Pre GE2025 RC Chalamila: Kama una miaka 40 na hauna pesa usimlaumu Rais Samia

Pre GE2025 RC Chalamila: Kama una miaka 40 na hauna pesa usimlaumu Rais Samia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mungu amrehem.
Takbiiir, hii kufri dharau kuburi na kibri, hii Allahu akbar, Allah mwenye rehma na utukufu ulio mkuu zaidi, angalia kibri na ulevi wa neema uliyomjalia kiumbe wako huyu, Allah tunakuomba tuonyeshe utukufu wako juu ya mwanadamu huyu, Amin.
Masheikh msifanye dhihaka juu ya Dua hii, - -Dua hii haina utaratibu wa kurudi nyuma.
 
View attachment 3002138

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amewashangaa wenye umri zaidi ya miaka 40 wanaolalamika kukosa pesa na kutoa lawama kwa Rais Samia.

Chalamila amesema: β€œKama una umri kama wa kwangu na bado hujawa na hela huna haja ya kutenda dhambi ya kumlaumu Rais aliyeingia miaka mitatu iliyopita.Umri huu zaidi ya miaka 40 hela sina nilizaliwa wakati wa Nyerere, akaja Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli pamoja na Samia huna pesa ninashangazwa”.

Chalamila amesema hayo leo Mei 28 ,2024 akiwa katika ziara ya Jimbo la Ukonga kukagua miradi mbalimbali na kusikiliza kero za wananchi wa jimbo hilo.
Sasa kwanini wasilmlaumu samia kwasababu wanalipa Kodi chungu mzima lakini mgawanyo wa hiyo Kodi hauko sahihi CCM wanatumia kwa hanasa na ufisadi Sasa ni kwanini huyo mwenyekiti wa CCM asilaumiwe hivi ukiwa na mashavu kuvimba akili inabaki huko!!?
 
Hili boya ni kulipiga shaba ya kichwa liondoke. Very stupid. Watu waibe?. Wawe majambazi? Kila kiongozi analaumu wananchi Sasa kuna haja gani ya kuwa na serikali? Stupid
 
Point yake ni kutomlaumu rais wa sasa wakati marais kadhaa wameshapita ukiwa duniani.
Mueleweshe huyo RC serikali Ina ridhi kila kitu Cha serikali ya nyuma. Kwa hivyo lawama atapewa huyo Samiah Kama walivyopewa wengine.
 
Kama hawakukusomesha au hawakujituma kutafuta mali ilihali sio wenye ulemavu wowote. Au hawakukutengenezea connection.

Ushauri: ikiwa wewe ni mzazi/mlezi, jitahidi sana kuwatengenezea watoto wako maisha ya kutolalamikia serikali hapo baadae
Ni rahisi kuongea ila vitendo ni vigumu. Wazazi wangapi wanajitahidi ila mambo ni magumu. Usipende kuongea kisa mambo yako yamekunyookea.
 
Mimi Huwa napenda sana maneno yanayonichoma kama haya hata kama ni kweli Sina.

Bill gates aliwahi kusema; Ukizaliwa maskini sio kosa lako, Lakini ukifa maskini Hilo ni kosa lako!

Sasa wewe kazana kumlaumu Raisi
Rais lazima alaumiwe Kama hajaweka mipango na sera endelevu. Tusipende kuwapaka mafuta wanasiasa na kuwatupia lawama raia.
 
Wazazi hawahusiki tena, wamakulea ukawa mtu mzima wakamaliza kazi yao.
Wewe pambana kivyako, serikali ikiwa na sera au mipango mibaya ungana na wengine kuweka mambo sawa. Utafanikiwa tu.
Kila raia ana wajibu wa kujiendeleza binafsi, familia, jamii na taifa lake. Hakuna sababu ya kulaumu, pambana kuondoa vikwazo.
Sasa serikali ikiwa na mipango mibaya na sera mbaya kwanini isilaumiwe. Yani unataka wananchi wafanye maendeleo gani wakati serikali Ina sera mbovu?.
 
Back
Top Bottom