Kahama ndiyo inastahili kuwa mkoa na siyo Chato. Hata hizo wilaya za Bukombe na Mbogwe zilimegwa kutoka wilaya ya Kahama. Sasa wameimega tena na kuanzisha wilaya za Ushetu na Ukune. Wilaya hizi zirudishwe kuifanya Kahama kuwa mkoa. Wanaweza kuimegea na wilaya za Ukene na Urambo. Kahama kimaendeleo na kiuchumi iko juu sana ukilinganisha na Chato. Mji tu wa Kahama ni zaidi ya Dodoma! Mzunguko wa fedha Kahama unazidi DSM. Shida ya watu wa Kahama ni wapole sana na hawajui kupiga kelele eg mbunge wao Kishimba yeye kila kitu poa tu. Hata kudai barabara ya kutoka Kahama hadi Urambo kupitia Ukune kujengwa kwa lami hajui wakati barabara hiyo ni ya muhimu sana ku tap utajiri wa eneo hili kwa manufaa ya taifa letu. Lina utajiri wa asali (nyuki), maziwa (ng'ombe), miwa (sukari), mahindi, mchele, mafuta (karanga), mahama, dhahabu na madini mbali mbali.