RC Chalamila: Kujifanya wanasheria pamoja na kupenda kiingereza kunakwamisha maendeleo ya mkoa wa Kagera

RC Chalamila: Kujifanya wanasheria pamoja na kupenda kiingereza kunakwamisha maendeleo ya mkoa wa Kagera

Hivi unafahamu Kasulu tu iko pembeni lakini hakuna wilaya kagera inaipita kasulu kwa kuchapa kazi na kukua kwa mji ule, katoro achana na tunduma ambako watu saa 11 alfajiri chakula kimeiva, maduka mbinga saa moja asubuhi walishafungua zamani, masasi mapema tu biashara ziko wazi wao kuelezwa wafungue biashara mapema wanaona wameonewa huo nao ujinga sana
Amekurupuka. Mafinga Kuna mabasi yanaingia saa kabla ya saa moja asubuhi, lakini hukuto Duka kubwa likiwa wazi hunabudi kusubili hadi saa 2:30 ndio wafungue na mji ule unayo maduka makubwa matatu. Ngori ,Mgaya, na vunja Bei kama Dar la bwana CF.

Kufungua biashara usiku inategemea na maatiji ya watu.
 
Wewe ni masikini jeuri tu na haina exposure ya kufanya kazi na watu tofauti na wabongo! Fanya kazi hata Gita Gold Mine GGM hapo uone watu wanavyotunza time! Utaahira wenu ndo mnaonaga elimu ndo kila kitu lakini dunia ya leo inahitaji watu wenye maarifana wanaotunza wakati sio elimu tu!
Sasa Kati ya mm na wewe tahira ambaye hajielewi ni nani......kwa hiyo unaona Sasa hapo huyo bwana wako Chalamila aliongea pointi si ndio
 
View attachment 2344085

Hayo ameyasema wakati wa kikao cha ndani cha siasa kilichohudhuriwa na makamu mwenyekiti wa CCM bara bwana Kinana.

===

“Mkoa huu hauendelei kwa sababu nyingi, ila sababu kubwa ni hata ninyi ndugu zangu wahaya, wanyambo mnaoishi hapa kwa kweli kuna muda bado hatujajitambua kwamba tupo kwenye ushindani.”

“Tukipita hapa hata siku za kawaida mpaka saa 3 maduka hayajafunguliwa. Sasa unajiuliza, duka linafunguliwa saa tatu. Inamaana mnalala sana au mnafanyaje? Sasa na ninyi mbadilike, fungueni duka mapema ili tuingie kwenye ushindani.”

“Jambo lingine linalokwamisha mkoa huu pia Mhe. Makamu mwenyekiti, Kila mmoja hapa kwenye mkoa huu huwa ni mwanasheria, mnapenda sana kubishana. Eeeeh…Mambo mengi wanapenda kiingereza kingi kingiii, sasa naomba niwaambie, sitaki kiingereza waa sitaki makaratasi”

“Nataka namna gani utakavyo tumia elimu yako kuibadilisha kuwa maendeleo kwa wanakagera. Basi.”
Wahaya ni shidaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Wameelezwa ukweli wanaanza kuleta maneno, hapo ujumbe waache uvivu waongeze kasi ya kuchapa kazi wafungue maduka mapema sana biashara zifanyike sio unaduka sababu ni lako ukafungue saa nne, wachukue ushauri wasonge mbele siri ya maendeleo ni kazi kwa bidii
Instanbul ukuje hukuuu
 
Unavyoongea kama vile kagera ni nchi nyingine

Hebu nenda katumie hio fursa ya mipaka maana hujakatazwa....
Kabla ya kuwaketukana watu wa kagera hebu angalia vzr mfumo wa ufanyaji wa biashara za mpakani ndo utajua kwa hali iko hivyo

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
Duuu kumbe upoooo[emoji3][emoji2][emoji3][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
 
Kabla ya kulaumu ni bora ufanye research kwa nini hali iko hivyo...

Watu baada ya kutafuta solution wanabeza personality, makabila nk ...serikali ambayo iko responsible kuleta maendeleo ya mkoa kwa sababu inachukua kodi ndo ya kwanza kwa kejeli na matusi...

Kuna professor mmoja juzi alisema " linapokuja suala la maendeleo ya mkoa wa kagera ambayo ni ya umma...serikali inajitetea kwa kuattack wahaya as wahaya wana serikali yao..lakin mikoa mingine no one cares about kabila"


Lakin hio simiyu sijui geita kote umaskini mtupu tena bora kagera kuna tatizo la miundombinu ya umma lakin maendeleo ya mtu mmoja mmoja yako vzr tazama hata makazi ya watu huko vijijini..

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
Kuna uhusiano gani kati ya serikali na kuchelewa kufungua maduka yao?
Je serikali inawaambia wachelewe kufungua?
Acheni viiingereza viiiiingi mfungue maduka mapemaas
 
Hayo maduka Chalamila au Serikali iliwasaidia kuyafungua?
Uongozi bora ni pamoja na kuheshimu tamaduni za uliowakuta. Wao wanajua wateja wao wanaanza kununua mahitaji saa 4, sasa afungue saa 12 amuuzie Nyani? Yaani kwa vile baa za Ulanzi Iringa zinafunguliwa saa 12 basi na maduka ya Wahaya yafunguliwe muda huo? Acheni ujuaji usio na maana wakati hata misingi ya biashara hamuijui.
Utumbo
 
Kiongozi sio kuongea yale mazuri tu au yale wanayopenda kuyasikia tu,ni pamoja na magumu na changamoto zinazowakabili,hapo RC alishausoma mkoa na watu wake na akagundua shida iko kwenye vijitabia vyao, na leo amapata jukwaa lakusemea akasema sioni tusi hapo wala shida, kikubwa waliolengwa wanajijua wajirekebishe waache kujifanya wajuaji.Rombo walisemwa kwa ulevi mpaka wanasaidiwa wake zao na wakenya lkn iliishia wapi zaidi ya kujirekebisha?wana kagera tusimuue rc tujirekebishe mkoa uko nyuma sana
 
Sasa mji si ndo reflection ya mkoa mzima?
Then hapo umepotea. Wahaya hawajengi mijini! Nenda kijijini uone! Mji ni wa serikali , lkn nyumba za wat zipo na mzuri tu! Stend ni ya serikali badala ya huyo RC kujenga stend analeta matusi
 
Mimi sijui wakisemaga kagera ni maskini...wanaongelea kagera ipi...

Maana huko vijijini kuna majumba na majumba...bila kusahau barabara za kunganisha wilaya nyingi ni za lami...
Wilaya kams muleba ina hospital tatu na shule kibao ...

Sasa sijui wanataka kagera nzima iwe na maghorofa kama dar?

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
Wacha maneno, hakuna alosema majengo na lami.
Afterall lami zimewekwa na serikali na hizo hospital.
Watu wanahoji kuhusu mji wa Bukoba ambao watu wanalala tu na kuongea viingereza bila kujituma
 
Wacha maneno, hakuna alosema majengo na lami.
Afterall lami zimewekwa na serikali na hizo hospital.
Watu wanahoji kuhusu mji wa Bukoba ambao watu wanalala tu na kuongea viingereza bila kujituma
Kwanini unataka watu waamke mapema? Unakwenda kumuhudumia nani? Kila mtu ana schedele ya shghuli zake, huyu RC ni wa ajabu sana. Anaropoka tu bila analysis. Kwa data ipi ambayp ameichapisha na kutoa conclusion hiyo! Unafungua duka kama kuna wateja wa mapema. kama watu hawaji barabarani mapema unafungua ili iweje?
 
Acha kujifariji mkoa wa Simiyu unaizidi kagera nenda bariadi ukaone watu wake walivo na mafanikio ndani ya mkoa wao! Mfano hata geita iko vizuri kuliko kagera japo umasikini upo ila mzunguko wa pesa geita na wananchi wake wanavopiga kazi hawawafikii hata kidogo! Angalia senta zao kama Katoro linganisha na nyinyi huko?
Usilinganishe Geita kwenye ukanda wa dhahabu inayowezesha mzinguko wa fedha na Kagera ambayo hakuna kiwanda wala mgodi wa kuwezesha hilo.
Kagera imekumbwa na vikwazo kadhaa vya kiuchumi vikiwemo vya bahati mbaya na vingine vya maksudi kutoka kwa watawala. Kwa kutaja vichache rejea vita vya Kagera, Anguko la bei ya kahawa na vikwazo lukuki ambalo ni zao kuu la biashara, Kuzama kwa MV Victoria nguvu kazi na mitaji vilipotea, Madhara ya HIV kimkoa, Kuteketea kwa zao la migomba ambacho ni zao la chakula kikuu, Udhibiti wa biashara ya mpakani likiwemo zao la Kahawa usiokuwa na tija unaofanywa na mamlaka za serikali. Zaidi ya yote, Serikali kutojishughurisha ipasavyo kushughurikia majanga yote hayo.

Yawezekana wewe ni kijana mdogo wa juzi kati. Ebu fuatilia historia ya mkoa huo na zao la kahawa(Rejea maneno ya M/M- CCM kwenye ziara inayoendelea kuhusiana na kahawa, hayo yameanza kabla hujazaliwa!!) na hayo mengine. Utaona misumari ambayo Wanakagera wamekuwa wakibebeshwa pasipo hatua sitahiki kuchukuliwa kwa muda stahiki.

Kwa ufupi kinachotajwa kama ujuaji kimesababishwa na watawala, ni kwa wakazi wa Kagera katika namna ya kujinasua kwenye minyororo ya ukandamizaji wa ujanjaujanja na vikwazo lukuki kutoka kwa watawala
 
Back
Top Bottom