Tunajua na wewe unajua kuwa hupendi wabunge wa upinzani na pengine hata ungesikia wamefutika kwako chozi lisinge toka.
Lakini pamoja na hayo, heshima ya mbunge wa Chadema au ACT ndio heshima ya bunge zima kama ilivyo katika mabunge yote ya Commonwealth countries.
Tamko hili la Makonda sio tuu limefedhehesha mamlaka ya mhimili wa Bunge tuu bali taifa zima la Tanzania.
Iko wapi sheria isemayo mheshimiwa Mbunge ambaye hajaingia bungeni akamatwe kuwa ni mzururaji? Kama ingekuwepo iweje wewe kama Spika wa muda mrefu tokea unaibu ulikuwa hujaona hilo mpaka aje alione RC ngumbaru aliyefoji vyeti vya elimu?
Jiulize tutasemwa mangapi na vyombo vya habari vya mataifa yenye ustaarabu kama kauli hiyo hutaipinga? Achana na utekelezaji, maana huko anaweza kusababisha mengine ikiwamo hata vurugu za kuangusha nchi.
Jee ni kweli muhimili wako unachezewa na kuwekewa sheria na mkuu wa mkoa? Na kama ni maagizo ya kitaifa kwa nini iwe Dar tuu na sio mikoa yote?
Mheshimiwa Ndugai acha kuruhusu jina lako kuingia katika orodha ya maspika wa hovyo kupata kutokea sio TZ tuu bali Afrika.
Sent using
Jamii Forums mobile app