WanaBodi..
Kwa wale tunaofatilia siasa za nchi hii kwa ukaribu naamini tunamfatilia na Makonda katika hatua zake zote za uongozi.
Anachokifanya Makonda kwa Sasa toka amerudishwa kwenye ulingo wa uongozi Wa kisiasa ndio kile kile ambacho Watanzania waliowengi ambao ni Masikini waliokata tamaa na kuvunjika Moyo, wanataka kusikia. Na kumbuka hili ndio Kundi kubwa la Wananchi wa Tanzania. Katika muktadha huo utaona umaarufu wa Makonda unaongezeka Kila uchwao. Kwa maana njia anayopita ndio aliyopitia Hayati Magufuli ambapo mpaka Sasa asilimia kubwa ya wanyonge inamkumbuka. Makonda pamoja na kusaidia pakubwa kutatua changamoto za Wananchi katika nafasi anazopewa Ila pia anajijenga Sana kitaasisi (hafanyi makosa) kiasi kwamba ananguvu kubwa ya ushawishi mbele ya Watanzania walio wengi.
Kutokana na Hilo vimeanza Kuibuka vikundi vya watu (japo nyuma vilikuwepo vichache) Ambavyo vinapinga Juhudi hizi za Makonda kiuwazi kwa Kutumia mwanya Mdogo Sana pale anapoteleza kama binadamu kwenye matamshi. Na Hawa ni wale wenye chuki na jamaa either kwa kutumika au kupandikiziwa chuki kutokana na historia "fikirishi" ya Makonda hapo nyuma au kutokana na "ukubwa" anaozidi kuujenga unaowatisha adui zake ambao wanajua kabisa baada ya miaka kadhaa hataweza kudhibitika.
Katika mahojiano yangu binafsi humu mtandaoni na Mitaani na watu kadha wa kadha unagundua wote hawana sababu za msingi za kumchukia Makonda zaidi ya UNAFIKI, UZANDIKI na WIVU, kwa kigezo eti ilisikika kwenye media kipindi Cha JPM kwamba alifanya mambo kadhaa mabaya kwa jamii, kitu ambacho hutukuwahi kupewa ushahidi. So utaona ni chuki binafsi zisizo na maana.
Wadau wanaBodi TWENDE na MAKONDA. Tumsapoti Makonda katika mazuri anayofanya, sababu anaisaidia Jamii. Kupitia yeye anaamsha na wakuu wengine wa mikoa waliolala na taasisi za Serikali. Tuwe wa kwanza kupongeza anapofanya vyema na WA mwisho kuhukumu anapofanya vibaya.
BRAVO, PAUL CHRISTIAN MAKONDA