Ratiba inaendelea: Waraka wa TEC unasomwa leo kwa mara ya tatu

Ratiba inaendelea: Waraka wa TEC unasomwa leo kwa mara ya tatu

Siamini kuwa waraka umesomwa leo, kanisani kwetu hapa St Thomas More Mbezi Beach ulisomwa mara moja tu siku ya kwanza.

Hakuna faida wala sababu ya kuja na waraka wakati TPA wameshaandika barua ya kutaka mwekezaji wa bandari na hata akiwa ni kampuni ya kizalendo hakuna tatizo lolote.

Lile lilikuwa ni jibu tosha kwa waraka, kwamba tujipange na kuja kimkakati ikiwa tunataka kushindana na makampuni yenye ukubwa wa DP World katika masuala ya uendeshaji wa bandari kisasa.

Lile halitakuwa tangazo la mwisho la serikali, kutakuwa na tangazo la bandari ya Mbamba Bay, kutakuwa na tangazo la Bandari ya Ziwa Tanganyika pia.
Mbona kinyonge sana!!
 
Leo Majaliwa atasikiliza live waraka wa TEC kwani yumo kanisani muda huu Angalia Tumaini TV wako live. Yuko na RC wa Tanga na Waziri wa Afya.
 
PM na yeye ni mtanganyika mwenye uwezo mkubwa wa kuona iwapo serikali ilikuwa sawa... ama vinginevyo!

Mwache asikilize Waraka unaoliponya Taifa na mali zake!
 
Unaweza kujiuliza kwanini TEC wakachagua kuusoma waraka wa kupinga kugawa bandari za Tanganyika kwa DPW kwa wiki sita na si pungufu ama zaidi?

Hili limekaa kiroho na kihesabu zaidi.. Dunia inaendeshwa na tarakimu na hesabu kupitia kanuni maarufu ya MAGAZIJUTO (BODIMUS)!

Mara sita inawakilisha siku sita za uumbaji, yaani siku sita za wiki.. Jumatatu mpaka Jumamosi! Kwahiyo ilipaswa waraka usomwe kila siku kwa siku sita mfululizo, lakini wanaosomewa ni waumini na waamini kanisani na siku pekee ya kuweza kuwasomea katika wingi wao ni siku ya ibada ambayo ni Jumapili

Kwahiyo ndio maana zikatengwa Jumapili sita mfululizo za kusomewa waraka husika, na leo hii ni Jumapili ya tatu

Waraka mpaka sasa umeonesha mafanikio makubwa sana! Dondoo zilizoandaliwa kisomi na kwa weledi mkubwa hazikutoka nje ya mstari wa katiba ya taifa

Zimejitokeza taasisi, vikundi na watu binafsi waliojaribu kuukosoa na kuupinga waraka lakini wakashindwa vibaya sana, kwakuwa badala ya kukosoa ama kupinga kilichomo kwenye waraka husika, wao wakaishia kutoa shutuma, kutuhumu na kukejeli watu binafsi, taasisi iliyoandaa waraka, imani ya waandaaji nk

Hawa wote walikuwa na haki kamili ya kufanya hivyo kwa mujibu wa katiba yetu, kakini kuna kila dalili kwamba hawakusukumwa na uzalendo na dhamira njema bali kwa maelekezo maalum na kwa malipo! Mbaya zaidi wakakurupuka sana na kuongea ujinga mtupu kisha haoo wakasepa zao kukinga mikono!

TEC hawakutetereka kwenye hilo na wala hawakuthubutu kunyanyua mdomo kujibizana nao! Walibaki na focus yao kukamilisha ratiba.. Na wanatambua wazi kwamba debe tupu haliishi kutika..!

Waraka wenye manufaa kwa watanganyika wote bila kujali
Itikadi zao
Imani zao
Makabila yao
Kipato chao nk nk unaendelea kusomwa leo kwa mara ya tatu, na ili kukamilisha ratiba bado mara zingine tatu. Wanaotumwa kuujibu kwa malipo wajitahidi kuujibu kwa hoja na si vioja

Watanganyika sio wapumbavu! Tunajitambua!!!!View attachment 2737210
Wiki 6 tu!
Someni huo waraka mpk atakapostaafu Samia, toeni nakala kwa watu wenu wote, bandikeni kwenye kuta za makanisa yenu yote
 
Siamini kuwa waraka umesomwa leo, kanisani kwetu hapa St Thomas More Mbezi Beach ulisomwa mara moja tu siku ya kwanza.

Hakuna faida wala sababu ya kuja na waraka wakati TPA wameshaandika barua ya kutaka mwekezaji wa bandari na hata akiwa ni kampuni ya kizalendo hakuna tatizo lolote.

Lile lilikuwa ni jibu tosha kwa waraka, kwamba tujipange na kuja kimkakati ikiwa tunataka kushindana na makampuni yenye ukubwa wa DP World katika masuala ya uendeshaji wa bandari kisasa.

Lile halitakuwa tangazo la mwisho la serikali, kutakuwa na tangazo la bandari ya Mbamba Bay, kutakuwa na tangazo la Bandari ya Ziwa Tanganyika pia.
Ratiba na maelekezo ni kusomwa kwa wiki, wasiosoma ni mipangilio yao ya ndani lakini hata hizo zilizokwisha somwa faida imeshaonekana
 
Back
Top Bottom