Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Pia huko zenji waongeze mikoaHivi bado Kuna wakuu wa mikoa ambao wana hamu sana ya kupigwa mti kimasihara?
Unawezaje kuja na hayo mapendekezo?
Hivi tunajua gharama za kuanzisha mkoa mpya na kuuendesha?
Kabla ya Chato kuwa mkoa, nadhani uindwe kwanza hii mikoa.
1. Butiama.
2. Kisarawe.
3. Lupaso.
4. Msoga.
Itifaki ni muhimu kuzingatiwa kwanza.
Hii nchi ya hovyo sana kuongeza maeneo ya utawala kunatatua vipi tatizo kubwa kama la ajira?
Kwanini kipaumbele isiwe kujenga hospitari kama Muhimbili,Kagera,au Mtwara,au chuo kikuu kama UD au Udom?kwanini tunakimbilia kuigawa nchi kama vile Kuna tija yoyote,zaidi ya kuongeza gharama za uendeshaji,RC,RAS,RPC,?
Unaunda mkoa mpya kwa kumega ardhi toka mikoa mingine isiyotaka kumegwa!!!!
brilliant! I would support Nyakanazi au Burigi! Majina mazuri sana hayo. Na yapo Neutral!Watu wanachangia kwa mihemuko bila kuangalia uhalisia. Binafsi nakubaliana na hili pendekezo kwa sababu hizi
1. Itarahisisha watu wa biharamulo na ngara kupata huduma kuliko ilivyo sasa
2. Itarahisisha hizo wilaya kutoka Kigoma nazo kupata huduma karibu.
3. Itarahisisha utoaji wa huduma katika mkoa wa Kagera ambao idadi yake ya watu inazidi kuwa kubwa zaidi (ni mkoa wa tatu kwa idadi ya watu lkn bado mkubwa)
4. Kanda ya ziwa inashuhudia ongezeko kubwa la watu kuliko maeneo mengine ya Tanzania kwa hyo kumegwa ni jambo jema.
5. Wilaya zilizopo pendekezwa zina rasilimali nyingi lakini bado zipo chini kimaendeleo, hivyo zikisimamiwa kwa karibu zinaweza kuinuka
Vilevile nipendekeze mambo yafuatayo
1. Makao makuu yawe biharamulo au nyakanazi (kuna uzi humu ulishapendekeza mkoa wa nyakanazi), hii ni kwa sababu hapa ndo katikati.
2. Lakini ili kuondoa mashaka na wasiwasi kwa wapinzani wa Magufuli vilevile jina la mkoa lisiwe chato, naona Burigi litakuwa bora ili kuitangaza na hifadhi ya Burigi
Hujanipata sawia, alitaka Chato isichanganyike na wasio wasukuma. Kwake wasubi aliwaita wahaya; wanyambo pia aliwaita kuwa ni wahaya nao. Isipokuwa alipokuwa Katoke seminari alichangamana na wahangaza ambao kwake hawakuwa wahaya. Kwake ilimradi lugha yako inasikilizana na wahaya basi ni mhaya na tuseme ukweli hakuwapenda! Hivyo kitendo cha kuingiza biharamulo kuwa part ya chato inaua dhamira yake maana lugha yao inasabihiana na kihaya.Mbona wakiufanya mkoa watafanikiwa mno .
Mkoa kagera unaachiwa na wahaya Tu peke Yao.
Biharamulo na ngara hazikuwa wilaya za wahaya Bali wasubi, wasukuma na wahangaza
[emoji23][emoji23][emoji23]Hakuna kukata kabla ya konaHivi bado Kuna wakuu wa mikoa ambao wana hamu sana ya kupigwa mti kimasihara?
Unawezaje kuja na hayo mapendekezo?
Hivi tunajua gharama za kuanzisha mkoa mpya na kuuendesha?
Kabla ya Chato kuwa mkoa, nadhani uindwe kwanza hii mikoa.
1. Butiama.
2. Kisarawe.
3. Lupaso.
4. Msoga.
Itifaki ni muhimu kuzingatiwa kwanza.
Who else,JPM mwenyewe!Pendekeza hapa jina la mkuu wa mkoa wa chato.
Hakuna umbali huo kati ya Ngara na Bukoba. Ukipita Karagwe ni KM 270 na ukipita Biharamulo ni KM 300. Pili KM haziwezi kuwa sababu ya kugawa kwa sasa, dunia inaelekea kuwa ya kidijitali na umbali wa kimawasiliano unazidi kupungua siku hadi siku.Nadhani ishu wabongo wengi wanaangalia kugawanywa mikoa Kwa umbali Tu sio population density na population.
Mkoa wa Dar ni mdogo kigiographia lakin Una wilaya nchini hivyo hivyo Kwa Kilimanjaro.
Kagera ambayo imemegwa wilaya mbili kulingana na makadirio ya idadi ya watu ina population ya 3.2 million people na population density ya 120 per km nyuma ya mkoa wa Dar na mwanza tu yaan hata Kilimanjaro inaziwa na kagera Kwa population density na population na kijiografia ni makubwa na mrefu. Kutoka ngara Hadi bk ni 400 km .
So nashangaa watu wanasema sijui mikoa ya Lindi, tabora igawanye.
Just imagine mkoa wa Lindi Una watu million Tu na population density ya 12 people per km. Sawa ni mkubwa sasa wakianzisha mkoa watu watatoka wap.
Kabila kubwa pekee lisilokua na umoja wa kuunga kuunga na lenye wivu wa maendeleo ndani kwa ndani ila ni la wachapakazi kweli kweli.Makabila mseto mangapi ? Waha, wasukuma, wasubi, wahangaza na wasumbwa. Na wasukuma watabaki kabila kubwa katika mkoa huo tarajiwa maana Wilaya hizo karibu zote isipokuwa Ngara na Kakonko wasukuma ndio majority
Tunachukua Letoktok na taveta kutoka kenya..ovaaaHahahaaaa..... Na sisi tutaunda mkoa wa Rombo!
Biharamulo vichwa maji tia maji tia maji sana. Wakipewa makao makuu ya mkoa haifumi pale. Hawana ali ya maendeleo pale. Majungu ndiyo yao, ndio maana kamebaki vile vile toka enzi za mjerumani mpaka leo. Ki wilaya ka wajuaji wasiojua kama hawajui. I rest my case.Naona wako Sawa Tu. Sema tatizo mkoa umeitwa chato Bora ungeitwa biharamulo na makao makuu yakawa pale.
Mkoa wa kagera wamefanya poa kuugawa na watafanikiwa maana mkoa Una population kubwa na mrefu.kutoka ngara to bukoba ni km 400
Umewasahau kabila la waha, aka wanadiasporaMbona makabila yanafanana Tu.
Ngara wahangaza
Biharamulo wasubi na wasukuma
Chato wasukuma
Bukombe wasukuma.
Kagera imebakiwa na wahaya na wanyambo Tu na walitofautiana Sana kimaendeleo na kitamaduni na biharamulo na ngara
Kweli kabisa waituAsante mkuu. Hivi vitu ukiviangalia bila kujifunza historia yake utakwama. Biharamulo na Ngara wamenyanyasika sana uwepo wao Kagera. kiuhalisia sidhani kama Ngara na Biharamulo wamefaidika kwa lolote kuwepo Bukoba.
mnyonge mnyongeni...JPM hili alilijua siku nyingi na alijitahidi kupambana. Bila juhudi za JPM sidhani kama Ngara, Biharamulo na Chato zingetoboa siku za hivi karibuni. Bukoba ilimeza kila kitu!
Ungeniuliza mimi ningeshauri makao makuu yawekwe Biharamulo.
Uitwe mkoa wa Rubondo-neutral name. Mji wa kiutawala ubaki chato na kibiashara uwe biharamuroBiharamulo panaweza kuwa makao makuu ya mkoa lakini jina likabaki Chato!
Imeisha hiyo!Sasa mbona umeandika Heading kama tayari imeshapitishwa kumbe ni mapendekezo tu?
Sasa unataka umaskini usogezwe Biharamulo makao makuu badala ya kuuvutia pengine ukapunguzwe! Kumbuka pia Kakonko alikua wa kwanza kwa umaskini kwa hiyo kiujumla ni mkoa mpya wenye changamoto na inatakiwa wananchi wachangamke kuukwamua. Anzeni na kuchagua wawakilishi wenye akili za kuwakwamua wananchi na maeneo yao. Wabunge na madiwani, halafu mpewe viongozi wasimamizi wenye uthubutu. Hilo ni eneo potentials sana hasa katika kilimo na ufugaj.Na ni kweli bukoba,misenyi,muleba,karagwe na kyerwa zina maendeleo makubwa hasa ya vijijini na Hali ya maisha kiujumla tofauti na biharamulo na ngara.
Imagine Biharamulo ilikuwa wilaya ya pili Kwa umaskini nchini.
Pia wahaya wameachiwa mkoa wao sasa maana walitofautiana mno na biharamulo na ngara .
Mkoa usiitwe chato mkoa uitwe biharamulo na makao makuu yawe biharamulo.
Watu wasichangie kisiasa maana hata kuumega mkoa wa kagera ni Sawa Sana maana mkoa Una population density na population kubwa pia zaidi million 3 na density ya 120 per km.
Wanaoagalia umbali Tu ili ianzishwe mikoa ya kutoka tabora na Lindi wanakosea maana mikoa hiyo ina population ndogo na density pia
Endapo hitaji lipo Basi Biharamlo ama Nyakanazi panaweza kuwa Kati . Ngara Hadi Chato ni km 257;Kakonko Hadi Chato km 193;Bukombe Hadi Chato km 137;Biharamlo Hadi Chato km 123; Endapo kigezo ni kuabudu mzimu Basi sawa Ila Kama ni jiografia na kusogeza huduma kwa wananchi kuifanya Chato makao makuu huo mkoa mpya ni uendawazimu, udikiteta,ushamba,ulimbukeni....Lakini kwa upande wangu naona ni poa kabisa. Hizi wilaya japo juu ziko mbali sana na makao makuu ya mikoa iliyo. Mfano Ngara to Bukoba ni mbali kuliko Ngara to chato. Kwa upande wangu naona imetulia tu.