RC Said Mtanda: Mkandarasi anayejenga Soko la Kirumba - CHINA RAILWAY GROUP ameanza kuingiza malipo ya NSSF ya Watumishi wake

RC Said Mtanda: Mkandarasi anayejenga Soko la Kirumba - CHINA RAILWAY GROUP ameanza kuingiza malipo ya NSSF ya Watumishi wake

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda amefafanua hoja iliyotolewa na Mdau wa JamiiForums aliyelezea kuwa Mkandarasi raia wa China anayejenga soko hilo hawasilishi michango ya Wafanyakazi wake katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).
WhatsApp Image 2026-06-11 at 23.03.33 (1).jpeg
GaAKi0oWYAIZlb6 (1).jpg

Mtaka amesema “Ukweli ni kuwa kampuni hii tangu kusajiliwa na mfuko mwezi Aprili 2025 hadi sasa imechangia kwenye mfuko Tsh. 93,801,200 huku wakiwa wanadaiwa Tsh. 78,271,800.00 kuanzia Novemba hadi Aprili 2026.

“Tarehe 8.4.2026 kuliundwa kamati ya kufuatilia madeni ya serikali ikihusisha vyombo kadhaa kama vile TAKUKURU, DPP na DCI chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na waajiri wote katika Mkoa wa Mwanza ambao wana madeni walitafutwa wakiwemo Wachina hawa mwisho wao makubaliano ya kumaliza madeni hayo yalifanyika.
GaAKi0hWcAAlEgD (1).jpg

“Kwa wafanyakazi wote walioachishwa kazi michango yao iliamriwa kulipwa kabla ya tarere 17.6.2026 na kufikia jana 16.6.2026 fedha kiasi cha milioni 8,662,800 kimelipwa.

“Tutaendelea kutumia plattform hii kupata taarifa na kuzifanyia kazi.

“Thank you for your attention to this matter.

Pia soma
~
Tunaojenga Soko Kirumba - Mwanza tunakatwa fedha lakini hazipelekwi NSSF
~ RC Mtanda aagiza NSSF kufuatilia madai ya michango ya wafanyakazi wanaojenga Soko la Kirumba kutowasilishwa kwao
 
Back
Top Bottom