Ratiba inaendelea: Waraka wa TEC unasomwa leo kwa mara ya tatu

Hata wakipewa nakala kila kondo, hamna kitakacho badilika hawawezi kumyumbisha Raisi wetu hao waramba misalamba Tanzania ni kubwa kuliko hao idol worshippers.........
We huangalii mechi?
1. Goli la kwanza lilifungwa baada ya kusitisha kubadili sheria ya rasilimali za nchi (wanaolinda rasilimali 1 : Wengine 0).

2. Goli la pili likaingia baada ya kubadili mawaziri yule mtoto wa mama kaondolewa kwenye wizara nyeti (Wanaolinda 2: wengine 0)
3. Sasa hivi kuna faulu nje kidogo ya 18 inapigwa kuelekea kwa wanaotetea kwa TPA kutangaza zabuni ya kuendesha gati kadhaa

Mechi inaendelea bado kuna wachezaji machachari wanasubiriwa kuingia na hawa ni katiba mpya, tume huru, uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu. Mechi kati ya wanaolinda na wanaofuja itaisha baada ya uchaguzi mkuu.
 
Acha waendelee kugeuza madhabahu kuwa jukwaa la kisiasa.

Wana haki zote kufanya hivyo kuliko kukaa kuwaibia watu hela Kwa kisingizio cha kumtolea bwana
Acha ulimbukeni! Mungu atabaki kuwa Mungu,na ndio maana viongozi hao wote wa kisiasa wanaapa mbele ya Mungu kwa kuvishika vitabu vitakatifu wkt wakipewa majukumu ya uongozi unaotokana na siasa. Hivyo siasa ni dini na dini ni siasa tangu enzi za kitabu cha agano la kale kwenye biblia Takatifu na hata kwenye misahafu pia. Na Mungu tunayemuabudu ndiye aliyetuumba na kutoa mamlaka zote za kidunia kwetu sisi wanadamu,tujichagulie watu wa kutuongoza Kwa namna na taratibu mbali mbali ikiwemo kufanya kampeni na upigaji kura. Vyote hivi ni siasa. Sasa kama vyote hivi vililetwa na Mungu,na dini ndizo zinazotufundisha kumjua Mungu aliyeziumba mbingu na nchi pamoja na vyote vilivyomo ndani yake,unawezaje kumtenga Mungu kwenye siasa na wkt huo huo mkianza mikutano ya kisiasa mnamtanguliza kwa njia ya maombi!?
 
Kwani hawabusu hizo rozari zao kama sehemu ya ibaada yao?.......au wewe sio mkatoliki?
Hapa rozali pale tasibihi tofauti yake moja ina Msalaba wa Yesu (Crucifix) na nyingine ina uzi unaning'inia.
 
We
Wewe ni Serikali?

Ule waraka umeleta shida huko vijijini!!

Mwanakijiji anapoaminishwa na kiongozi wake wa Dini kuwa mna Nia Ovu na bandari zetu huamini direct.

KAZI IPO!!
Sawa wapeni tu hiyo shida
 
Leo umesomwa kanisani kwetu.Serikali iachane kabisa na huu mkataba
 
anatamani ata angekuwa na mamlaka ya kuwavua Uaskofu Wajumbe wa TEC[emoji23]
 
Niko live Tumaini TV. Namwona waziri Ummy Mwalimu na RC wa Tanga wamenuna kabla hata waraka wenyewe haujasomwa.
Ha ha ha[emoji1787] wakipewa nakala zao wapige picha
 
Acha waendelee kugeuza madhabahu kuwa jukwaa la kisiasa.

Wana haki zote kufanya hivyo kuliko kukaa kuwaibia watu hela Kwa kisingizio cha kumtolea bwana
mbona wanasiasa haohao huwa wanaenda kuomba kura kwenye madhabahu hayohayo, ila hamsemi, ila tec wakiongea jambo la kisiasa mnalalamika?
 
Kama hawa kuchaguliwa mbona hatukuona waraka kutoka kanisani wakumshauri au kumlaani alio wa teuwa bila kuchaguliwa, tukiwambia hao watu ni wadini amna uzalendo wowote mnabisha.
We ni mgeni umeanza kuijua TEC juzi. Fuatilia hotuba zao mwaka 2020 kwenye mitandao tafuta usije kuangukia kwa wenzako wanaojificha nyuma ya udini.
 
Tumeshatoa jibu nenda kwenye mitandao na link ziko nyingi Fr.Kitime na wengine walitoa hotuba mwaka 2020 za kulaani uhuni wa uchaguzi.
 
Kwani Tanzania ina bunge? Au umaanisha hayo majizi yaliyojazana huko bila ya kupelekwa na wananchi. Mwizi siku zote hubakia mwizi.
Wewe uliyachagua hayo majizi yaliyopo Bungeni ambayo hata mahakama imewakataa kuwa siyo wawakilishi wa wananchi?
Hoja yako ina msingi sana.
Huenda uchaguzi uliowaweka madarakani wabunge wale haukuwa huru na haki.

Kwasababu hiyo tumepata wabunge wa ovyo.
Hivi wakati wabunge hao wasio na sifa wanachaguliwa/ kuteuliwa hawa watoa waraka walikuwa wapi?
Je walithubutu kukemea na kutahadharisha madhara ya nchi kuwa na wabunge wa ovyo ovyo?
Walitoa waraka uliosomwa makanisani mwezi mzima kukemea hilo?

Tunapenda sana kulaumu tulipoangukia..

Udhaifu wa aina hii ndiyo unaotoa dalili kwa baadhi ya watu waone waraka una viashiria vya udini.
Watanzania ni vema tujue, udini wetu hautalifikisha taifa letu mahali salama.

Tumeishi pamoja kwa upendo tangu uhuru, tusikubali kugawanywa kizembe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…