Ratiba inaendelea: Waraka wa TEC unasomwa leo kwa mara ya tatu

Ratiba inaendelea: Waraka wa TEC unasomwa leo kwa mara ya tatu

Wiki 6 tu!
Someni huo waraka mpk atakapostaafu Samia, toeni nakala kwa watu wenu wote, bandikeni kwenye kuta za makanisa yenu yote
Hatupangiwi tunapanga
Hatuelekezwi tunaelekeza
 
Unaweza kujiuliza kwanini TEC wakachagua kuusoma waraka wa kupinga kugawa bandari za Tanganyika kwa DPW kwa wiki sita na si pungufu ama zaidi?

Hili limekaa kiroho na kihesabu zaidi.. Dunia inaendeshwa na tarakimu na hesabu kupitia kanuni maarufu ya MAGAZIJUTO (BODIMUS)!

Mara sita inawakilisha siku sita za uumbaji, yaani siku sita za wiki.. Jumatatu mpaka Jumamosi! Kwahiyo ilipaswa waraka usomwe kila siku kwa siku sita mfululizo, lakini wanaosomewa ni waumini na waamini kanisani na siku pekee ya kuweza kuwasomea katika wingi wao ni siku ya ibada ambayo ni Jumapili

Kwahiyo ndio maana zikatengwa Jumapili sita mfululizo za kusomewa waraka husika, na leo hii ni Jumapili ya tatu

Waraka mpaka sasa umeonesha mafanikio makubwa sana! Dondoo zilizoandaliwa kisomi na kwa weledi mkubwa hazikutoka nje ya mstari wa katiba ya taifa

Zimejitokeza taasisi, vikundi na watu binafsi waliojaribu kuukosoa na kuupinga waraka lakini wakashindwa vibaya sana, kwakuwa badala ya kukosoa ama kupinga kilichomo kwenye waraka husika, wao wakaishia kutoa shutuma, kutuhumu na kukejeli watu binafsi, taasisi iliyoandaa waraka, imani ya waandaaji nk

Hawa wote walikuwa na haki kamili ya kufanya hivyo kwa mujibu wa katiba yetu, kakini kuna kila dalili kwamba hawakusukumwa na uzalendo na dhamira njema bali kwa maelekezo maalum na kwa malipo! Mbaya zaidi wakakurupuka sana na kuongea ujinga mtupu kisha haoo wakasepa zao kukinga mikono!

TEC hawakutetereka kwenye hilo na wala hawakuthubutu kunyanyua mdomo kujibizana nao! Walibaki na focus yao kukamilisha ratiba.. Na wanatambua wazi kwamba debe tupu haliishi kutika..!

Waraka wenye manufaa kwa watanganyika wote bila kujali
Itikadi zao
Imani zao
Makabila yao
Kipato chao nk nk unaendelea kusomwa leo kwa mara ya tatu, na ili kukamilisha ratiba bado mara zingine tatu. Wanaotumwa kuujibu kwa malipo wajitahidi kuujibu kwa hoja na si vioja

Watanganyika sio wapumbavu! Tunajitambua!!!!View attachment 2737210
Majaliwa leo atasomewa akiwa Kanisa Katoliki Tanga akihudhuria afla ya kusimikwa Askofu wa Kanisa Katoliki Tanga.
Yaani Mama Abdul kashikwa pabaya,anatamani ata angekuwa na mamlaka ya kuwavua Uaskofu Wajumbe wa TEC lakini mamlaka yake yanaishia kwenye katiba chakavu tu ya 1977!
 
Usomwe hadi Oktoba 2025


Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
Ahaa, kumbe bado unahangaika na majibu yako.
Wenzio wanasomeana waraka huko makanisani kwenu halafu wewe unaleta maswali yako huku, wapoteza nguvu bure
 
We
Serikali haitambi mitandaoni inatamba katika utendaji wa vitendo.
Wewe ni Serikali?

Ule waraka umeleta shida huko vijijini!!

Mwanakijiji anapoaminishwa na kiongozi wake wa Dini kuwa mna Nia Ovu na bandari zetu huamini direct.

KAZI IPO!!
 
TEC Wana makusudi mabaya kweli😂😂 hawaoni kama jamaa amekalia kuti kavu🏃🏃🏃
 
We
Wewe ni Serikali?

Ule waraka umeleta shida huko vijijini!!

Mwanakijiji anapoaminishwa na kiongozi wake wa Dini kuwa mna Nia Ovu na bandari zetu huamini direct.

KAZI IPO!!
Wataelimishwa kwa vitendo, zikishaanza kuondoka foleni pale TPA wataanza kufikiwa mapema na hizo bidhaa walizoagiza.

Kuna kundi kubwa la watu wanakwenda kuaibika baada ya DP World kuanza kazi pale TPA mwezi ujao mwishoni.
 
Wataelimishwa kwa vitendo, zikishaanza kuondoka foleni pale TPA wataanza kufikiwa mapema na hizo bidhaa walizoagiza.

Kuna kundi kubwa la watu wanakwenda kuaibika baada ya DP World kuanza kazi pale TPA mwezi ujao mwishoni.
DP World ndo imeisha hvyoo!!

Hakuna kitu kitaendelea pale.
 
Unaweza kujiuliza kwanini TEC wakachagua kuusoma waraka wa kupinga kugawa bandari za Tanganyika kwa DPW kwa wa leo kwa mara ya tatu, na ili kukamilisha ratiba bado mara zingine tatu. Wanaotumwa kuujibu kwa malipo wajitahidi kuujibu kwa hoja na si vioja

Watanganyika sio wapumbavu! Tunajitambua!!!!View attachment 2737210
Jamaa hawajapeleka polisi!?
 
Mkuu kweli hilo ni tusi au ni sehemu ya ibaada yetu, angalia hiyo picha af unijibu.View attachment 2737368
Mkuu yaan ndo unazidi kuharibu .kaka ikiwa sio Iman yako iache .tec wameongelea mkataba sio namna ya Imani yao au ya wengine .ni kama nakuelimisha ili umuheshimu kaka yako acha kumfatilia mke wake ww unaenda kutafuta chati za bodaboda na mke wake .ujumbe ni achana nayo .ukiwa na swali juu ya ukatoliki ni dini isiyo ya siri baada ya Misa kazi ya mapadre waliojaa hadi vijijini wenye .ningekuona muungwana sana kama ungejikita kujibu kisheria na kiuchumi hoja 7 za kupinga ujio wa dpw
 
Back
Top Bottom