RC Makalla: Kuanzia usiku wa leo hakuna Panya Road atasalimika, operesheni inayoanza si salama kwao

RC Makalla: Kuanzia usiku wa leo hakuna Panya Road atasalimika, operesheni inayoanza si salama kwao

Hii kauli inatia shaka sn..

Katika nchi za kiafrika,ukisikia kiongozi ameongea kauli km hii, kinachofuata hapo ni mateso Kwa wanaohusika na wasiohusika..nguvu unayotumika inakuwa nyingi sn alafu akili kisoda

Wengi waneuawa Kwa staili hii Kwa kisingizio cha neno "tunafanya operation maalum"

Hapa mzazi km Una mtoto wako wa kiume kuanzia 8-21 years,wiki hii mkataze mitoko ya jioni hasa mambo ya mipira ya 'chandimu'..polisi wanasomba wote wanakuwa ktk vikundi vikundi,mtajieleza mkifika kituoni

Naongea Kwa experience kubwa Kwa sababu nimekulia uswahili Temeke,tandika,Sheraton,maputo,relini,buza na viunga vyake..Enzi za Yule Askari mbabe wa kuitwa Tyson,jamaa anawakamata,kisha anawatembeza Kwa miguu na Pingu hawafungi alafu anauliza ambae anajiona ana ubavu wa kupigana na Mimi ajitokeze,akinishinda namruhusu asepe..sijui Yuko wapi Yule jamaa siku hizi

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
Well said kutoa threat tegemeo watu wasio na hatia kukamatwa
 
View attachment 2208639

Yaani mbinu nzuri ingekuwa ile ya kipindi cha Augustino, mzazi au ndugu unapewa taarifa kachukue maiti sehemu fulani au mochuari.

Hiyo ya nenda kituo cha polisi imekaa kama ina upendo fulani hivi!.

IMG_20220502_201642.jpg
 
Polisi huwa wakiuwa jambazi humu Jf mnaleta maneno ooh kwann wamemuaa kwann wasingempeleka mahakaman
Sasa mi naomba polisi wasihangaike kabisa na hao vijana waachane nao tu raia wenyewe watawakamata wawapeleke mahakamani
 
Siraha nyingine ya kujilinda dhidi ya waharamia kama hawa ni kutembea na 'Pepper spray'. Akikusogelea una spray pilipili machoni kwake. Lazima atimue mbio. Hapa sasa inabidi uwe na ki-spray kidogo kiwe portable. Kama una gari unakuwa na chupa kubwa kidogo. Ukitembea unaweka kwenye koti.
 
Kazi ya week moja tu hiyo wakiwa serious, mji utakuwa salama kabisa...uzuri wake Polisi wanawajua woote...wakianza kupunguza mmoja mmoja wengine wataanza kukimbilia vijijini kwao....wengi ni kula kulala watoto wa mama..

Ukiona mtu anafanya wizi wa kifala kuwaibia wanyonge uswazi huko ujue mtoto wa mama tu huyo muoga bado anapenda kuishi...
 
Siraha nyingine ya kujilinda dhidi ya waharamia kama hawa ni kutembea na 'Pepper spray'. Akikusogelea una spray pilipili machoni kwake. Lazima atimue mbio. Hapa sasa inabidi uwe na ki-spray kidogo kiwe portable. Kama una gari unakuwa na chupa kubwa kidogo. Ukitembea unaweka kwenye koti.
Naipata wapi
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amesema "Kuanzia leo, baada ya tamko langu leo, usiku wa leo na kuendelea hakuna 'Panya Road' atasalimika katika mkoa wa Dar, oparesheni inayoanza usiku wa leo si salama kwa 'Panya Road', oparesheni inayoanza leo inaenda kuua uti wa mgongo wa mtandao mzima wa 'Panya Road"

Ameongeza "Niwasihi wazazi kwamba operesheni hii haitowaacha watoto wao wahalifu, kama mzazi ulizoea kupata zawadi kwa mtoto, TV bila kujua kipato chake, akudanganye 'amebeti', kawatafuteni watoto wenu kwenye vituo vya Polisi kuanzia kesho"

Amesisitiza "Kila Wilaya kwa mikoa ya Kipolisi, kutoa taarifa za kila siku za Operesheni ondoa 'Panya Road' na kudhibiti uhalifu katika mkoa wa Dar es Salaam kila siku, toeni taarifa tusipotoa taarifa watazitoa taarifa mbaya"

Ameyasema hayo siku moja baada ya kundi hilo la uvamizi kuvamia na kujeruhi watu 19 katika Maenel ya Mtongani, Kunduchi mkoani humo
Tunataka vitendo, siyo maneno maneno tuu yasiyokuwa na msingi.
 
Hakutakiwa kuongea kabisa hiyo kaz ingefanywa kimya kimya bila makelele hao wahalifu watakimbia wanaweza kimbilia Moro au Tanga hii operations ingefanywa kimya kimya tu
 
Naipata wapi
Hebu jaribu ku-google uandike 'self defence body spray' au Pepper spray self protection'. Utaona zinakouzwa kwa hapo Dar. Mie nime-google naona kuna hadi watu wanaziuza zoom Tanzania (Kinondoni. Tsh 40K). Sema siwezi weka link JF wazije wakanipiga ban. Hawaruhusu kuweka link humu.

Hizi spray pia zinatumika haswa kwa wadada wanaoenda kutoa huduma nyumbani kwa mtu kwa kazi kama usafi ama kazi za ndani kwa siku. Akifika kwa boss ake kisha boss akataka kumfanyia unyanyasaji wa kijinsia, mdada anatoa kwenye kimkoba chake na kum-spray huyo janaume. Hatarudia tena kunyanyasa wanawake.

Nimekupa mbinu zaidi mkuu. Elimisha na wengine huko uliko. Ulinzi binafsi ni jukumu lako kwanza kabla Polisi hawajafika.
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amesema "Kuanzia leo, baada ya tamko langu leo, usiku wa leo na kuendelea hakuna 'Panya Road' atasalimika katika mkoa wa Dar, oparesheni inayoanza usiku wa leo si salama kwa 'Panya Road', oparesheni inayoanza leo inaenda kuua uti wa mgongo wa mtandao mzima wa 'Panya Road"

Ameongeza "Niwasihi wazazi kwamba operesheni hii haitowaacha watoto wao wahalifu, kama mzazi ulizoea kupata zawadi kwa mtoto, TV bila kujua kipato chake, akudanganye 'amebeti', kawatafuteni watoto wenu kwenye vituo vya Polisi kuanzia kesho"

Amesisitiza "Kila Wilaya kwa mikoa ya Kipolisi, kutoa taarifa za kila siku za Operesheni ondoa 'Panya Road' na kudhibiti uhalifu katika mkoa wa Dar es Salaam kila siku, toeni taarifa tusipotoa taarifa watazitoa taarifa mbaya"

Ameyasema hayo siku moja baada ya kundi hilo la uvamizi kuvamia na kujeruhi watu 19 katika Maenel ya Mtongani, Kunduchi mkoani humo
Panya road nini? Siamini kabisa kwamba kuna watu wanaitwa Panya road ila kuna wezi wanaotumia mapanga kuvamia watu kuwaibia na kuwajeruhi wanotaka kuwazuia wasichukue wanachotaka.
Kwa vyovyote iwavyo polis baadhi wanahusika katika matukio aya haiwezekani wezi wateke mtaa mzima afu polis washindwe kuwanasa. Kibaya zaidi wanaiba mchana mimi sikubaliani na ayo majina yenu mnayobatiza wezi kwakuwaita Panya road.
 
Mawazo ya kipuuzi kbs na mawazo km haya ndy wanakuwa Nayo polisi baadhi wakishapewa kazi ya kuingia mtaani kutafuta wahalifu..

Enzi hizo za wahuni wa Temeke Mimi nimewahi kusombwa polisi kisa tupo kitaani tunacheza draft na polisi wanatafuta vikundi vya kihalifu

Wangekuwa na mawazo km yako wengi tungekufa bila hatia

Km umezaliwa uswahilini wanakotokea hawa panya road,mburahati,kigogo,manzese,tandika nk haiwezi kuepuka kukutwa na majanga ya kihalifu ktk safari ya maisha yako..

Hao watoto wamejikuta Tu wamezaliwa uswahilini,hawakujichagulia wao wenyewe ingawa uhalifu ni Jambo walilolichagua..Polisi wakiingia mtaani wanachojua wanaenda kukamata panya road uswahilini,sasa mara kadhaa inatokea wanakamatwa na wasiohusika..Je,kuua ni solution?? Fikiria tena mkuu!!

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app

Hapa ndiyo nasema waimarishe ulinzi shirikishi.wale wanawajuwa waharifu wa mtaani kwao.Yaani badala ya kuwatafuta hewani kama ilivyo sasa wangeweza kuwafuata majumbani mwao kabisa.kwa sababu kila mtaa nyumba zinazofuga vibaka zinajulikana.Ijapokuwa ni maumivu sana kwa mzazi(Hasa mama) kuona mwanae anakamatwa na kuteswa.Ila hiyo ni gharama ya kumdekeza mtoto wako
 
Back
Top Bottom