RC Chalamila: Tunaweza kuwa na ‘Magufuli Ruling Party’ na mambo yakaenda vizuri kabisa

Kama kuna mtanganyika/mtanzania anaona hizi kauli ni bahati mbaya akapimwe akili. Ukweli ni kua Vibaraka wa Shetani a.k.a Mapoyoyo yameandaliwa waseme wanayosema na kutenda wanayotenda. Shetani MKUU anawatuma hao. KATIBA itabadirishwa kibabe na propaganda itakua, "wananchi/wazalendo wamenisukumia humo milele, nimesikia kilio chenu sitawaangusha, fanyeni kazi" .
 
Huwa najiuliza hiki cheo alipataje huyu kijana? Yaani dah akili yangu huwa inatatizika sana!
Alikipata kupitia CCM, ndo alikuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa. Alivyoteuliwa ukuu wa mkoa akaambiwa achague cheo kimoja, akachagua ukuu wa mkoa.
 
Hivi ni dada yake rayc mana wamefanana sana mpka majina
Mwalimu wa kiswahili huyo, bingwa wa kuchomekea maneno. wanambeya wanamkubali sana huyo mwamba wa lugha, hapo kawaacha CHADEMA , ACT, na wengine kuitafakari kauli hiyo bila majibu
 
Upambe umezidi hadi nuksi.Mwanaume unamsifia vipi mwanaume mwenzio eti nae ni msomi INA Maana ajui faida za vyama vingi. Haya mambo wayafanyayo ni sababu ya pressures ya upinzani.
 
Hao walioteuliwa kwa ajili ya kupambana na chadema wana tabu kweli kweli awajui hata job description ndo madhara ya kuondoa seminar elekezi. Wanachojua ni kupambana na upinzani tu.
 
Alikipata kupitia CCM, ndo alikuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa. Alivyoteuliwa ukuu wa mkoa akaambiwa achague cheo kimoja, akachagua ukuu wa mkoa.

Alishindwa kumng'oa msigwa IRINGA je ataweza kumng'oa sugu Mbeya?Ni kati ya ma rc watakaopigwa chini kwa kushindwa kuwapa ushindi.
 
Alishindwa kumng'oa msigwa IRINGA je ataweza kumng'oa sugu Mbeya?Ni kati ya ma rc watakaopigwa chini kwa kushindwa kuwapa ushindi.
Huyu RC hakuletwa kwa ajili ya kumng'oa Sugu, aliyeletwa kwa ajili hiyo ni Vurugu Jackson. Huyu Chalamila hajui fitna na figisu za siasa ndo maana hotuba zake zina ukakasi wa tamaa za mwili tu.
 
Mwalimu wa kiswahili huyo, bingwa wa kuchomekea maneno. wanambeya wanamkubali sana huyo mwamba wa lugha, hapo kawaacha CHADEMA , ACT, na wengine kuitafakari kauli hiyo bila majibu
Hivi Magufuli Ruling Party ni Kiswahili? Sasa mwalimu wa Kiswahili anapendekeza chama kipya kwa jina la lugha nyingine. Halafu ndio mnasema Kiswahili kitumike kufundishia kwenye ngazi zote za elimu wakati walimu wenyewe wa Kiswahili hawakitaki Kiswahili badala yake wanapendekeza majina ya Kiingereza. Chema chajiuza Kibaya chajitembeza. Naona Kiingereza kinajiuza chenyewe hata kwa walimu wa Kiswahili
 
mnasema maendeleo hayana chama,na mimi nasema kujikomba hakuna chama
 
Vyama vya upinzani vipo kikatiba na ni muhimu kuvilinda ili viendelee kuwepo, ila CCM ndiyo inatakiwa iendelee kutawala daima.
 
Ndio tatizo la kulewa sifa hadi kuvimbewa, unabaki kutoa harufu mbaya pande zote zenye matundu hewa chafu inatoka tuu
 
Mwalimu wa kiswahili huyo, bingwa wa kuchomekea maneno. wanambeya wanamkubali sana huyo mwamba wa lugha, hapo kawaacha CHADEMA , ACT, na wengine kuitafakari kauli hiyo bila majibu
Na wewe kwa kusifia vitu vya hovyo hovyo umejaliwa
 
Pipa na mfuniko!!!
Kutarajia maendeleo endelevu katika fikra za aina hii itakuwa sawa na ndoto ya mchana...
Tunapaswa kujifunza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…