nimeingia jf nikawakuta mwaka 2011,hiyo ni wazi kuwa kama hukuuza hii account we ni mtu ambae umri umesonga sana,about 80 years old,lakini mara nyingi unakuaga mtu wa kupost vitu vyenye chuki,kiasi kuwa huwa najiuliza,au Nyerere alikunyimaga cheo ikabidi ukimbukie US kuganga maisha na bado una kinyongo na serikali ya ccm😂😂,kiufupi sikumbuki lini umewahi kunishinda kwa hoja,hakuna mtu anaweza kunishinda kwa hoja humu,na hata kwamatusi endapo nikiamua kuchafukwa
Wewe ni mtu mjinga tu.
Hata unavyoanza kuandika hapa unajionesha ni mtu mjinga tu.
Hiyo 80 years old hata baba yangu hajatimiza.
Nyerere hakuninyima cheo nilikuwa mdogo sana enzi zake, Nyerere kaondoka urais hata shule ya msingi sijamaliza. Ila Nyerere alikuwa anafanya kazi na Mama yangu Ikulu. Nimeanza kutembea corridors za Ikulu Tanzania kabla sijazaliwa. Ikulu ya Nyerere kulikuwa na Uncles zangu wawili walikuwa kwenye prominent positions, familia yangu ilikuwa inakaa nyumba ya Ikulu Upanga, kwa hiyo kama unaangalia mambo kibongobongo hivyo, sina sababu ya kumchukia Nyerere. Nyerere ni mtu ambaye, kwa rationale yako, sina sababu ya kumchukia, na nina kila sababu ya kumpenda.
Watu wangapi hapa wanaweza kusema wamekaa nyumba ya Ikulu Upanga enzi za Nyerere? Watu wangapi hapa wanaweza kusema wamekaa Oysterbay kuanzia enzi za Nyerere?
Sina sababu ya kumchukia Nyerere kama unavyosema. Tena, kwa rationale zenu za kuchumia tumbo, nina kila sababu ya kuwa muimba pambio wa Nyerere.
Serikali ya CCM, katika sababu hizo personal, sina sababu ya kuwa na kinyongo nayo. Familia yangu imenufaika na ujinga wenu. We have a multimillion dollar crib in Oysterbay kwa sababu ya ujinga wa serikali ya CCM. Mwaka jana kuna mtu katupa a starting offer ya $3 million, US dollars, tumekataa kuuza kwa sababu hatuna shida hivyo.
Sasa kama unaangalia manufaa binafsi hapo, kwa nini niichukie serikali ya CCM? Mimi nilitakiwa kuwa muimba pambio wa CCM.
Ninapinga mambo kifalsafa, si kwa sababu ya chuki au umasikini.
Ningekuwa naangalia habari za chuki na umasikini, mimi ni mtoto wa mfumo niliyeanza kutembea corridors za Ikulu tangu niko tumboni mwa mama yangu, nimekula ma apples ya Miss Wicken.
Unamjua Miss Wicken?
Jadili hoja, usimfanye Kiranga kuwa hoja.
Unasema hakuna mtu anayeweza kukushinda kwa hoja, labda ni kwa sababu hujadili hoja.
Sasa mtu atakushindaje kwa hoja wakati unamjadili Kiranga personally, kwa ujinga usio na hoja wa wa "ana chuki", badala ya kujadili hoja iliyopo hapa, ya viongozi wa Tanzania na meritocracy?
Unafahamu hata "meritocracy" maana yake ni nini?
Unafahamu hii ndiyo hoja hapa, si Kiranga?
Hujadili hoja, sasa mtu atakushinda vipi kwenye ligi ambayo hata huchezi?
Jadili hoja, usimjadili Kiranga.
Kiranga si waziri katika serikali ya Tanzania.