Tetesi: Ray C akimbizwa Muhimbili

Tetesi: Ray C akimbizwa Muhimbili

Alaaniwe aliyesababisha huyu dada akaanza kutumia hayo madude.
Mh ukishaingia hujijui ni sawa na kumwambia mtu asinywe kili au serengeti yaleyale tofauti wa kili anafika nyumbani anajitambua huyu wa sembe mhu ikiisha kichwani ataiba hata tail la gari la abiria ili auze apate mhogo.
 
Jamani nn tena Dada ray c kinachomsumbua ?naombeni jibu jumapili iliyopita nilimwona mwananyamala na tukapiga story fresh yuko poa tunacheka nn kimemsibu tena
 
Mh ukishaingia hujijui ni sawa na kumwambia mtu asinywe kili au serengeti yaleyale tofauti wa kili anafika nyumbani anajitambua huyu wa sembe mhu ikiisha kichwani ataiba hata tail la gari la abiria ili auze apate mhogo.
Inasikitisha sana tunawapoteza vijana kwa haya madude.
 
madawa bado yapo kwenye damu yani kama ikiwezekana atoe damu aweke nyengine aisee ile kitu ya alosto bado inamuandama na hiv ameacha kunywa methadone ndo kabisaaaa . ndugu zangu msijaribu hata kutest pafu moja coz hutaacha kurudia sababu ya utamu wake
 
Hakawii kusema Shigongo huyu...
na hili ndo lina nifanya nisimwonee huruma...anapoambiwa anapotea anajifanya mjuaji na kutishia watu!mficha maradhi kilio humuumbua...simhurumii hata kidogo
 
Huyu dada anahitaji kusaidiwa; kumlaumu kuwa alijichagulia haya maisha sio sahihi (unless tuna ushahidi wa tunayoyasema). watu wengi hapoa tanzania na kwignineko wanaingia kwenye madawa ya kulevya kwa kudanganywa kama vile kuchanganyiwa katika sigara, vinywaji nk. Ifahamike kuwa mtu akitumia madawa ya kulevya kwa siku tano hadi wiki tu! inatosha kumfanya huyu mtu awe addicted (mteja). Madawa ya kulevya (Cocaine, Heroine) yana physiological dependency, yaani mtu anapoacha kuyatumia anapata mabadiliko ya kimwili (ki-fiziolojia) kama vile, kuharisha, kusikia baridi, kutokwa makamasi, kuona maluweluwe na kuota ndoto za kutisha-hali hii wenyewe ndio huiita ''arosto''. Tusiwanyanyapae hawa watu sio wote waliamua kwa hiari yao, wakiwa wanafahamu possible consequence za haya ''makitu''.
Jk alimsaidiA sasa yy badala ya kujiratahid kaenda kutafuta mabwana mateja..... Haina haja ya kumihurumia
 
Nani kakudanganya?
Mimi nimewahi kuwa na ukaribu na mateja fulani.
Maana mimi napenda sana kudadisi,waliniambia mengi sana ambayo ningeambiwa na watu tofauti nao (mateja) nisingeamini.

Hayo mambo wanayafanya sana tu,pole zako kama unadhani nao 'hawaponi'.
Ni kweli, na pia mtumiaji wa madawa ya kulevya anakuwa katika hatari ya kuambukizwa magonjwa ya zinaa muda wowote, iwe kwa hiari yake au kulazimishwa..

Pole kwake Ray C na M / Mungu ampe tumaini jipya.
 
Duuu walaaniwe wote waingizao madawa haya kwa jina la Yesu...I REMEMBER AMINA CHIFUPA..R.I.P
Wanaoingiza dawa wanatafuta pesa kwa sababu wanafahamu kuna maf'ala wenye akili zao timamu watatoa pesa walizotafuta kwa jasho lao huku wakifahamu fika kwamba wanajiua! Kwahiyo acheni drug dealers watengeneze pesa kupitia migongo wa wapumbavu!

Hivi wewe umekutana na demu akakuthibitishia kwamba ana ngoma! Pamoja na yote hayo ukang'ang'ania tunda lake na ulipopewa ukaenda kavu kavu na mka-share kaugonjwa!! Bado hapo utataka uhurumiwe wewe na dada wa watu ndie alaaniwe?
 
Back
Top Bottom