RC Makala: Wafanyabiashara ndogo ndogo kupangwa upya Dar es Salaam, walioko barabarani kuondolewa

RC Makala: Wafanyabiashara ndogo ndogo kupangwa upya Dar es Salaam, walioko barabarani kuondolewa

Hayati alikosa exposure hakuna mji duniani uko ovyo kama dar,mamalishe anapikia kuni chini ya transfoma pembeni kuna bank mbele kuna jengo la ubalozi.Mungu fundi
Hawa waliitwa Wanyonge aka Wapiga Kura.
 
Mkuu wa mkoa Ana Nia njema kabisa ya kuwasaidia Hawa wafanyabiashara mdogomdogo hasa wakipangiwa eneo lao maalum itapendeza Sana.
Niwaambie hao madiwani na wenyeviti wa mtaa kuwa nao Wana jukumu la kuwapanga Hawa machinga vizuri ili iwe rahisi kwao kukusanya ushuru.
Pia serikali za mitaa watoe maeneo na kuruhusu yawe magulio ya kila siku ili waweze kukusanya mapato ya kuziendesha halmashauri zao. Mbona ni kazi nyepesi Sana hasa wakiweke ukada wa kutafuta hizo cheap popularity na kuisaidia serikali kupata mapato!
 
Naunga hoja,na hili lisiishie Dar pekee,lisambae majiji yote,mwaka huu kidogo nigongwe na coster nikiwa Mwanza maeneo ya Natta kisa vibanda vya machinga maaana sikuweza kuona gari lililokuwa upande wangu kwenye Kona

Mungu alikuwa upande wangu ,nashukuru Niko mzima lakini Hawa watu ni hatari Sana kwa afya za biniadamu wenzao
 
Na wale wamachinga kwenye kituo cha mabasi cha Magufuli nao ni kero tu uwekwe utaratibu mzuri vinginevyo miundombinu na ubora wa stend yenyewe utafifia.
 
Hayati alikosa exposure hakuna mji duniani uko ovyo kama dar,mamalishe anapikia kuni chini ya transfoma pembeni kuna bank mbele kuna jengo la ubalozi.Mungu fundi
Mitaa ya kama unaelekea BOT kuna mwana alikuwa anachoma mshikaki na ndizi
Kwengine mtu katundika minguo anauza mitumba,basi vurumaiii

Ova
 
Mmetulipisha kitambulisho cha machinga ili msitusumbue, watch it mnachezea legasi😡
 
Hakuna bavicha wa kufanya vurugu nchi hii bwashee!
Ile kauli ya mwendamahoka ya kuwa " msiwafukuze Wala kuwabugudhi kwani ndio walionipa Kura"! Hao walikuwa bavicha? Acha kunywa banana mchana! Unafahamika Sana mtaani kwetu kuwa wewe ni ccm maslahi na mwabudu mwendamahoka!
 
Vile vitambulisho visivyo na jina Wala picha viliishia wapi?
 
Hili la wamachinga ni time bomb
Rais Samia asiliendee kichwakichwa, litamuondolea kuaminika na kuungwa mkono na maelfu ya wamachinga akiliendea kwa pupa

Hakuna short term solution kwenye ishu ya wamachinga, linahitaji bajeti, ujenzi wa miundo mbinu ya kuwaaccomodate n. k

Isitoshe, Wamachinga walihakikishiwa na serikali kutosumbuliwa, Sasa Samia atimize ilani na ahadi waliyoitoa kwa wamachina mwaka 2020, la sivyo hii ni hadaa.

Serikali ya Magufuli ambayo Samia alikuwa makamu wake iliwahakikishia Wamachinga kutowasumbua, na hadi 20000 za vitambulisho ikawatoza, Sasa iweje awageuke? —Hii itamsumbua sana Samia, It is a political gamble akifanya hili KWA SASA BILA MIUNDO MBINU YA KUWAACCOMODATE WAMACHINGA

Tuchague moja, kile tunachokiita uchafu wa Machinga, au jeshi la vijana lililokata tamaa kwa kushindwa kujiajiri.
Ule ni uchafu tu hao çhinga ni asilimia ngapi ya wapiga kura
 
Back
Top Bottom