Regional Per Capita GDP: Hii ndio Mikoa 7 ambayo Wananchi wake wana kipato cha Uchumi wa kati Tanzania Bara

Sasa wewe ni mjinga , Takwimu hizi ni za PPP na Takwimu nilizoleta ni za chapisho rasmi kutoka NBS sio kipeperushi kama hiki hapa,na zime base kwenye per capita at Current Market Prices by 2019

Afu inashangaza hao IMF kuleta figures kwa PPP kwa sababu Tzn hatutumii sarafu tofauti kwamba ufanye kuconvert kwa kutumia index ya PPP , na bidhaa ni zilezile na hata prices ni ndogo Nyanda za Juu Kusini kuliko huko Kanda ya ziwa ko niliyegemea purchasing power parity iwe kubwa Kusini kuliko Kaskazini.
 
Tofautisha kuwa na rasilimali na kuwa na utajiri. Rasilimali zinaweza kukuletea utajiri if and only if zinatumika katika namna inayoleta tija kiuchumi.

Mfano mzuri ni Tanzania yetu ambayo ni miongoni mwa nchi zilizobarikiwa utajiri wa rasilimali lakini kwa kuwa 'maboga' yanatawala, nchi imebaki kuwa ombaomba huku wananchi wake wakiishi under extreme poverty for years.
Swala sio watawala ni tu watanzania wengi vichwa vibovu kikiwemo chako

Japan haina raslimali yeyote na ni tajiri hasa sababu private sekta watu wana akili sana

Fikiria familia moja ya TOYOTA inajaza magari Tanzania nzima kila uendapo unakutana na TOYOTA

Wewe na familia yako cha maana mlichogundua na kuzalisha ni nini?
 
Uongo mbona bakheresa ni bilionea namba Moja Afrika Mashariki kwa kuuza juice na vyakula
Dah!! We kiumbe unahitaji maombi aisee, sio kwa reasoning hiyo uliyo nayo.

Kwani huyo Bakhresa utajiri wake kaupatia Mwanza pekee? Fine, Bakhresa ni tajiri kwa kuuza juice na vyakula, kwa hiyo na kila anayenunua juice na chakula naye anatajirika kama Bakhresa?! Kati ya mnunuzi na muuzaji ni nani anatengeneza 'utajiri' in the process?
 
Habari zenu wadau!

Mwaka 2020 tulitangaziwa Tanzania kusajiliwa kuwa miongoni mwa nchi ambazo wananchi wake wamefikia kiwango cha Uchumi wa Kati wa chini yaani Lower Middle Income Country.

Hesabu hiyo huwa inazingatia GNI per Capita Income ambayo ina range Kati ya $1'036-$4,045 ,,ambapo kwa Tanzania hapa ni mikoa michache Sana ambayo wananchi wake ndio wako Uchumi wa Kati,yaani wenye kipato kuanzia milioni 3 kwenda juu.

Ifuatayo ni orodha ya mikoa 7 ambayo wananchi wake Wana mapato yaliyofikia hicho kigezo cha Uchumi wa Kati, pato la kila mwananchi kwenye mkoa husika limeanishwa.

Regional Per Capita GDP at Current Market Prices,Tanzania Mainland, financial year 2019.Figures in Million TZS

1. Dar es Salaam (4,529,876)

2. Iringa (3,868,283)

3. Mbeya (3,675,999)

4. Kilimanjaro (3,302,915)

5. Ruvuma (3,288,252)

6. Arusha (3,198,260)

7. Njombe (3,073,361)

Sambamba na hiyo kuna Mikoa 5 iliyopo mkiani ambayo hali ya vipato kwa wananchi wake ni mbaya sana,mikoa hiyo ni;

1. Shinyanga (1,857,610)

2. Tabora (1,740,554)

3. Dodoma (1,677,901)

4. Singida (1,578,040)

5. Kagera (1,143,992)

MY TAKE;

Hongera Sana wachapa Kazi wa Nyanda za Juu Kusini.

ANGALIZO,

Kwa kweli hali za sisi wananchi ni mbaya, Serikali ijitahidi kuwekeza kwenye uchumi wa watu la sivyo tunakoelekea hali itazidi kuwa mbaya maana na kasi ya kuzaliana ni kubwa mno. Ikumbukwe Tanzania ni kati ya nchi 5 zenye idadi kubwa ya watu na pia zenye idadi kubwa ya maskini barani Afrika.

SOURCE-TANZANIA IN FIGURES 2019.(pg 50-53)

CREDITS-National Bureau of statistics,Ministry of Finance and planning, 2020.
View attachment 1773908
Pale Chadema iliposhamiri pana maendeleo. CCM ni laana inapokita mizizi ni umaskini mtupu.
 
Swala sio watawala ni tu watanzania wengi vichwa vibovu kikiwemo chako

Japan haina raslimali yeyote na ni tajiri hasa sababu private sekta watu wana akili sana

Fikiria familia moja ya TOYOTA inajaza magari Tanzania nzima kila uendapo unakutana na TOYOTA

Wewe na familia yako cha maana mlichogundua na kuzalisha ni nini?
Angalia hiyo distribution ya umaskini na mtawanyo wa ccm vs chadema. Utajua mikoa iliyokumbatia CCM ni mafukara
 
Kila sehemu kuna ardhi mkuu ila wako aggressive kutafuta pesa na ni hard working kweli kweli si wamama si wanaume
Uko sahihi, hawa watu wanapambana kwenye kufanya kazi ni hatari. Kuna kipindi niliona Mbeya inasumbuliwa na malnutrition sana nikashangaa mno kwa kuzingatia hali ya uzalishaji wa chakula, ikabidi nimuulize Sister angu ni Doctor hapo.

Akaniambia changamoto kubwa waliyo nayo watoto wa Mbeya ni kwamba mama zao hawana muda wa kutosha kuwalisha kwa kuwa muda mwingi wapo kwenye utafutaji/uzalishaji na si kwamba wana shida ya chakula.
 
Dah!! We kiumbe unahitaji maombi aisee, sio kwa reasoning hiyo uliyo nayo.

Kwani huyo Bakhresa utajiri wake kaupatia Mwanza pekee? Fine, Bakhresa ni tajiri kwa kuuza juice na vyakula, kwa hiyo na kila anayenunua juice na chakula naye anatajirika kama Bakhresa?! Kati ya mnunuzi na muuzaji ni nani anatengeneza 'utajiri' in the process?
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Swala sio watawala ni tu watanzania wengi vichwa vibovu kikiwemo chako

Japan haina raslimali yeyote na ni tajiri hasa sababu private sekta watu wana akili sana

Fikiria familia moja ya TOYOTA inajaza magari Tanzania nzima kila uendapo unakutana na TOYOTA

Wewe na familia yako cha maana mlichogundua na kuzalisha ni nini?
True mkuu ifike mahala watu tuthubutu kwa ujuzi,maarifa na ubunifu.

Hii biashara ya ulalamishi,lawama,uoga na kusubiria serikali tuiache kabisa.
 
Kwahiyo wewe binafsi unaamini tupo uchumi wa kati??
Mkuu katika kutathmini uchumi wa mtu/taifa wanahusisha hadi vitu vingine ambavyo ukivitazama kwa kawaida haviongezi welfare za watu kimaisha.

Mfano mataifa mengi ya ulaya yanahitaji vifaa kama heating systems na kwa raia wengi wa nchi husika. Sasa ukianza kurecord assets na heater zitahusika ila kiuhalisia haziongezi tija kwenye maisha halisi ila zinaboost figure za kiuchumi.

Nnacho taka kusema ni kuwa, ukijumlisha thamani ya miradi inayoendelea nchini (SGR, Stiegler's Gorge, Ndege nk) lazima figure za kiuchumi kwa taifa zipae. Kwamba miradi hii inaongeza tija kwenye maisha ya raia ama lah, hilo ni jambo jingine kabisa.

Ni kama tu ambavyo Ethiopia inasifika kwa ukuaji wa kiuchumi ila raia wake daily wanakamatwa mataifa mbalimbali wakikimbia hali ngumu ya maisha kwao.
 
Habari zenu wadau!

Mwaka 2020 tulitangaziwa Tanzania kusajiliwa kuwa miongoni mwa nchi ambazo wananchi wake wamefikia kiwango cha Uchumi wa Kati wa chini yaani Lower Middle Income Country.

Hesabu hiyo huwa inazingatia GNI per Capita Income ambayo ina range Kati ya $1'036-$4,045 ,,ambapo kwa Tanzania hapa ni mikoa michache Sana ambayo wananchi wake ndio wako Uchumi wa Kati,yaani wenye kipato kuanzia milioni 3 kwenda juu.

Ifuatayo ni orodha ya mikoa 7 ambayo wananchi wake Wana mapato yaliyofikia hicho kigezo cha Uchumi wa Kati, pato la kila mwananchi kwenye mkoa husika limeanishwa.

Regional Per Capita GDP at Current Market Prices,Tanzania Mainland, financial year 2019.Figures in Million TZS

1. Dar es Salaam (4,529,876)

2. Iringa (3,868,283)

3. Mbeya (3,675,999)

4. Kilimanjaro (3,302,915)

5. Ruvuma (3,288,252)

6. Arusha (3,198,260)

7. Njombe (3,073,361)

Sambamba na hiyo kuna Mikoa 5 iliyopo mkiani ambayo hali ya vipato kwa wananchi wake ni mbaya sana,mikoa hiyo ni;

1. Shinyanga (1,857,610)

2. Tabora (1,740,554)

3. Dodoma (1,677,901)

4. Singida (1,578,040)

5. Kagera (1,143,992)

MY TAKE;

Hongera Sana wachapa Kazi wa Nyanda za Juu Kusini.

ANGALIZO,

Kwa kweli hali za sisi wananchi ni mbaya, Serikali ijitahidi kuwekeza kwenye uchumi wa watu la sivyo tunakoelekea hali itazidi kuwa mbaya maana na kasi ya kuzaliana ni kubwa mno. Ikumbukwe Tanzania ni kati ya nchi 5 zenye idadi kubwa ya watu na pia zenye idadi kubwa ya maskini barani Afrika.

SOURCE-TANZANIA IN FIGURES 2019.(pg 50-53)

CREDITS-National Bureau of statistics,Ministry of Finance and planning, 2020.
View attachment 1773908
sikubaliani na utafiti huo. mikoa uliyoiacha mfano Geita na Shinyanga na Mwanza, kuna mzunguko mkubwa wa pesa which means watu wengi wana pesa mifukono kuliko huko nyanda za juu kusini. wafanyabiashara watakubaliana na mimi. mkoa kama iringa ambako mzunguko n i mdogo sana kuna watu hawana hela mifukoni balaa, sasa sijui uchumi wenu wa kwenye vitabu huo kama unalingana na uhalisia.
 
Mkuu katika kutathmini uchumi wa mtu/taifa wanahusisha hadi vitu vingine ambavyo ukivitazama kwa kawaida haviongezi welfare za watu kimaisha.

Mfano mataifa mengi ya ulaya yanahitaji vifaa kama heating systems na kwa raia wengi wa nchi husika. Sasa ukianza kurecord assets na heater zitahusika ila kiuhalisia haziongezi tija kwenye maisha halisi ila zinaboost figure za kiuchumi.

Nnacho taka kusema ni kuwa, ukijumlisha thamani ya miradi inayoendelea nchini (SGR, Stiegler's Gorge, Ndege nk) lazima figure za kiuchumi kwa taifa zipae. Kwamba miradi hii inaongeza tija kwenye maisha ya raia ama lah, hilo ni jambo jingine kabisa.

Ni kama tu ambavyo Ethiopia inasifika kwa ukuaji wa kiuchumi ila raia wake daily wanakamatwa mataifa mbalimbali wakikimbia hali ngumu ya maisha kwao.
Ni sahihi but taarifa ya hali ya uchumi au house hold survey huwa inaleta picha nzuri zaidi maana kunakuwa na bidhaa na huduma ambazo zimeainishwa kama za lazima ndizo zitaangaliwa na kuleta hitimisho

Hata hivyo Maeneo yenye Per Capita income kubwa huwa yako vizuri kuliko maeneo amabaya hayana kwa hiyo stii hizi parameters ziko reliable na precise kuonesha standard of living ya watu wa maeneo husika.
 
Mikoa ya kusni mbona hawana madini na grits na mwanza kuna mzunguko wa pesa kuliko mikoa ya kusni. Source of your information please, short of that unaweza kuwa umejiandikia tu kadri ya mapenzi ya nafasi yakp. Hivi mahindi ya Njombe na ruvuma yanayouzwa gunis 18,000/- kea gunis ndiyo yafanye hiyo mikoa iwe juu? . Tujengebtabia ya kuhoji chanzo cha taaria , tusiwe tunalishsa fake news. Kazi iendelee!
Vitu vingine tembea ujifunze sio umekaa ndani kama utumbo huku umekumbatia smartphone yako kubisha. Mikoa ya nyanda za juu kusini ina hali nzuri sana za maisha.

Hayo madini umewahi kufatilia yanachangia kiasi gani kwenye pato la taifa? Ni maeneo yenye wachimbaji wadogo tu yenye uzalishaji ndio yanaweza kuongeza tija ya ndani. Hiyo migodi mikubwa, zaidi ya ajira chache na social benefits hamna cha maana tunacho nufaika kwa hayo mamikataba mnayo ambiwa ni siri.
 
sikubaliani na utafiti huo. mikoa uliyoiacha mfano Geita na Shinyanga na Mwanza, kuna mzunguko mkubwa wa pesa which means watu wengi wana pesa mifukono kuliko huko nyanda za juu kusini. wafanyabiashara watakubaliana na mimi. mkoa kama iringa ambako mzunguko n i mdogo sana kuna watu hawana hela mifukoni balaa, sasa sijui uchumi wenu wa kwenye vitabu huo kama unalingana na uhalisia.
Kumbuka hii kitu inahusisha GDP against population sasa hili la mzunguko wa pesa halina mashika hapa.Inawezekana watu wa mijini wakawa na pesa kuliko wengi wa vijijini.

Maisha ya watu wa Nyanda za juu hayategemei maeneo machache ya mijini kama ilivyo kanda ya ziwa.Kwa mfano halmashauri za Iringa na Mbeya unakuta zote zina mapato zaidi ya 3.5b wakati kwa Mikoa ya kanda ya ziwa ni miji ichache ina makusanyo makubwa wakati sehemu zingine hakuna kitu.

Hizi ni takwimu sahihi na mara kadhaa imeripotiwa kanda ya ziwa kuwa na idadi kubwa ya maskini kulinganisha na mnachozalisha na kasi kubwa ya kuzaana inayosababishwa na utamaduni uliopitwa na wakati.Sasa kukubali au kutokubali halinihusu mimi unaweza fanya utafiti wako uka refute huu wa NBS.
 
Back
Top Bottom