Ratiba yako ya Chakula cha Ijumaa Kuu ikoje?

Ratiba yako ya Chakula cha Ijumaa Kuu ikoje?

Nimeangusha ugali dagaa iliyowekwa nyanya chungu,Karoti, hoho,bilinganya,bamia.

Jioni ndizi za kukaangwa na kikombe cha tangawizi kaliiii
 
Hahahah nimekuelewa
Bro alijiona yupomo,
Kama yule anavyojisema amekulamo kivile
Na kawala kweli enzi zile. Si unajua tena nyumba za Oysterbay, servant quarter alikuwa anakaa yeye, katengeneza na backyard gate anawapitishia huko.

Siku moja baba akakadaka kabinti, kumbe mzee kafunga cctv na sisi hatujui. Kila siku ananuona binti yuko ghetto
 
Lete Maneno.....
Unakula Mashelisheli Siku Nzima
 
Mchunga,

Mlenda (bamia Na ngogwe),

Ugali,

Thamaki (Kipande cha mkule) wa kulumangia,

Pepsi
 
Chapati moja na maji ya moto
mchana ugali maziwa mtindi
jioni desh

Hii ni Kwaresma.



Katika kitu huwa kimenishinda ni pamoja Na kula ugali Kwa maziwa ya mtindi.

Yaani naona vyote vimepooza! [emoji848]

Siijui ni mazoea?!

Afadhali nipate mlenda wa unga wa nyanya (mkubugwa).
 
Back
Top Bottom