Rekodi yangu bora kimasomo haijaniwezesha kupata ajira. Naathirika Kisaikolojia

Mpango wa kipumbavu. Angalia kwanza mwelekeo wa mtoto wako na sio kumlazimisha afanye unachotaka wewe. Wazazi kama wewe ni wabinafsi wanaojijali wao tu.
Unazungumzia mwelekeo? Unafikiri kila mtoto anamwelekeo? Kwanza mtoto wa kitanzania/Kiafrika anatoa wapi mwelekeo?? Huoni akinamwigulu wanafosi kuingiza watoto wao kwenye mfumo wa siasa unadhani huo ndio mwelekeo wao? Bro, hapa ni Africa, ukiplaya kizungu unaambulia manyoya.
 
Unasoma ili uelimike, na si uajiriwe.
Hata wewe unasema tu lakini mentality yako inagoma. Tumekuwa tukijua unaenda shule kusoma tuje tuajiriwe tulipwe vizuri tuishi maisha kama akina fulani. Tuliambiwa hivo nyumbani na wazazi, hadi na walimu shuleni na wahadhiri vyuoni.

Waliojua mapema habari za kuelimika waliishia la7 wakajua kusoma na kuandika kisha wakazama mtaani kuuface uhalisia. Ndio waajiri wenu hivi sasa.
 
Ulidanganywa, za kuambiwa changanya na zako.
 
True true..
 
Ondoa akilini mwako kuwa wewe ni kipanga. Kuna wenye rekodi bora kuliko hiyo yako na bado mambo hayajakaa sawa. Maisha nje ya darasa yako complicated sana. Wajanja wote walishaona muhimu ni kupata hela na sio vinginevyo. Fanya kazi yoyote ya halali iliyoko mbele yako. Vyeti hifadhi sehemu salama kwa wakati huu. Halafu kuajiriwa sio suluhisho kwa 100% ya changamoto zako. Unaweza ukapata ajira mshahara ni chini ya Tsh 3m ukaishia kuteseka kwenye ajira. Kwa hiyo elimu yako ukiamua kuwa mfanyabiashara unaweza ukafanya vizuri zaidi.
 
Uliwekeza kwenye kukariri mambo ya vitabu yasiyo na Tija ukasahau kuwekeza kwenye maarifa ya Maisha na connection
😊☺️😅 Hii comment nimecheka Sana Ila nimecheka kwa mazuri sio kwa ubaya.

Ulicho kieleza ndio uhalisia ulivyo kwa Sasa duniani na popote.

NB.
Kuna jamaa angu mmoja ni mshikaji aliwai kunialika alikua anafanya TEACHING PRACTICE (TP) kwenye hiyo shule yule bwana mdogo alikua anafundisha HISTORY kwa kiwango Cha juu Sanaa.

Huko chuoni kwao walikua wamempa nickname ya PROFESSOR Ila jamaa mpaka leo hii yupo nje ya mfumo Hana ajira ya ualimu kwa miaka 10 Sasa..

Uone Sasa Maisha ni sometimes luckiness dogo mmoja mzembe mzembe hakua hata na uwezo mzur sanaa yeye kasoma language akapata kazi huyu mwingine professor still yupo mtaa anapambanaa..

Hatunaa budi kubadilisha mindset zetu dunia imesha badilika Sasa inabidi wasomi wawe job creater not job seekers.



Kwa Sasa kijijini
MPUMBWI
 
SUA form 4 fresh hawapokelewi labda vyuo vya LITA na MATI
 
Ebu tuanzie hapa mkuu job creators wa uchuuzi ama?? Maana tunachofanya ni kuuza biashara za wenzetu(maproducer China, Japan and so on)
 
Hahaaaa
Engineer tuliza ndonga hiyo ,
Wengine sekondari tulikuwa T.O kabisa na tumebomoa first class za Engineering Ila kazi tunafanya tofauti kabisa na tulivyosomea
Nchi ngumu hii mkuu
Mimi ni Electrical Engineer lakini ni dalali sasa hivi town hapa
Bongo miyeyusho sana hii ,sometimes elimu ya juu ni kama westage ya muda na resources , nahisi ningekuwa mbali sasa hivi kiuchumi kama ningefanya kuanza shughuli yangu hii baada ya kumaliza form four Tu
 
Cha kukushauri sina zaidi ya kukwambia funga mkanda mdogo angu! Hapo hujapata shida, shida zinakuja na mateso mengi mpaka utajuta kuzaliwa! Na hazitokwisha mpaka siku ya mwisho! Mimi saizi ndo nmeelewa Mbaraka Mwinshee aliimba nini wallah
NB: Shida sio pesa tu au kazi!
 
Acha visingizio wewe how old are u? Il mradi huko Hai mda bado nao unavosema ulipoteza mda wapi??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…