RC Hapi: Jumamosi ya pili ya kila Mwezi itakuwa ni siku ya kufanya mazoezi watumishi wa umma na Wananchi wote mkoa wa Iringa

RC Hapi: Jumamosi ya pili ya kila Mwezi itakuwa ni siku ya kufanya mazoezi watumishi wa umma na Wananchi wote mkoa wa Iringa

Mkuu wa mkoa wa Iringa Salum Happi amesema jopo la madaktari wa mkoa wa Iringa wamemweleza kuwa mkoa huo unanyemelewa na magonjwa nyemelezi kama kisukari nk.

Kufuatia hali hiyo RC Happi amewaagiza Wakuu wa wilaya mkoani humo kuhakikisha kila Jumamosi ya pili ya kila mwezi inakuwa ni siku ya mazoezi ya Umma ambapo watumishi wote na wananchi kwa ujumla watapaswa kufanya mazoezi.

Watakaopuuza hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Source: Channel ten

Maendeleo hayana vyama!
Kwa sheria ipi na kwa kifungu gani?!!!!
 
Mazoezi ya viungo endelevu, ndio yanaweza kuweka miili yetu sawa.
Pia lishe bora nayo ni changamoto.
Kunywa maji ya kutosha kama lita 3 kila siku.
Pia body massage inapunguza tension at least once month kama wafanyavyo South East Asia.
Ventilation ya kutosha kazini na nyumbani.
Usafi wa mazingira yaliokuzunguka.
 
Namuunga mkono kabisa.. Watumishi wengi Sana wanakufa na kisukari ..madaktari wanaweza dhibitisha hili... Mara moja kufanya mazoezi inaweza isitoshe lakini anaanza wajengea watu culture ya kufanya mazoezi... Viongozi wengine Waige hili... Ikiwezekana Iwe kampeni ya kitaifa kabisa
 
Mazoezi ya viungo endelevu, ndio yanaweza kuweka miili yetu sawa.
Pia lishe bora nayo ni changamoto.
Kunywa maji ya kutosha kama lita 3 kila siku.
Pia body massage inapunguza tension at least once month kama wafanyavyo South East Asia.
Ventilation ya kutosha kazini na nyumbani.
Usafi wa mazingira yaliokuzunguka.
Walivyo na fikra fupi wanadhani mazoezi ni kukimbia tu kama wehu mabarabarani. Mazoezi mengine hufanyika nyumbani si lazima uende katika viwanja vya michezo.
 
Happy hajui kabisa what is leadership, hv anafikiri watumishi wa umma kama watumwa wake? Jmosi & jpili ni siku za mapumziko kisheria na sheria zinawalinda watumishi, huwezi kukurupuka tu na kujiamualia lolote lile juu ya watumishi, hao sio watumwa wana haki na stahiki zao kisheria. Very wrong guy to be RC
 
Na wale ambao jumamos ndio siku ya ibada je wao watafanyweje?
 
Back
Top Bottom