Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
NANI? Bashite? Huyo ni chui waliemlea wenyewe. Hao wote pamoja na mkubwa wao anaelalalala kwenye mawe, sasa wanamwogopa.Wakati wa vita kuna kitu kinaitwa commanding post ambapo mashambuliz na mipango yote hufanyika.
Corona ni vita,commanding post imeshatangazwa.Ni wajibu wetu wote tufuate maagizo toka commanding post.
Tuombe Mungu,sijui itakuwaje tukifikiwa na hali kama ya Italy,Allah aepushie mbali!!
RC Makonda: Watu wanafunga maduka, wanajifungia majumbani kisa Corona, mtakufa na njaa - JamiiForumsWewe ni mgonjwa wa ajili,Tanzania ina Marc 30+ sasa sijui mh Samoa na majaliwa waanze kupiga ramli kumbaini ni RC yupi una chuki naye,wewe boya kweli
Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee!Bashite haguswi wewe mzee, kaa kimya tu
Tanzania wananchi wanajifungia ndani lakin Serikal inawahamasisha watoke Nje wafanye kazi
Kwingineko Duniani Wananchi wanataka kutoka nje kuchapa kazi Serikal zao zinawazuia kwa hofu ya Corona
Maana yake Wananchi wa TZ ni waoga na wavivu wakati Serikal yao ni ya kijasiri na kichapa kazi
Kwingineko Serikal zao za kivivu na kioga wakati wanancho wao ni wachapakazi na majasiri
Sent using Jamii Forums mobile app
"Tokeni kafanyeni kazi eti Watu wanafunga maduka, wanajifungia majumbani kisa Corona, mtakufa na njaa, ndio maana leo nawafuatilia wakandarasi, sasa nimkute mkandaraai hayupo site kisa corona, kuna wapuuzi huko wanasema Serikali inadanganya idadi imeongezeka, kwenu kuna Mtu amekufa na corona?, kuna Mtu kwenu anaumwa corona?, hiyo idadi imetoka wapi?" - Paul Makonda, RC DSM
Good work our focused leader
======
Wananchi wanaingia hasara kwa kukwepa majukumu yao huku mambo yakienda tofauti wanaanza kuilalamikia serikali ili iweze kupatia msaada.
Amesema hayo leo mkuu wa mkoa wa Dar es Salaaam Mh Paul Makonda wakati akikagua mradi wa TARURA katika eneo la Kinondoni shamba ambapo kumekuwa na mgogoro baina ya TARURA na wananchi wa eneo hilo.
Pia amewataka wananchi kuacha kujifanya wajuaji wakati tatizo linapokuwa kubwa kwasababu wakati watu wanaingia katika eneo la mradi ambalo hawatakiwi kuvamia.
Vilevile amewataka wananchi kufanya kazi huku wakichukua tahadhari ya ugonjwa wa Corona wasikae ndani watafute hela ili wasije wakafa na njaa.
“Tokeni ndani mkafanye kazi Corona isiwe kigezo cha kujifungia ndani tumepambana na magonjwa mengi ikiwemo kipindupindu na magonjwa mengine tufanye kazi huku tukichukua tahadhari’amesema Makonda.
Aidha Makonda amekukagua miradi ya barabara inayotekelezwa na TARURA katika wilaya ya Ilala na Kinondoni kujua maendeleo ya miradi hiyo.
“Barabara ni ahadi ya muda mrefu ya Mh Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli ijengwe kutoka makao makuu wa Bakwata hadi Biafra”amesema Makonda.
Hatahivyo amepokea taarifa ya mgogoro kutoka kwa wananchi wa eneo lile kwa kutaka kuvunjiwa nyumba zao bila kupata fidia na walio lipwa wapo na hawajipotiwa na barabara hiyo.
Aidha amewataka wananchi kuwa atatuma kamati yake ifanye ukaguzi na wataanza jumatatu ili walete majibu kamili ili mradi huo uende kwa haraka.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu wa mkoa wa Dar Makonda amewashangaa wananchi kujifungia ndani kisa Corona.
Makonda amesema watu watoke wakafanye kazi taratibu za kujikinga na corona ziko wazi, hivyo kujifungia ndani kisa Corona ni uzembe.
Amewashangaa wafanyabiara kufunga maduka kisa Corona.
Pia ameonya wanaosambaza habari kuwa kuna wagonjwa wengi ila wanafichwa, amehoji kwenye familia yako kuna mtu anaumwa corona ama amekufa na corona serikali imeficha.
NB. Kwa hizi kauli za viongozi ikitokea Corona ikatupiga sawasawa sidhani kama kuna Taifa litatia mguu kutusaidia.
Hata kama serikali ina msimamo wake kuhusu hili wangefanya kimya kimya, kutangaza hadharani hivi ni hatari kwa mstakabali wa Taifa letu.
Bwashee kodi isipolipwa mishahara na marupurupu ya watumishi wa umma utalipa wewe?!
Kama hukubaliani na data za serikali basi tuletee ushahidi!
Hii ni komenti yangu bora ya mwezi!Tanzania wananchi wanajifungia ndani lakin Serikal inawahamasisha watoke Nje wafanye kazi
Kwingineko Duniani Wananchi wanataka kutoka nje kuchapa kazi Serikal zao zinawazuia kwa hofu ya Corona
Maana yake Wananchi wa TZ ni waoga na wavivu wakati Serikal yao ni ya kijasiri na kichapa kazi
Kwingineko Serikal zao za kivivu na kioga wakati wanancho wao ni wachapakazi na majasiri
Sent using Jamii Forums mobile app
Hizi kauli tata za viongozi muda wowote dunia inaweza kututenga!
Unawaonea gere walimu?Wafungue vyuo na shule kwa sababu walimu na wakufunzi hawafanyi kazi muda huu
Sent using Jamii Forums mobile app
Jitoe muhanga kusaidia wengine kama yule daktari wa China.Na ole wako uropoke eti nyumba fulani kuna mgonjwa wa Corona au amekufa kwa Corona kama utaona Makonda akikutetea mbele ya shtaka la kutoa taarifa za uchochezi.