GE2025 Ratiba ya chaguzi imetoka, NRNE chali. Liwe fundisho kwa wanaharakati

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
..uchaguzi ukifanyika katika mazingira haya utaonekana feki.

..Na watakaochaguliwa kutokana na uchaguzi huo watakosa uhalali mbele ya wananchi.

..hatua zilizochukuliwa na serikali bado sio jibu kwa hoja zilizowekwa mezani na Chadema.
Kwa Samia na GENGE lake, ni jambo moja tu: Kubaki madarakani. Haya ya "FEKI"; au kukosa uhalali hayamo kabisa akilini mwao.
 
Kwa Samia na GENGE lake, ni jambo moja tu: Kubaki madarakani. Haya ya "FEKI"; au kukosa uhalali hayamo kabisa akilini mwao.

..wangeweza kushinda kihalali, na hakukuwa na ulazima wa kushinda kwa dhuluma.

..kama jambo wanaweza kulipata kwa njia za halali, kwanini walazimishe dhuluma na umwagaji damu?
 
Huu ndio ukweli
 
Tunatiki
 

CCM hawajali hilo mkuu, wao ni watawale kivyovyote tu
 
 
Nawashauri chadema warudi kwenye ulingo wa mapambano kwa kushiriki uchaguzi.wanaweza pata wabunge wengi sana hata 20-50 wanatosha!! Waje niwape Siri !!
 
Hiyo picha hapo juu ni ya mfanyakazi wa tume ya uchaguzi? Kama siyo, kwani wameiweka hapo kwenye tangazo lao?
Kama bado huioni hiyo dosari ya tume kuiweka picha ya mgombea mmojawapo jua uchafuizi wao siyo mpya hapa bongo! Njaa ni laana!
 
..wangeweza kushinda kihalali, na hakukuwa na ulazima wa kushinda kwa dhuluma.

..kama jambo wanaweza kulipata kwa njia za halali, kwanini walazimishe dhuluma na umwagaji damu?
Wewe na mimi tunaweza kuamini kuwa CCM wanaweza kupata ushindi halali, kwa sababu mbali mbali.
Samia Suluhu Hassan na GENGE lake, hawana uamini huo tulio nao sisi.
Wao wanaijuwa vizuri hali yao kuliko sisi tuijuavyo.

Wewe na mimi tunaamini, ni CCM ndiyo yenye uwezo wa kupata ushindi, na wala hatujihangaishi kutazama CCM ni nani, na GENGE lililo teka CCM kama chama ni nani. Hivi ni vitu viwili tofauti kabisa.
 
Kwa maoni yangu naona NRNE imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa maana hadi sasa watakaoenda kupiga kura hawafiki 30% ya waliojiandikisha naamini hivyo, kwahiyo NRNE haipo hadharani ila kwenye akili za watanzania hadi sasa kuna "sitoenda kupiga kura"
Tuweke uvyama pembeni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…