Pre GE2025 RC Chalamila: Kama una miaka 40 na hauna pesa usimlaumu Rais Samia

Pre GE2025 RC Chalamila: Kama una miaka 40 na hauna pesa usimlaumu Rais Samia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wazazi hawahusiki tena, wamakulea ukawa mtu mzima wakamaliza kazi yao.
Wewe pambana kivyako, serikali ikiwa na sera au mipango mibaya ungana na wengine kuweka mambo sawa. Utafanikiwa tu.
Kila raia ana wajibu wa kujiendeleza binafsi, familia, jamii na taifa lake. Hakuna sababu ya kulaumu, pambana kuondoa vikwazo.
Ni kweli wazazi hawahusiki, lakini kuilaumu serikali ni sahihi kwa kuwa tunailipa kodi.
Ukimlipa fundi akurekebishie mlango wako lakini akasepa, hautamlaumu?
 
Namuelewa hana qualification za kuwa nafasi hiyo kwa hiyo kasoma game na anaenda nalo.ni kama hapi mm nlikuwa namuelewa kuwa anaenda na floo ya magu
 
Yupo sawa kwa sababu mama SAMIA ana mchango mchache sana kwenye umasikini wako tusitumie mihemko kumuelewa Mh RC Chalamila a.k.a Toto tundu la taifa
 
Ni sahihi kabisa. 40+ yrs labda uwalaumu wazazi wako.
Hivi nyie mtatetea serikali kwa lipi?. Ufisadi wote kwa CAG hizo pesa zingepelekwa kuwezesha vijana wenye ideas ingekuwaje, mmekalia vijembe tu bila sera na maono.
 
Yupo sawa kwa sababu mama SAMIA ana mchango mchache sana kwenye umasikini wako tusitumie mihemko kumuelewa Mh RC Chalamila a.k.a Toto tundu la taifa
Pesa zikitilewa ni za mama Samiah ila mambo yakienda kombo sio mama Samiah. Serikali ipo kwaajili ya kuwezesha raia wake kiuchumi. Sasa Kama raia hawawezeshwi wamlalamikie nani wakati Viongozi wanajipangia posho na pesheni kwa wenzako wao. Tuwe wakweli na tuache siasa. Kila siku mabiliini yanapotea mpaka ripoti ya CAG imepoteza mvuto siku hizi.
 
Ni kweli wazazi hawahusiki, lakini kuilaumu serikali ni sahihi kwa kuwa tunailipa kodi.
Ukimlipa fundi akurekebishie mlango wako lakini akasepa, hautamlaumu?
Tupo pamoja kifikra. Sera, sheria, miongozo na maamuzi ya serikali ndiyo huathiri maendeleo ya raia.
Na nimeandika kuwa wananchi lazima wapambane kwa ushirikiano kusawazisha hayo.
 
Hata kuliko endelea ulaya na amerika alichokisema Chalamila HAKIPO!
Human incomes varies!
Riches 5%
Midlle 35%
Lower 60%
 
View attachment 3002138

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amewashangaa wenye umri zaidi ya miaka 40 wanaolalamika kukosa pesa na kutoa lawama kwa Rais Samia.

Chalamila amesema: “Kama una umri kama wa kwangu na bado hujawa na hela huna haja ya kutenda dhambi ya kumlaumu Rais aliyeingia miaka mitatu iliyopita.Umri huu zaidi ya miaka 40 hela sina nilizaliwa wakati wa Nyerere, akaja Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli pamoja na Samia huna pesa ninashangazwa”.

Chalamila amesema hayo leo Mei 28 ,2024 akiwa katika ziara ya Jimbo la Ukonga kukagua miradi mbalimbali na kusikiliza kero za wananchi wa jimbo hilo.
Bila shaka Chalamila atakuwa alilewa
 
Tofautisha ukweli na dhihaka. Alichoongea Chalalamila ni dhihaka sio ukweli. Wao wanaiba pesa kila mwaka kwenye ripoti za CAG imeandikwa. So wanaweza kuropoka maana ameshiba.
Huna ushahidi wa kumhusisha huyo Chalamila na huo wizi anaousema CAG, ni yale yale maongezi ya ndani ya daladala ya abiria.
 
Kama kiongozi mteule wa Mheshimiwa Raisi halipi wakandarasi wanafilisika hadi na kuuziwa mali zao mfano Arushana Ifakara nani alaumiwe zaidi ya mamlaka ya uteuzi?
Je rushwa na urasimu unaolalamikiwa kila siku katika kila sekta,je hauleti umasikini?
Mtu anawekeza fedha zake kwa mtaji wa aliotafuta kwa muda mrefu halafu mwajiriwa wa serikali anaomba hela ya mafuta,Serikali haioni kuwa hivi virushwa vidogo vidogo vinarudisha nyuma maendeleo ya wengi, na mtu kuamua akipewa mradi tu awakatia chao na anafanya chini ya kiwango, hawaoni nyufa kwenye majengo yao mchanga mwingi kwenye zege?
 
Wazazi hawahusiki tena, wamakulea ukawa mtu mzima wakamaliza kazi yao.
Wewe pambana kivyako, serikali ikiwa na sera au mipango mibaya ungana na wengine kuweka mambo sawa. Utafanikiwa tu.
Kila raia ana wajibu wa kujiendeleza binafsi, familia, jamii na taifa lake. Hakuna sababu ya kulaumu, pambana kuondoa vikwazo.
Kuna watu wanapambana,lakini bado wanadhulumiwa haki zao kupitia hiyo hiyo Serekali, siku na yeye aite wananchi wenye kero zao kama wenzake Makonda na Silaa wanavyofanya aone mtimti wa watu wasiokua na pesa waliodhulumiwa haki zao na wenye pesa watakavyo mjalia hapo kwa office yake,alafu aanze kutatua kero zao! Siyo kila masikini ni mvivu, wengine umasikini wao umetokana na dhuluma pamoja na kesi zisizoisha za nenda rudi kesho huko Mahakamani!!
 
Kama angeelezea tu fursa zinazotokana na uwekezaji wa serikali kama umeme na barabara bila kusema mambo ya umri kungekuwa na shida gani? Vi hela vya ukuu wa mkoa vinamzuzua?
 
Kuna watu wanapambana,lakini bado wanadhulumiwa haki zao kupitia hiyo hiyo Serekali, siku na yeye aite wananchi wenye kero zao kama wenzake Makonda na Silaa wanavyofanya aone mtimti wa watu wasiokua na pesa waliodhulumiwa haki zao na wenye pesa watakavyo mjalia hapo kwa office yake,alafu aanze kutatua kero zao! Siyo kila masikini ni mvivu, wengine umasikini wao umetokana na dhuluma pamoja na kesi zisizoisha za nenda rudi kesho huko Mahakamani!!
Sawa kabisa wafuate mtindo huo wa Waheshimiwa Makonda na Jerry kwa nchi nzima, kifupi watendaji wengi wa serikali mikoani , wilayani sasa hadi katani ndio mitambo ya kuzalisha na kuongeza umasikini, je serikali haiwalipi mishahara hadi wa omba omba kwa wanaotafuta huduma mfano RITA eti cheti cha mtoto elfu 20?
 
Back
Top Bottom