RC Makala: Wafanyabiashara ndogo ndogo kupangwa upya Dar es Salaam, walioko barabarani kuondolewa

RC Makala: Wafanyabiashara ndogo ndogo kupangwa upya Dar es Salaam, walioko barabarani kuondolewa

Mkuu
Dar ingekuwa jiji la mfano hata sisi tukiingia tujisikie kuwa Tanzania kuna mji mzuri. Sasa hivi huko Buguruni, Ubungo, Karume, Tegeta hapana tofauti na Lindi
Mkuu leo Mbezi/Kimara utadhani watu wako eneo la machimbo ya madini, vibanda vyenye maturubai chakavu vimetamalaki.
 
Mkuu wa mkoa Ana Nia njema kabisa ya kuwasaidia Hawa wafanyabiashara mdogomdogo hasa wakipangiwa eneo lao maalum itapendeza Sana.
Niwaambie hao madiwani na wenyeviti wa mtaa kuwa nao Wana jukumu la kuwapanga Hawa machinga vizuri ili iwe rahisi kwao kukusanya ushuru.
Pia serikali za mitaa watoe maeneo na kuruhusu yawe magulio ya kila siku ili waweze kukusanya mapato ya kuziendesha halmashauri zao. Mbona ni kazi nyepesi Sana hasa wakiweke ukada wa kutafuta hizo cheap popularity na kuisaidia serikali kupata mapato!

Kabisa ni kazi rahisi sana. Miundombinu ya kawaida sana. Mabati, zege au lami chini, miundombinu ya maji taka, Vyoo visafi vya kutosha, Parking, sehemu za kupakua mizigo yao na abiria.

Wanaweza wakapewa meza na kawaida sana. Kila kibanda kinakuwa na namba. Asubuhi wakilipa kiingilio wanapewa meza.

Pia magulio yawepo siku zote za wiki. Vitu kama hivi havitushindi.

1622629602399.png

1622629747426.png
 
Leo RC Makalla amekaa na madiwani kuwaelezea nia yake ya kuwapanga upya wamachinga ktk jiji hili la kibiashara

Chanzo: ITV habari

Wamachinga walipewa Uhuru usiyokuwa na mipaka kiasi kwamba waligeuka kuwa kero kwa kila mtu.

Uamuzi wa RC Makalla uungwe mkono ili hawa wanyonge wafuate utaratibu. Na wawe na maeneo maalumu ya kufanyia kazi zao. Wasizagae hovyo.
Juzi nilipita Posta kuna machinga anauza mpaka geti kuu la kuingia bank, mama lishe amewasha jiko la mkaa kwenye lami ndani ya mchoro wa zebra. Katika vitu ambavyo Mzee Jiwe alikosea ni kuwapa wamachinga uhuru uliopitiliza! Sasa hivi itamcost RC wa Dar kupanga jiji. Madiwani watamuunga mkono? Au watakuwa upande wa machinga na mama ntilie? RIP Jiwe!
 
Kujali mazingira ya usafi, magonjwa, ajali bado tuko nyuma. Ubunifu mdogo.
Na hili tatizo ccm wanalilea kwasababu wanachagua viongozi wenye elimu mdogo imayowakosesha ubunifu na kufikiri sawasawa! Laiti wangeweka vigezo vya kupata uenyekiti wa serikali ya mtaa, diwani, mbunge na hata waziri waombe hizo nafasi wakitumia CVS zao hakika nchi yetu ingepaa kiuchumi kwani kila mwananchi angelipa Kodi!
Lakini wanachaguana kwa vigezo vya kuzidiana uchawi na ulozi! Hatutafika hata rais angekuwa malaika!
 
Sio Dar es Salaam tu...

Huku Mwanza City nako ni balaa hususani ikifika masaa ya jioni kuanzia saa 10 na kuendelea...

Hawa watu huziba barabara zote za waenda kwa miguu katikati ya jiji kiasi cha kuhatarisha maisha yao na ya wengine has a waenda kwa miguu kwani badala ya kutembelea kwenye njia zao (pedestrian), hutembelea kwenye barabara za magari kwa sababu pedestrian road hugeuzwa kuwa meza za nyanya, vitunguu, dagaa nk kila aina ya bidhaa...

Jamani tukubaliane tu kuwa maendeleo haina maana ya kuwa na vitu tu (barabara nzuri, majengo mazuri, ndege nk nk...

Maendeleo ni pamoja na ustaarabu wa watu, kuheshimu sheria na utaratibu, kutunza mazingira na mambo mengine yafananayo na hayo...
 
Kabisa ni kazi rahisi sana. Miundombinu ya kawaida sana. Mabati, zege au lami chini, miundombinu ya maji taka, Vyoo visafi vya kutosha, Parking, sehemu za kupakua mizigo yao na abiria.

Wanaweza wakapewa meza na kawaida sana. Kila kibanda kinakuwa na namba. Asubuhi wakilipa kiingilio wanapewa meza.

Pia magulio yawepo siku zote za wiki. Vitu kama hivi havitushindi.

View attachment 1805849

View attachment 1805851
Hii ni wapi chief?
 
Juzi nilipita Posta kuna machinga anauza mpaka geti kuu la kuingia bank, mama lishe amewasha jiko la mkaa kwenye lami ndani ya mchoro wa zebra. Katika vitu ambavyo Mzee Jiwe alikosea ni kuwapa wamachinga uhuru uliopitiliza! Sasa hivi itamcost RC wa Dar kupanga jiji. Madiwani watamuunga mkono? Au watakuwa upande wa machinga na mama ntilie? RIP Jiwe!
Jiwe alikuwa kiongozi wa hovyo sana
 
Hii ni wapi chief?

Huko duniani. Ila hata sisi tunaweza kujipanga, hakuna ugumu wowote nia ya dhati, mikakati, utekelezaji.

Uzuri ni kwamba yoyote anaweza kuuza, unakuja asubuhi unalipa labda 5000. Unapewa ticket namba ya meza. Uzuri wa huu utaratibu unajua ni watu wangapi wameingi, mahitaji ni kiasi gani.

Serikali itapata kodi stahiki, rahisi kuweka mipango thabiti.
 
Na hili tatizo ccm wanalilea kwasababu wanachagua viongozi wenye elimu mdogo imayowakosesha ubunifu na kufikiri sawasawa! Laiti wangeweka vigezo vya kupata uenyekiti wa serikali ya mtaa, diwani, mbunge na hata waziri waombe hizo nafasi wakitumia CVS zao hakika nchi yetu ingepaa kiuchumi kwani kila mwananchi angelipa Kodi!
Lakini wanachaguana kwa vigezo vya kuzidiana uchawi na ulozi! Hatutafika hata rais angekuwa malaika!

Muhimu kuruhusu wagombea binafsi katika level zote. Kuanzia serikali za mitaa hadi Uraisi.

Ukifanya hivyo unaweza kupata viongozi wa ukweli, wanaojali, wabunifu.

Wananchi wengi ( majority) hawako kwenye chama chochote. Uchaguzi uliopita waliopiga kura kwa vyama vyote ni chini ya 15m Tanzania ina watu 60m.

Kwahiyo kuna vipaji vingi havina nafasi kulitumikia taifa lao.
 
Nakushukuru Sana Mh Makalla kwa kuona jambo hili ni KERO iliyopitiliza huko barabara kila mahali majiko ya mkaa vituo vya daladala vimehodhiwa huthubutu kumwambia mmachinga pisha au sogeza vitu nipite na gari wanavunja VIOO na matusi ya nguoni Waelekezwe waende hata ndani ya viwanja kuliko hii vurugu ya kutafuta siasa RAHISI
 
Back
Top Bottom