Real Madrid (β€ŽLos Blancos) | Special Thread

Tunashindwa kutumia hizi nafasi za hawa jamaa kufungwa, Atletico ndio ninaona wapo serious.

Ligi imekuwa ngumu msimu timu nyingi zina vijana wazuri. Unajua wachezaji wengi sasa hivi wanakuja kucheza la liga! Wanatukamia kila game mpaka tunaonekana wa kawaida, lakini mechi bado nyingi sana huko mbele tutakaa vizuri tu
 
Umepigwa kidude dakika ya 4' mpaka sasa ni ya 35' bado huna hata shot on target
Niliiwahi game, nikawa naangalia huku najiuliza, kwa huu uchezaji tuliwezaje kumkanda mtani goli nne na Bayern? Nafasi zinatengenezwa kama mia, ila hakuna anaetaka kufunga.

Huu msimu Atletico akiwa na consistency, anaweza chukua ndoo.
 
Tupo dimbani vs Valencia. Papa Perez alitoa msaada wa takribani bilioni tatu za kibongo kwa wa Valencia baada ya janga la DANA.

Mashabiki wa Valencia wamempokea Perez na Madrid kwa vigelegele leo. Tunasubiri uwanjani, watatulia au wataleta ya last season, ubaguzi.
 
Kwahiyo unasubiri mbeleko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…