RC Rose: Mkoa wa Chato utakuwa na wilaya 5 Kakonko, Biharamulo, Ngara, Bukombe na Chato yenyewe

Sawa Mkuu, ila ukitazama kwenye ramani hata hivyo mtu wa kutoka Bukombe ni kama Chato kwake ni mbali zaidi kuliko Geita
Bukombe watakuwa mbali na Makao Makui ya Mkoa
 
Kaka una akili sana
 
Uitwe mkoa wa Rubondo-neutral name. Mji wa kiutawala ubaki chato na kibiashara uwe biharamuro
Hivi unafahamu kwamba kisiwa cha Rubondo kiko Tarafa ya Bugando Wilaya ya Geita ? Sasa utasemaje mkoa mpya uitwe Rubondo ?
 
Butiama ishapewa Wilaya
Kisarawe halijawahi kutoa Rais
Lupaso inakwenda kuwa Wilaya
Chalinze inapewa Wilaya
Chato wacha wajisikie kidogo, maana yeye kafia Madarakani

Sent from my vivo 1915 using JamiiForums mobile app
 
Solution ni nchi kuwa digitized na kuboresha transport system kama treni za umeme, ndege nk kwa bei ya chini hata barabara pia zipitike mikeka, subways system hiyo hata makao makuu yawe namtumbo mtu wa ngara atateleza tu.

Naota lakini ila nimeyaona kwa macho nina imani tutafika.
 
Kwa nini walazimishe hivyo mkoa wa Chato kuzaliwa ? Kwa nini uende ukapore Wilaya 3 za mikoa mingine Ili tu kutimiza adhma ya Mwendazake?
Tunamuenzi shujaa wetu ambaye alikuwa na hiyo ndoto kwa kuwa katufanyia mambo makubwa sana ikiwemo ujenzi wa miundombinu na kufufua mashirika mbalimbali kama ATCL, ujenzi wa SGR, Bwawa la Nyerere, kufufua TAFIRI shirika la uvuvi,ujenzi daraja la Sarenda, WAMI, ujenzi wa vituo vya afya nchi nzima, ujenzi wa shule nchi nzima, flyover mfugale na kijazi, stend mpya mbezi Luis na zingine nchi nzima ikiwemo ya dodoma, maji kutoka ziwa Victoria kuja Dodoma na miradi mingine mingi ambayo naweza kukesha kuorodhesha sasa kuna shida gani tukaipa heshima CHATO alipozaliwa na kukulia huyo shujaa wa Afrika.
 
[emoji3][emoji3]hayo uliyotaja kweli ndoto mkuu!! Maana hata maji tu yameshindikana.
 

Na ikiwa mtu wa Ngara ana kesi Dodoma inakuwaje?
Basi ni vyema tujiulize kama mfumo wetu wa utawala kiserikali uko sawa. Hii dhana ya kuanzisha mikoa kwa lengo la β€œkusogeza” huduma au maendeleo kwa wananchi haina mantiki katika zama hizi. Ni kutaka kuongeza wigo wa ukiritimba na ulaji kwa wateule wa wanasiasa.
Tunahangaika kutanua serikali kuu mikoani huku tukidhoofisha serikali za mitaa ambazo ndizo zingekuwa zikiongoza utoaji huduma na kuchochea maendeleo ya maeneo yao kama ilivyo kwenye nchi zilizoendelea.
 
Alizaliwa Katoma wilaya ya Geita akakulia Chato.
 
Hahaha mpaka raha yaani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…