RC Makalla: Kuanzia usiku wa leo hakuna Panya Road atasalimika, operesheni inayoanza si salama kwao

RC Makalla: Kuanzia usiku wa leo hakuna Panya Road atasalimika, operesheni inayoanza si salama kwao

huu nao ni kama uoga sasa unataka kwenda kuwa kabili panya road then unawatangazia ili iweje yani wakijificha ili kukwepa operation je itakua ime solve tatizo?

Muhimu kuwapa Taarifa. Wahuni wote wasionekane mjini.
 
Mawazo ya kipuuzi kbs na mawazo km haya ndy wanakuwa Nayo polisi baadhi wakishapewa kazi ya kuingia mtaani kutafuta wahalifu..

Enzi hizo za wahuni wa Temeke Mimi nimewahi kusombwa polisi kisa tupo kitaani tunacheza draft na polisi wanatafuta vikundi vya kihalifu

Wangekuwa na mawazo km yako wengi tungekufa bila hatia

Km umezaliwa uswahilini wanakotokea hawa panya road,mburahati,kigogo,manzese,tandika nk haiwezi kuepuka kukutwa na majanga ya kihalifu ktk safari ya maisha yako..

Hao watoto wamejikuta Tu wamezaliwa uswahilini,hawakujichagulia wao wenyewe ingawa uhalifu ni Jambo walilolichagua..Polisi wakiingia mtaani wanachojua wanaenda kukamata panya road uswahilini,sasa mara kadhaa inatokea wanakamatwa na wasiohusika..Je,kuua ni solution?? Fikiria tena mkuu!!

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
Wakikamatwa wakiwa kwenye matukio ni sahihi kuwamaliza
 
Kama wamejichagulia kua wahalifu then bunduki Ni halali Yao hata kupigwa miti pia yafaa wapigwe.
 
Kule Kenya wakati Kibaki (R.I.P.) anaingia Madarakani, alikuta tatizo kubwa la chokoraa , watoto wa mtaani.

wakifanya uhalifu kwenye mitaa ya Nairobi na Viunga vyake, ilikuwa ni tatizo kweli siyo mchezo.
Alikaa na taasisi mbali mbali kuona namna ya kummaliza hilo tatizo,

Vilianzishwa vituo mbali mbali wakakusanywa ,wakapewa elimu ikawaingia ,wengi walikuwa na urahibu wa kuvuta (Gam) yaani chupa ya plastic ndogo inawekwa gundi patex inachanganywa na petrol,walikuwa ni hatari sana ukikutana nao kwenye anga zao.
Baada ya kuwakusanya walipelekwa kwenye vituo vya ufundi vilivyokuwa vimeanzishwa kila mmoja kwa namna alivyopenda awe kama ni fundi Magari, Selemara,Uchomeleaji nk.
Hii kitu ilisaidia sana kupunguza uhalifu kwenye jamii na wengi walipungua mtaani.

Naona na hapa kwetu inahitajika hekima siyo nguvu tu ili kummaliza hili tatizo ,huenda hawa wanafanya hivi sababu ya hali zao kimaisha .

Ndiyo wakamateni wawekwe sehemu waulizwe kwa nini wanafanya uhalifu wa namna hii vijana bado wadogo wanahitaji msaada kwa kweli.

Wasaidiwe zipo taasisi zinazoshughulikia haya mambo , wapelekwe vyuo vya ufundi wapate ujuzi wao wa kuwasaidia ili kuachana na uhalifu wa namna hii.

Lakini suala la kuwaua ,utaua na wengine wasio na hatia, hapa hekima kubwa itumike ni watoto wetu hawa , ni wadogo zetu hawa, ni wajukuu zetu hawa, tunaishi nao mtaani tunawafahamu tuwashauri.

Huenda ni urahibu wa Madawa ya kulevya unapelekea yote haya .
Panyaroad ni matokeo ya failure state kutimiza majukumu yake.
Hivi mfano kungekuwa na vyuo vya ufundi kama veta KILA kata ingesaidia kuwapa vijana matumaini na sio hili la kuwaacha wajiongoze wenyewe
 
HAKUNA kitu hapo.solution NI kumwaga vijana wa JKT na JWTZ mitaani wazurure zurure TU waache kukaa makambini.
Kulinda usalama wa raia ni kazi inayohitaji mafunzo ambayo wanajeshi hawana. Na zaidi, kuwa na mazoea ya kutumia wanajeshi kulinda mitaani siyo jambo zuri hata kidogo na mara nyingi linakuja na matokeo hasi.
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amesema "Kuanzia leo, baada ya tamko langu leo, usiku wa leo na kuendelea hakuna 'Panya Road' atasalimika katika mkoa wa Dar, oparesheni inayoanza usiku wa leo si salama kwa 'Panya Road', oparesheni inayoanza leo inaenda kuua uti wa mgongo wa mtandao mzima wa 'Panya Road"

Ameongeza "Niwasihi wazazi kwamba operesheni hii haitowaacha watoto wao wahalifu, kama mzazi ulizoea kupata zawadi kwa mtoto, TV bila kujua kipato chake, akudanganye 'amebeti', kawatafuteni watoto wenu kwenye vituo vya Polisi kuanzia kesho"

Amesisitiza "Kila Wilaya kwa mikoa ya Kipolisi, kutoa taarifa za kila siku za Operesheni ondoa 'Panya Road' na kudhibiti uhalifu katika mkoa wa Dar es Salaam kila siku, toeni taarifa tusipotoa taarifa watazitoa taarifa mbaya"

Ameyasema hayo siku moja baada ya kundi hilo la uvamizi kuvamia na kujeruhi watu 19 katika Maenel ya Mtongani, Kunduchi mkoani humo
Watuachie tu tuwaue jamani, tumewachoka sasa hata na polisi hatuwaamini kwani tunahisi wanashirikiana nao.
 
Kwani sheria ya kupeleleza kwanza kabla ya kukamata imefutwa au umesimamishwa kwa muda?
Jambazi aliye site unamkamata wa nini? Au unapeleza nini? Kinachotakiwa ni exchange of fire between the police and the suspect. That's all
 
Back
Top Bottom