RC chalamila hatumii akili anaropoka tu kwakuwa yeye, maaskari, mwamnyange na wengine serikalini ndio wamiliki wa bajaji wakiwemo wana jeshi wanaotumia vibaya nafasi walizo nazo.
Wenye daladala wanalipa kodi nyingi, TRA, LATRA, Ushuru wakati bajaji hawalipi hizo hasa hiyo sticker ya LATRA.
Vile vile bajaji wanaendesha rough barabarani na wamekuwa ndio wasababishaji wa ajali na ajali zikitokea faini anapigwa mwenye daladala kwa kuwa mwenye bajaji ni mwanajeshi, au bajaji ya mwamnyange au ya chalamila mwenyewe.
Bajaji hawana vituo rasmi wao wana simama na kupakia popote amabapo ni hatari huku ukizingatia udereva kenge wao+rough driving)
Bajaji zimekuwa kero mjini kwasababu hawafuati wala kuzingatia usalama barabarani kwenye zebra hawasimami hatakama kuna wenda kwa miguu wapo, bajaji wao wanachomekea tu kwasababu udereva wao ni wa kenge.
Bajaji ndio zimekuwa chanzo cha foleni mbeya mjini kitu ambacho kina didimiza uchumi na ustawi wa jiji kwasababu watu wanachelewa kazini nk
Bajaji wengi kuanzia madereva hadi mabosi zao wengi wamefoji kuanzia license hadi sticker kitu ambacho kinaipunguzia mapato serikali.
Bajaji zitumike kutanua jiji badala ya kubanana mjini. Bajaji zifanye safari za pembezoni mwa jiji mfano uyole - isyesye, ilomba - isyesye, mwanjelwa - ilemi iyunga - must n.k. ili daladala tuziache high way hii itasaidia kupunguza kero zote za bajaji hapo juu.
Chalamila jifunze kuzungumza kwa staha na kwa amri hiyo ni Biashara ya watu, hao ndio wawekezaji wenyewe uwekezaji sio hadi atoke nje au ajenge kiwanja.
Bajaji zitumike kupanua jiji liwe kama dar sio jiji limejibana kisa watu wanaogopa kwenda kufanya biashara nje ya jiji kwa kuhofia changamoto ya usafiri.
Otherwise Sumatra mu assign route mpya za daladala au LATRA na TRA muondoe kodi katika daladala au takukuru na vyombo vingine vya usalama wafanye kazi ya ziada kitu ambacho hawakiwezi kwasababu wao ndio wamiliki na ndio wanaongoza kumiliki bajaji jijini mbeya.
Acheni kufanya siasa kwenye uchumi.