RC Rose: Mkoa wa Chato utakuwa na wilaya 5 Kakonko, Biharamulo, Ngara, Bukombe na Chato yenyewe

RC Rose: Mkoa wa Chato utakuwa na wilaya 5 Kakonko, Biharamulo, Ngara, Bukombe na Chato yenyewe

Hivi bado Kuna wakuu wa mikoa ambao wana hamu sana ya kupigwa mti kimasihara?
Unawezaje kuja na hayo mapendekezo?
Hivi tunajua gharama za kuanzisha mkoa mpya na kuuendesha?

Kabla ya Chato kuwa mkoa, nadhani uindwe kwanza hii mikoa.
1. Butiama.
2. Kisarawe.
3. Lupaso.
4. Msoga.

Itifaki ni muhimu kuzingatiwa kwanza.
Shida yako ni unafiki na kujipendekeza.... Sasa chato ikitangulia kuwa mkoa unapungukiwa nini..? Na itifaki gani kama sio chuki tu zisizo na sababu....
 
Mkuu wa mkoa wa Geita mh Rose amesema ombi la kuunda mkoa wa Chato likipita basu mkoa wa Geita utabakiwa na wilaya za Busanda, Nyang'wale na Geita yenyewe na Mbogwe

RC Rose amesema mkoa mpya wa Chato utapokea wilaya 1 kutoka Kigoma na 2 kutoka Kagera.

Kwa maana hiyo mkoa mpya wa Chato unaopendekezwa utakuwa na wilaya 5 ambazo ni Kakonko kutoka Kigoma, Bihalamuro na Ngara kutoka Kagera na Bukombe na Chato yenyewe kutoka Geita.

Source: ITV habari!

Kazi Iendelee

Mikoa iliyokaa vibaya kijiografia ni Morogoro, Tabora, Pwani na Lindi, hiyo ndiyo ingepewa kipaumbele kugawanywa
 
mara ya mwisho kwenda chato ilikua 2018 palikua pamechangamka , pamejengeka watu wanapachukulia poa chato ila ni pazuri, lakini sidhani kama kua mkoa ni chaguo sahihi
 
Back
Top Bottom