Ni kweli ukiwasikiliza watu wa humu JF unaweza kufikiri Chato ni kijiji na mapori ya wanyama na hakuna watu wengi. Mwaka jana nilifika Chato nikakuta vitu tofauti kabisa na vinavoongelewa humu. Serikali ikifuata vigezo vinavyotumika kupata mkoa Chato ina vigezo vyote na zaidi kwa sasa maana Chato kuna Viwanda, Bandari, miundombinu ya barabara, kiwanja cha ndege, soko la samaki la kimataifa, hospitali ya kanda na pia kwenye wilaya zitakazounda mkoa zina jumla ya watu milioni mbili na zaidi na utakuwa kati ya mikoa yenye watu wengi Tanzania. Mwalimu Nyerere alijenga kiwanda Chato na bandari ya Nyamirembe mwaka 1968. Chato ni eneo muhimu sana kiuchumi hasa ukizingatia kuwa jirani na nchi za Rwanda na Burundi.