RC Makala: Wafanyabiashara ndogo ndogo kupangwa upya Dar es Salaam, walioko barabarani kuondolewa

RC Makala: Wafanyabiashara ndogo ndogo kupangwa upya Dar es Salaam, walioko barabarani kuondolewa

Ila siku magari yakiwazoa wakafa bado atalaumiwa serikali sio?.

taratibu lazima zifuatwe jmn.,
Machinga complex iko pale wamejaa popo tu
Wana siasa kama wa mawazo yenu walipaharibu. Umeona wapi unajenga viriba vya ndege watu waiingie humo ili mradi viwe vingi
 
RC Makala amesema wafanyabiashara ndogondogo jijini Dar es salaam wamekaa bila utaratibu maalumu na barabara zimezibwa na sasa wanalikaribia geti la Ikulu.

Makala amesema hali hii haikubaliki na ni lazima wafanyabiashara hao wapangwe upya katika utaratibu rasmi kwenye maeneo yote ya mkoa na waliopo barabarani na mbele ya maduka au ofisi za watu wengine wataondolewa.

Chanzo: ITV habari!
Ukipita kwenye lango la chuo cha IFM na Wizara ya Afya ni aibu
 
Du kazi imeanza tunaomba iishe salama. Huu ulikuwa cheap popularity za mwendazake zimetutumbukiwa kwenye enzi za ujima. Ploe sans Rias wetu Kazi iendelee.
 
Ila siku magari yakiwazoa wakafa bado atalaumiwa serikali sio?.

taratibu lazima zifuatwe jmn.,
Machinga complex iko pale wamejaa popo tu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] sasa unataka wajae Nan? Kila mtu yuko barabaran watu wako wengi wanunuzi.
 
Hii ingefanyika Tanzania nzima.Hawa wapangishe frame ya duka,ili kuingiza mapato ya serekali kwenye kodi ya zuio(with holding Tax)Frem nyingi kwenye miji,zimejengwa,hazina wapangaji,wakipatikana wapangaji na kodi ya zuio,imepatikana.Wengi wanaingiza faida kubwa,lakini hawalipi kodi.
Bora hao wenye fremu wakose wapangaji maana wanatoza kodi kubwa sana
 
Siasa ndiyo imechangia kuliharibu jiji..wanasiasa wenye mawazo muflisi kama haya ndio wamesababisha jiji limekuwa la vibanda kile sehemu. Huwezi kutofautisha manzese na posta. Na hii imezagaa maeneo yote,...Mwanza kule ndio kabisa hata gari haliwezi kupita.
Kwani manzese na posta watu wake wanatofautiana
 
Huo upangaji machinga utakuwa kituko tu. Tusubiri tuone

Huwa tunafanya mambo kwa kukariri au kwa kukopi na kupesti. Kusipokuwepo na kukariri na kukopi na kupesti tunaishia kuharibu tu.

Utataka ukopi kutoka london, new york halafu upestie dar. Ndo maana tunashindwa. Tunalazimishia kupestia kwetu tulivyokopi huko sababu ya uzembe na uvivu wa kufikiri na kufanya kazi.

Nakubali huwezi kupikia chini ya transfoma na kujenga banda lako mbele ya Duka LA mwenzio lakin shughuli nyingi wanazofanya hao machinga wala hazina shida yoyote kuendelea kama zilivyo zaidi Labda ya marekebisho madogo madogo ya hapa na pale
 
ni Jambo zuri, yaani wafanyabiashara ndogondogo wamekaa ovyo ovyo afadhali hata viazi.
kariakooo ovyoooo.....hakuna utaratibu unao eleweka biashara zinapangwa hadi kwenye mitaro ya maji taka!!
uongozi upo kama haupo!!
RC Makala anapaswa afanye zoezi la kuwapanga tena mapema iwezekanavyo.
tunatakiwa kuona barabara za mitaa ya tandamti, kongo na mitaa mingine inapitika bila kiziwizi chochote sio kama ilivyo sasa.
 
Wana siasa kama wa mawazo yenu walipaharibu. Umeona wapi unajenga viriba vya ndege watu waiingie humo ili mradi viwe vingi
Sasa barabarani humo hata kodi wanalipaje?

watu kipato wanapata ila kulipa kodi hawataki inawezekana vipi?.

wapangwe walipe kodi
 
Subiri kwanza mkuu litokee semi imefeli break ikishachukua roho kadhaa ndio tutachukua hatua.

Sisi ndio tulivyo.
Mimi natamani siku moja gari limpandie yule mtu pale friends corner arusha limvunje kiuno kabisa,amefunga njia ya waenda kwa miguu na ukijaribu kumuomba asogee anakutukana mbaya kabisa,yupo hapo posta ya zamani ukivuka tu barabara kutokea crdb, afie mbali huko
 
Hiyo sehemu ina kero mbaya. Hasa ikifika jioni ndio wale wa soko kuu nao wanajazana barabarani mara hiace na wapiga debe asee kero tupu.

Huyu mzee aliharibu kutaka kujipatia umaarufu kwa aliowaita wanyonge kwa kuruhusu biashara kufanyika popote.
 
ni Jambo zuri, yaani wafanyabiashara ndogondogo wamekaa ovyo ovyo afadhali hata viazi.
kariakooo ovyoooo.....hakuna utaratibu unao eleweka biashara zinapangwa hadi kwenye mitaro ya maji taka!!
uongozi upo kama haupo!!
RC Makala anapaswa afanye zoezi la kuwapanga tena mapema iwezekanavyo.
tunatakiwa kuona barabara za mitaa ya tandamti, kongo na mitaa mingine inapitika bila kiziwizi chochote sio kama ilivyo sasa.
mbagala rang tatu je? pale ni janga yan kwanz kuna mrad mkubwa ambao ni aibu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zoezi gumu hili. Ajira hakuna, kila kijana kaamua kuwa mmachinga. Hayo maeneo ya kuwapeleka yako wapi?

chochote kilichopo sehemu isiyotakiwa kuwepo ni uchafu.

Nakumbukia sayansikimu yangu ya darasa la tatu!
 
Back
Top Bottom