RC Makalla: Kuanzia usiku wa leo hakuna Panya Road atasalimika, operesheni inayoanza si salama kwao

Well said kutoa threat tegemeo watu wasio na hatia kukamatwa
 
Polisi huwa wakiuwa jambazi humu Jf mnaleta maneno ooh kwann wamemuaa kwann wasingempeleka mahakaman
Sasa mi naomba polisi wasihangaike kabisa na hao vijana waachane nao tu raia wenyewe watawakamata wawapeleke mahakamani
 
Siraha nyingine ya kujilinda dhidi ya waharamia kama hawa ni kutembea na 'Pepper spray'. Akikusogelea una spray pilipili machoni kwake. Lazima atimue mbio. Hapa sasa inabidi uwe na ki-spray kidogo kiwe portable. Kama una gari unakuwa na chupa kubwa kidogo. Ukitembea unaweka kwenye koti.
 
Kazi ya week moja tu hiyo wakiwa serious, mji utakuwa salama kabisa...uzuri wake Polisi wanawajua woote...wakianza kupunguza mmoja mmoja wengine wataanza kukimbilia vijijini kwao....wengi ni kula kulala watoto wa mama..

Ukiona mtu anafanya wizi wa kifala kuwaibia wanyonge uswazi huko ujue mtoto wa mama tu huyo muoga bado anapenda kuishi...
 
Naipata wapi
 
Tunataka vitendo, siyo maneno maneno tuu yasiyokuwa na msingi.
 
Hakutakiwa kuongea kabisa hiyo kaz ingefanywa kimya kimya bila makelele hao wahalifu watakimbia wanaweza kimbilia Moro au Tanga hii operations ingefanywa kimya kimya tu
 
Naipata wapi
Hebu jaribu ku-google uandike 'self defence body spray' au Pepper spray self protection'. Utaona zinakouzwa kwa hapo Dar. Mie nime-google naona kuna hadi watu wanaziuza zoom Tanzania (Kinondoni. Tsh 40K). Sema siwezi weka link JF wazije wakanipiga ban. Hawaruhusu kuweka link humu.

Hizi spray pia zinatumika haswa kwa wadada wanaoenda kutoa huduma nyumbani kwa mtu kwa kazi kama usafi ama kazi za ndani kwa siku. Akifika kwa boss ake kisha boss akataka kumfanyia unyanyasaji wa kijinsia, mdada anatoa kwenye kimkoba chake na kum-spray huyo janaume. Hatarudia tena kunyanyasa wanawake.

Nimekupa mbinu zaidi mkuu. Elimisha na wengine huko uliko. Ulinzi binafsi ni jukumu lako kwanza kabla Polisi hawajafika.
 
Panya road nini? Siamini kabisa kwamba kuna watu wanaitwa Panya road ila kuna wezi wanaotumia mapanga kuvamia watu kuwaibia na kuwajeruhi wanotaka kuwazuia wasichukue wanachotaka.
Kwa vyovyote iwavyo polis baadhi wanahusika katika matukio aya haiwezekani wezi wateke mtaa mzima afu polis washindwe kuwanasa. Kibaya zaidi wanaiba mchana mimi sikubaliani na ayo majina yenu mnayobatiza wezi kwakuwaita Panya road.
 

Hapa ndiyo nasema waimarishe ulinzi shirikishi.wale wanawajuwa waharifu wa mtaani kwao.Yaani badala ya kuwatafuta hewani kama ilivyo sasa wangeweza kuwafuata majumbani mwao kabisa.kwa sababu kila mtaa nyumba zinazofuga vibaka zinajulikana.Ijapokuwa ni maumivu sana kwa mzazi(Hasa mama) kuona mwanae anakamatwa na kuteswa.Ila hiyo ni gharama ya kumdekeza mtoto wako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…