RC Makonda: Idadi ya maambukizi imepungua Dar, kuna watu walinunua majeneza na kupiga picha ili kuzua taharuki

RC Makonda: Idadi ya maambukizi imepungua Dar, kuna watu walinunua majeneza na kupiga picha ili kuzua taharuki

Huyu kiongozi ni "ZERO ZERO ZERO KICHWANI" kabisaaa. Yani kichwa chake kimejaa "MATOPE". Akili zake hua anakua amezikalia. Yani ni punguwani kabisa hili jamaa.

Haya maradhi sio yakufanyia mzaha, ni hatari sana, yapaswa tuyachukulie "SERIOUS" sanaa.

Imefikia hatua nchi zote za jirani zinatuona kama mkaa wa moto. Tanzania tumekua kama vile "WAZALISHAJI/BREEDERS/INCUBATOR" ya COVID-19.
Umeongea kwa hisia sana mkuu mpaka umenigusa
 
upo sahihi mkuu!. ila pia hali sio shwari kwa takwimu ipi pia!? nauliza tu kuondoa ujinga nna imani utanijibu kwa weledi bila hisia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata tukisimamia takwimu zao za mwisho za wagonjwa 480 bado sio shwari,lakini tukiachana na hio tutumie tu zile za madereva wanaokutwa na Corona mipakani mwa nchi jirani,kwa siku za Jana pekee madereva 23,Namanga hapo tukirudi nyuma kidogo kuna madereva 9 walikutwa na covid mpakani na Uganda,halafu Uamuzi wa Rwanda kwamba kila dereva alietoka Tanzania hataingia nchi hiyo bali atamkabidhi dereva wa Rwanda,bila kusahau Uamuzi wa Uganda kwamba Dereva kutoka tz kwanza atakuwa pekeyake na hatatakiwa kulala popote ndani ya Uganda,Halafu tumalizie na Uamuzi wa Zambia kufunga mpaka wake,
Hapo Ushwari upo wapi?hao wanatoka nchini hususani Dar wanaenda kukutwa na Ugonjwa nchi za watu.

Halafu angalia na tahadhari hizi zinazotolewa na balozi zilizopo hapa Tanzania(Dar)kuhusu ugonjwa
tapatalk_1589435077581.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii Ni kweli na nimbinu zinazoratibiwa na upinzani apa nchini,lengo ni kumkomoa kingizi wa nchi na KUZUSHA hofu kwa raia . UPINZANI NCHI HII WANATUMIKA NA MABEBERU TUWE NAO MAKINI KWANI WANANIA OVU KWA NCHI JUU YA MASLAI YAO BINAFSI

CCM DAMUDAMU!!!,CHAMA CHA MAMA &BABA
 
Mimi Mpumbavu Mimi

Wacha nikae kimya na Upumbavu wangu.

Hivi, lile gari la Huduma ya Maziko la Halmashauri lilivyokuwa likipita usiku wa saa 7 kwenda Kondo kumbe walikuwa wanakwenda kushoot!

Hakika mimi ni Mpumbavu.
 
Majeneza yananunuliwa mtandaoni? Yale Yale ya Yule baba yake kuwa amefanya utafiti kakuta mapapai yana corona, hivi hawa watu shule walienda kweli?

Au kuna dhambi wamefanya inawatafuna? Maaana ujue mtu alietenda dhambi kubwa unamkuta anajiongelesha vitu vya kitoto kabisa na yeye anajisikia raha kuona yuko sawa

Sent using Jamii Forums mobile app
Damu za watu zinawatafuna
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Ndugu Paul Makonda amenena yake kuhusu hali ya Corona mkoani Dar es Salaam. Akizungumza na vyombo vya habari amesema hali sasa inaelekea kuwa shwari, idadi ya wagonjwa inazidi kupungua na kuwatoa hofu wakazi wa mkoa huo.

Vile vile amesema alifanya uchunguzi na kugundua watu wenye nia ovu mtandaoni walinunua majeneza na kwenda kwenye maeneo ya makaburini na kuchimba chimba na kujifanya wanazika ili kuleta taharuki.
Idadi imepungua namna gani? kutoka wangapi hadi wangapi? Wewe huna kipimo, unatoaje taarifa kama hiyo!
Kauli kama hizi zinatuchanganya - tufuate ya RC au ya Rais wetu mpendwa?
Je ile picha iliyopigwa wakionekana ndugu wakiwa makaburini na majeneza mengine pembeni, tuseme hao ndio walikuwa wamenunua ya ziada na kwenda kupiga nayo picha makaburini?

Mambo kama haya hayampendezi Mungu, na tukiendelea hivi hatatusikiliza, Tutasali sana, tutafunga sana, tutavaa magunia, lakini kwa kuwa maombi na sala zetu hazitoki ndani ya roho zetu - Mungu aonaye sirini hatatusikiliza maana yote yanakuwa ni unafiki tu.
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Ndugu Paul Makonda amenena yake kuhusu hali ya Corona mkoani Dar es Salaam. Akizungumza na vyombo vya habari amesema hali sasa inaelekea kuwa shwari, idadi ya wagonjwa inazidi kupungua na kuwatoa hofu wakazi wa mkoa huo.

Vile vile amesema alifanya uchunguzi na kugundua watu wenye nia ovu mtandaoni walinunua majeneza na kwenda kwenye maeneo ya makaburini na kuchimba chimba na kujifanya wanazika ili kuleta taharuki.

alipata wapi takwimu
 
Bongo bwana!
Yaani na wasomi wote,wataalamu wote,
Tumeamua kukabidhi nchi kwa hawa vilaza wawili,huyu wa dar na mwenzie aliyejificha kwao,
Nchi zingine zenye watu wenye akili,hawa wote ilibidi wale shaba tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata mimi nimeshangaa sana, wachimbe makaburi, wanunue majeneza, wanunue PPE, wakodi na Ambulance kwa ajili ya kwenda kufanya "shooting", Duu!
We jiulize,kama wasiojurikana waliweza kuiba rekodi na makabrasha ya migodini ya makinikia,hao walionunua majeneza,wakachimba makaburi,wakapiga picha,mbona hawajakamatwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani DAB ni msemaji wa Corona kimbele mbele kitamponza huyu nae
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ametutangazia kuwa maambukizi ya Korona mkoa wa Dar es Salaam yamepungua, hii ni habari njema pamoja na kutotoka kwenye chanzo rasmi kama serikali ilivyoagiza.

Habari si njema kwa watengeza barakoa na sanitaiza kwani mauzo yatapungua kutokana na wengi kutoona umuhimu wa vitu hivyo, asante Mungu.
 
Kwa ushahidi upi wa kuthibitisha coronavirus imepungua Dar?
 
Yamepungua kutoka watu wangapi?
Wamejuaje yamepungua?
 
Kama maambukizi yamepungua, basi JIWE asingekimbia hata vikao vya EAC (Japo vilifanyika kutumia VIDEO CONFERENCE, ila jamaa akaogopa asiambukizwe Covid-19).

Jamaa ni muoga balaa, ila kwa kupiga porojo na kuongea ni bingwa.
 
Back
Top Bottom