Gazeti la Mwananchi online limeripoti maneno aliyoyatoa Makonda alipokuwa anatembelea sehemu za Ilala kukagua miradi. Kilichonishangaza ni kuwa huyu mkuu wa mkoa anavyotoa maneno ya kuropoka bila kuwa na scientific evidence.
Kila mara anatuambia Dar Es Salaam ipo salama wakati watu wanaugua na mmoja amefariki...Kuna habari ambazo zinaonekana kuwa za kweli kuhusu kufichwa kwa idadi ya wagonjwa waliopo sasa, Kuna idadi kubwa kuliko hiyo iliyotangazwa na huyo waziri.
Nchi hii hasa awamu hii inaficha habari nyingi sana ndiyo maana tumepata ban ya kufanya application ya D-visa lottery (Inaonekana bado hao viongozi uchwara hawajakoma).
Magufuli amekwenda Chato, hatujaambiwa kama amesharudi Dar (Kuna watu walio kwenye payroll ya CCM watauliza inanihusu/Inatuhusu nini kutaka kujua wapi alipo rais?) Sisi kama walipa kodi tunaolipa mshahara wa rais tunapaswa kujua rais yupo wapi na anafanya nini huko Chato badala ya kuwa Magogoni akishughulia matatizo ya watanzania!
Au atuambie kama amemwachia ofisi Makonda? Maana anazungumza Makonda mambo ya CORONA na hakuna anayemuuliza.
Haya yanayofichwa fichwa yataleta matatizo, Dunia nzima kuna tatizo....Mbona wengine hawafichi? Tunayo figures za nchi zetu na ongezeko la maambukizi linavyokwenda ni kitu cha wazi....Linafahamika.
Kuficha ficha itaigharimu nchi hii, wakati kwingine kumeisha mlipuko huku kwetu kutakuwa ndiyo kumeanza.
VIONGOZI KUWENI WAKWELI