TAARIFA KWA UMMA
Uongozi wa Young Africans Sports Club unapenda kuutarifu umma kuwa umevunja mkataba na Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza, Angel Miguel Gamondi.
Vilevile, Uongozi wa Young Africans Sports Club, umesitisha mkataba wa kocha msaidizi wa kikosi cha kwanza, Moussa Ndaw.
Uongozi wa Young Africans Sports Club unapenda kuwashukuru Makocha hao kwa mchango wao ndani ya Klabu yetu na unawatakia kila la kheri katika majukumu yao mapya.
Tayari mchakato wa haraka wa kutafuta Makocha wapya wa kikosi chetu cha kwanza umeanza na unatarajiwa kukamilika hivi punde.
Daima Mbele Nyuma Mwiko.
Imetolewa na
Ofisi ya Mtendaji Mkuu (CEO)
Young Africans Sports Club
15.11.2024
View attachment 3152851