objectively, kuimega Chato kutoka Geita (ilikuwa Kagera kabla), Ngara-kutoka Kagera, Kakonko kutoka Kigoma, Bukombe na Biharamulo kuwa mkoa ni jambo jema. Kwa sasa wanaofaidi matunda ya mkoa Kagera ni Bukoba, Muleba na Karagwe. waiache Ngara iondoke tuu. mfano Ngara ilichangia sana kujenga miundo mbinu ya shule za Bukoba miaka ya nyuma....mda si mrefu wakaambiwa kila wilaya ijitegemee kwa kujenga miundombinu yake. Mpaka leo Ngara haija recover. ni miaka ya juzi tuu imeanza kupata shule zake. Ndo maana hata wana ngara waliopata elimu kupitia shule za bukoba ni wachache. Pia kutoka Ngara kwenda Bukoba ni mbali.
Chato utakuwa mkoa wenye coherence. Ngara na Kakonko lugha yao ni almost ile ile. Biharamulo na Chato zamani ilikuwa wilaya moja. imagine mtu kutoka Kakonko kwenda Kigoma kutafuta huduma. kwa raslimali walizonazo...utakuwa mkoa wenye potential sana. Ngara kuna madini ya kutosha...Chato uvuvi nk....Hata kikanisa..Ngara, Chato, baadhi ya sehemu za Kakonko, na Biharamulo ziko chini ya Jimbo moja la Rulenge-Ngara......(ingawa hili kiuhalisia halina uzito-maana imani za kidini na serikali ni tofauti)
Sema, kurahisisha maisha na huduma kwa wananchi....huu mkoa ungewekwa katikati pale Biharamulo. Ila hata makao makuu yakiwekwa Chato sioni shida...
Changamoto hapa ni kwamba wengi wanamchukia Hayati kwa hiyo hata swala la huu mkoa wanaliangalia kwa miwani ya mwendazake. ila kiukweli Chato na hizo wilaya tajwa.. unastahili kuwa mkoa.
Ingawa nashauri kuondoa au kupunguza hizi chuki dhidi ya mwendazake....tunaweza kuuita jina lingine ila isiwe Chato. Mf. mkoa wa Rubondo au mkoa wa Nyabugombe...au Burigi....nawaza tuu.
Ingawa nimalizie kwa kusema kwamba ingawa Hayati alikuwa anatokea Chato, Chato na hizo wilaya kuna watanzania wengine pia. Wathaminiwe na kuheshimiwa pia. sioni kwa nini mwananchi wa Ngara au Kakonko awe penalized kwa sababu tuu hizi wilaya ziko karibu na Chato.