Nyanda za juu Kusini, ukiacha miji, ipo juu sana kuliko vijiji vya kanda ya ziwa kwa ubora wa maisha na maendeleo.
Usukumani wanafuga, lakini quality ya mifugo ni duni sana ukilinganisha na mifugo inayofugwa nyanda za juu. Kanda ya ziwa wanalima, lakini ni vishamba vidogo, na hawajui ukulima wa kisasa. Lakini pia kanda ya ziwa wanazaana sana, na familia nyingi ni duni. Sorry to say this - ukimpata mwanakijiji wa kanda ya ziwa ambaye hajasoma kabisa, na wa namna hiyo hiyo wa Nyanda za juu kusini, uelewa wao katika mambo mengi, ni mbingu na nchi. Kanda ya ziwa, mpaka leo hii, wapo watu ambao hawajui hata kusalimia tu, kwa Kiswahili.
Kuna wakati nilikuwa nakagua baadhi ya maeneo, wilayani Bukombe, tulikuwa tunatumia chopa, tukatua kijiji kimoja karibu sana na hifadhi ya Kigosi, kwenye programu hiyo ya siku 2 ilihusisha kuchukua sampuli, tukawachukua vibarua wa hapo kijijini, na wengine toka Ushirombo. Jioni baada ya kazi, walikuwa wakiongea mambo ya kawaida. Kukawa na mjadala wa kidini, kijana mmoja wa kisukuma, baada ya kusikiliza kwa muda mrefu, aliuliza, "huyo Yesu ina maana ni mkubwa kuliko Mwanamalunde?". Nilisoma habari za Mwanamalunde nikiwa shule ya msingi, nilicheka na kutafakari sana. Yule kijana, karne hii, hajui habari ya ukristo, wala uislam. Kwa kumjaribu tu, nilimwuliza kama anamjua Rais wa Tanzania (wakati ule alikuwa Kikwete), alinijibu, 'Unyerere".
Kanda ya ziwa, suala la elimu, hasa maeneo ya vijijini, achilia mbali elimu ya darasani, hata ile elimu tu ya mazingira wanayoyaishi, bado sana. Yapo maeneo, mpaka leo hii, mtu anajisikia ufahari kumiliki fisi wa kishirikina.
Umaskini wa Tanzania ni reflection ya kiwango cha elimu cha watu wa eneo husika.