Hebu tuiache Biblia itueleze:
Yesu akaondoka huko, akaenda kando pande za Tiro na Sidoni. Na tazama, mwanamke Mkananayo wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa sana na pepo. Wala yeye hakumjibu neno. Nao wanafunzi wake wakamwendea, wakamwomba, wakisema, Mwache aende zake; kwa maana anapiga kelele nyuma yetu. Akajibu, akisema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. Naye akaja akamsujudia, akisema, Bwana, unisaidie. akajibu, akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa. Akasema, Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yaangukayo mezani za bwana zao. Ndipo Yesu akajibu, akamwambia, Mama, imani yako ni kubwa; na iwe kwako kama utakavyo. Akapona binti yake tangu saa ile.
Mathayo 15.21-28
Kwa maneno yasiotatanisha Yesu Kristo anasema kuwa yeye hakutumwa ila kwa "kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli."
Hakuwajia Waarabu, wala Wazungu, wala Wahindi, wala Waafrika, wala Machina.
Kama hayo hayakutosha kuonyesha kuwa yeye hakuwajia wasio Mayahudi anazidi kufahamisha kwa mfano wa kumkata mtu kiu:
Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa."
Ikiwa ipo shaka yo yote katika akili ya mtu kuwa maana ya maneno hayo ni kuwa Yesu anasema kuwa hakutumwa kwa kabila nyengine zo zote ila Waisiraili tu na atazame mwenye shaka tafsiri kubwa kabisa ya Wakristo inayoeleza maana wazi maneno ya Biblia, The Interpreter's Bible, sahifa 441 jalada VII ambamo imeandikwa hivi:
"Yaonekana wazi kuwa Yesu hakika aliamini kuwa ujumbe wake kwanza na khasa ni kwa watu wake mwenyewe." Ndio maana alisema:
Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua.
Mathayo 7.6
Mbwa na nguruwe ni watu wa mataifa yasiyokuwa wana wa Israili. Ukristo haufai kufundishwa watu wo wote isipokuwa Mayahudi.