RC Makonda anafanya lile Watanzania Tunataka. Wanaomchukia ukiwauliza hata sababu hawana wamerithishwa chuki

RC Makonda anafanya lile Watanzania Tunataka. Wanaomchukia ukiwauliza hata sababu hawana wamerithishwa chuki

instagramer

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2024
Posts
215
Reaction score
492
WanaBodi..

Kwa wale tunaofatilia siasa za nchi hii kwa ukaribu naamini tunamfatilia na Makonda katika hatua zake zote za uongozi.

Anachokifanya Makonda kwa Sasa toka amerudishwa kwenye ulingo wa uongozi Wa kisiasa ndio kile kile ambacho Watanzania waliowengi ambao ni Masikini waliokata tamaa na kuvunjika Moyo, wanataka kusikia. Na kumbuka hili ndio Kundi kubwa la Wananchi wa Tanzania. Katika muktadha huo utaona umaarufu wa Makonda unaongezeka Kila uchwao. Kwa maana njia anayopita ndio aliyopitia Hayati Magufuli ambapo mpaka Sasa asilimia kubwa ya wanyonge inamkumbuka. Makonda pamoja na kusaidia pakubwa kutatua changamoto za Wananchi katika nafasi anazopewa Ila pia anajijenga Sana kitaasisi (hafanyi makosa) kiasi kwamba ananguvu kubwa ya ushawishi mbele ya Watanzania walio wengi.

Kutokana na Hilo vimeanza Kuibuka vikundi vya watu (japo nyuma vilikuwepo vichache) Ambavyo vinapinga Juhudi hizi za Makonda kiuwazi kwa Kutumia mwanya Mdogo Sana pale anapoteleza kama binadamu kwenye matamshi. Na Hawa ni wale wenye chuki na jamaa either kwa kutumika au kupandikiziwa chuki kutokana na historia "fikirishi" ya Makonda hapo nyuma au kutokana na "ukubwa" anaozidi kuujenga unaowatisha adui zake ambao wanajua kabisa baada ya miaka kadhaa hataweza kudhibitika.

Katika mahojiano yangu binafsi humu mtandaoni na Mitaani na watu kadha wa kadha unagundua wote hawana sababu za msingi za kumchukia Makonda zaidi ya UNAFIKI, UZANDIKI na WIVU, kwa kigezo eti ilisikika kwenye media kipindi Cha JPM kwamba alifanya mambo kadhaa mabaya kwa jamii, kitu ambacho hutukuwahi kupewa ushahidi. So utaona ni chuki binafsi zisizo na maana.

Wadau wanaBodi TWENDE na MAKONDA. Tumsapoti Makonda katika mazuri anayofanya, sababu anaisaidia Jamii. Kupitia yeye anaamsha na wakuu wengine wa mikoa waliolala na taasisi za Serikali. Tuwe wa kwanza kupongeza anapofanya vyema na WA mwisho kuhukumu anapofanya vibaya.

BRAVO, PAUL CHRISTIAN MAKONDA
 
Hizi nazo ni miongoni mwa mada za kipumbavu mno, nani alisema anamchukia Makonda? Watu wanazungumzia utendaji wake mbovu na sio yeye as an individual, jifunzeni kutofautisha haya mambo vijana. Vyeo vipo na vilikuepo na vitaendelea kuwepo hata baada ya yeyey na nyie, humble yourself
 
Try hide ur foolishness bro by clearing the so seems ambiguity to you. Never attack personality rather attack the topic, if fail then relax, read and take a way out.

Cheers!

Wewe ni Platinum Member na verified so tumia akili kidoogo uliyobakiza kuvukia barabara ili u'comment.
 
Kama wewe unaona kuongoza kwa matamko ndo kunafaa basi utakua na shida yakufikiri.Tunahitaji ufumbuzi wakudumu wa changamoto zilizopo sio kupiga porojo ambazo kesho akiwa hayuko tunarudi kule kule.
 
Kama wewe unaona kuongoza kwa matamko ndo kunafaa basi utakua na shida yakufikiri.Tunahitaji ufumbuzi wakudumu wa changamoto zilizopo sio kupiga porojo ambazo kesho akiwa hayuko tunarudi kule kule.
Toa ushauri wako kabla ya kukashifu... Mi nimeona yupo sawa kwa nafasi yake kama RC. Kama wewe unauwezo Mkubwa wa kufikiri labda utuambie majukumu ya RC ni yapi ambayo yeye hayatekelezi. Maana naona wewe ndio unaandika porojo bila kujua kama porojo..
ULITAKA AFANYE NINI???
 
Daah hii ndio mijizi anayopambanayo Makonda, Hii nchi inasafari ndefu sana
 
Try hide ur foolishness bro by clearing the so seems ambiguity to you. Never attack personality rather attack the topic, if fail then relax, read and take a way out.

Cheers!

Wewe ni Platinum Member na verified so tumia akili kidoogo uliyobakiza kuvukia barabara ili u'comment.
Being a Platinum member or Verified member got nothing to do with this level of stupity you are addressing here! Makonda hajui na hana ethics za uongozi, full stop
 
Kama wewe unaona kuongoza kwa matamko ndo kunafaa basi utakua na shida yakufikiri.Tunahitaji ufumbuzi wakudumu wa changamoto zilizopo sio kupiga porojo ambazo kesho akiwa hayuko tunarudi kule kule.
Dogo mjina huyu, wanajua uongozi ni kufoka, tunamuelewesha anajifanya mjuaji.
 
Kama wewe unaona kuongoza kwa matamko ndo kunafaa basi utakua na shida yakufikiri.Tunahitaji ufumbuzi wakudumu wa changamoto zilizopo sio kupiga porojo ambazo kesho akiwa hayuko tunarudi kule kule.
Anachofanya kiko sahihi wewe ndio hujielewi
 
Toa ushauri wako kabla ya kukashifu... Mi nimeona yupo sawa kwa nafasi yake kama RC. Kama wewe unauwezo Mkubwa wa kufikiri labda utuambie majukumu ya RC ni yapi ambayo yeye hayatekelezi. Maana naona wewe ndio unaandika porojo bila kujua kama porojo..
ULITAKA AFANYE NINI???
Wewe endelea kusifia.Kinachotakiwa kufanyika kinajulikana hakuna sababu yakukirudia kwasababu hakitakua na maana.Muda utatupa majibu sahihi.
 
Being a Platinum member or Verified member got nothing to do with this level of stupity you are addressing here! Makonda hajui na hana ethics za uongozi, full stop
Huna hoja bro (as u termed me dogo) huna na inawezekana hata hujui Nini maana ya hoja na ujibu vipi hoja. Kupinga hoja bila hoja is regarded as highly stupid mind... I guess Hujui hata umeandika Nini..
 
Dogo mjina huyu, wanajua uongozi ni kufoka, tunamuelewesha anajifanya mjuaji.
Kama ungepata nafasi ya kunijua ungebadili kauli yako hii... Na hata bila hivyo tukitumia tu kipimo Cha uandishi wa hapa Itabidi ujitathmini kama akili zako ziko sawa..
It's either uwe na discipline au urudi darasani. Kama sivyo ficha upuuzi wako kwa kupost as anonymous sio verified...
 
Wamrudishe ngazi ya kitaifa maana hata huko mkoani atafanya as if yuko taifani. Vibe atalitengeneza tu kujitofautisha na wakuu wengine wa mikoa wasio na impact kwa wananchi wanaowaongoza
 
Unadhalilisha watendaji wako mbele ya umma, umma unakushangilia sana.

Ukiondoka baada ya makofi tele umma unabaki na huduma zake duni kama huko nyuma.

Inahitajika mifumo ya kuhakikisha watoa huduma wote wanatimiza wajibu wao vema nyakati zote, bila kuhitaji kufokewa na viongozi wa juu. Hata hivi viongozi wa juu hawawezi kufika pembe zote za nchi kila siku.

Kiongozi atakayeweka mifumo ya kuhakikisha kwamba mfanyakazi yeyote wa serikali asiyewajibika kikamilifu anatemwa, bila kusubiri fokeo la kiongozi wa juu. huyu ndiye atastahili kupigiwa makofi ya umma.

Vinginevyo ni kutwanga maji kwenye kinu.
 
Back
Top Bottom