesa zake mfukoni mambo yaende nani angemuhoji kuhusu wachezaji wake wengi waliokua wa kawaida?.Ni mara chache kwa Africa kocha kuwa na power ya kusajili